Mambo yanayopunguza malipo ya funga au swaumu

Mambo haya yanaweza kuharibu funga ya mtu ama kupunguza malipo ya funga.

Yanayoharibu au Kupunguza Thamani ya Funga


Yanayoharibu funga ya mtu au kupunguza thamani yake ni kujiingiza katika mazungumzo yaliyokatazwa kama vile kusengenya, kusema uwongo, kupiga porojo, n.k., na kujiingiza katika matendo maovu. Japo mtu mwenye kufanya matendo haya atajiona amefunga kwa vile atakuwa hajala, au hajanywa au hajafanya kitendo chochote katika vile vinavyobadtilisha funga atakuwa hana funga au hakupata malipo ya funga kwa ushahidi wa Hadith ifuatayo:


Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Yoyote yule ambaye hataacha mazungumzo mabaya na vitendo viovu, Allah (s.w) hana haja na kuacha kwake chakula chake na kinywaji chake (Allah (s.w) hatapokea funga yake). (Bukhari).


Wakati mmoja Mtume (s.a.w) aliwaamuru watu wawili wafuturu (wavunje funga) kwa sababu walikuwa wanasengenya.
Wanachuoni wameshindwa kutoa uamuzi kuwa mtu akizungumza maneno maovu na machafu au akijiingiza katika matendo maovu, atakuwa amefungua kwa sababu ni vigumu kujua matendo ya ndani ya mtu. Hivyo, japo hapatakuwa na mtu yeyote atakayekuambia umefungua kwa kufanya vitendo viovu, wewe mwenyewe ujihesabu kuwa hukupata kitu kutokana na funga yako kama Mtume (s.a.w) anavyotufahamisha katika hadith ifuatayo:


“Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Ni watu wangapi wanaofunga, lakini hawana funga ila huambulia kiutu ...” (Darimi).
Mfungaji anatakiwa, ili funga yake iweze kutimia na kufikia lengo, ajiepushe na mambo yote maovu na machafu. hata akichokozwa na mtu, ajiepushe kugombana naye kwa kumwambia, “Nimefunga, nimefunga” kama anavyotushauri Mtume (s.a.w):


Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Wakati mmoja wenu atakapoamka akiwa amefunga, asitumie au asitoe lugha chafu na asifanye matendo maovu. Na kama yeyote yule anamchokoza au anagombana naye, hana budi kusema: “Nimefunga, nimefunga.”

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1973

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe

Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio.

Soma Zaidi...
Maswali juu ya Mambo anayopaswa kufanyiwa maiti ya muislamu

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kwanini wengi wanaohijji hawafikii lengo la hijjah zao

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nini maana ya funga na ni lipi lengo lake

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la funga na maana yake katika uislamu.

Soma Zaidi...
Umuhimu na nafasi za hijjah katika uislamu

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...