Ni zipi siku ambazo ni haramu kufunga? na ni kwa nini hairuhusiwi kufunga katika siku hizo
Siku Zilizoharamishwa Kufunga Sunnah
(i)Siku kuu za Iddil-Fitri na Iddil-Hajj
Imeharamishwa kufunga katika siku hizi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Abu Sayyid al-Khudri (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema: Hakuna funga katika siku mbili - siku ya (Iddil) Fitr na siku ya (Idd ya) kuchinja.” (Bukhari na Muslim).
(ii)Siku za Tashriq
Siku za Tashriq ni mwezi 11 hadi 13 Dhul-Hijjah. Ni haram kufunga
katika siku hizi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Ibn Al-Hazali(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Siku za Tashriqu ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka Allah (s.w) (kwa Takbira). (Muslim).
(iii)Siku ya Shaka
Siku ya Shaka ni siku moja kabla ya Ramadhani. Yaani mwezi 30 Shaabani ambapo inawezekana ikawa ni siku ya kufunga. Mtume (s.a.w) amekataza kufunga sunnah katika siku hii ya mashaka ila kwa yule mwenye ada ya kufunga. Kwa mfano mtu mwenye ada ya kufunga Jumatatu ameruhusiwa kufunga endapo siku hiyo itaangukia Jumatatu. Hadith ifuatayo inabainisha makatazo haya:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume wa Allah amesema: “Usifunge siku moja au mbili kabla ya Ramadhani ila kwa mtu yule mwenye ada ya kufunga funga fulani (k.m. funga ya Alhamisi), yeye anaruhusiwa kufunga ” (Muslim).
Inatakiwa siku moja au mbili kabla ya Ramadhani tusifunge ili tuweze kuukabili tukiwa na nguvu mpya na ili tutofautishe funga ya Ramadhani na funga za Sunnah.
(iv) Siku ya Ijumaa
Mtume (s.a.w) amekataza funga ya Sunnah katika siku ya Ijumaa tu, lakini kama mtu ana tabia ya kufunga sunnah, ikatokea siku ya Ijumaa ni miongoni mwa siku anazofunga, basi hapana ubaya. Tunajifunza haya katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Na asifunge siku ya Ijumaa yeyote miongoni mwenu; ila tu akiwa ameanza kufunga kabla yake au ameendelea kufunga baada yake”. (Muslim).
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Usiuchopoe usiku kabla ya Ijumaa ukafanya usiku pekee kwa kusimama kwa swala na usiichague siku ya Ijumaa pekee kati ya siku za wiki kuwa ndio siku ya kufunga, ila kama mmoja wenu ana tabia ya kufunga sunnah na ikatokea siku ya Ijumaa imeangukia katika tarehe anayopaswa kufunga. ” (Muslim).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Vituo vya kunuia hijjah au umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?
Soma Zaidi...Jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa
Kutawadha ni katika ibada muhimu za mwanzo kutakiwa kuzijuwa na ni lazima. Swala yako haitaweza kutimia bila ya kujuwa udhu. Inakupasa kujuwa nguzo za udhu, yanayoharibu udhu na namna ya kutawadha kifasaha. Hapa utajifunza hatuwa za kutawadha
Soma Zaidi...Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa
- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.
Soma Zaidi...