Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
4.2. Maana ya Kusimamisha Swala.
Ni kuswali kwa kutekeleza kikamilifu nguzo, sharti zote za swala na kuwa na unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.
Nafasi na Umuhimu wa Kusimamisha Swala katika Uislamu.
Swala imesisitizwa na ina umuhimu katika Uislamu kwa sababu zifuatazo;
Kusimamisha Swala ni Amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Mwenyezi Mungu (s.w) ameamrisha waumini (waislamu) wote wasimamishe swala zote za faradh na sunnah ipasavyo.
Rejea Quran (29:45), (4:103) na (14:31).
Kusimamisha swala ni nguzo ya Pili ya Uislamu.
Baada ya shahada mbili, nguzo ya pili na ya msingi mno katika Uislamu ni kusimamisha swala.
Swala humtakasa muislamu na mambo machafu na maovu.
Bila shaka swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mja na mambo machafu na maovu.
Rejea Quran (29:45).
Swala ni amali ya mwanzo kabisa kuhesabiwa siku ya Qiyama.
Swala ya muumini ikitengemaa vizuri ndio sababu ya kufaulu kwake Duniani na Akhera pia.
Rejea Quran (23:1-2,9), (87:14-15) na (22:34-35).
Kutosimamisha swala ni sababu ya mtu kuingizwa motoni.
Hii ni baada ya muislamu Kupuuza swala kwa kutozingatia sharti na nguzo zake kikamilifu na kukosa unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.
Rejea Quran (74:42-47), (68:42-43) na (107:4-5).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...