Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji wengi?
Pamoja na waislamu wengi kujizatiti katika kufunga mwezi wa Ramadhani na funga zingine za sunnah, lakini wengi wao hafikii lengo la funga kwa sababu zifuatazo;
Wengi wafungao hawajui lengo la funga.
Wafungaji wengi hufunga kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio kuwa wacha-Mungu kama lilivyo lengo la funga.
Rejea Quran (2:183).
Wafungaji wengi chumo lao ni la haramu.
Waislamu wengi wafungao chakula chao, futari yao na daku zao zinatokana na chumo la haramu ambalo ni sababu ya kutopata matunda ya funga zao.
Kutofahamika lengo la maisha na uhusiano na lengo la funga.
Waislamu wengi hutekeleza ibada maalumu kama swala, funga, n.k na kuona kuwa ndio lengo kuu la maisha yao na kuacha nyanja zingine za maisha yao.
Rejea Quran (51:56).
Wengi wafungao hawazingatii miiko na sharti za funga zao.
Waislamu wengi wafungao huishia kushinda njaa na kiu bila kupata faida ya funga zao kwa kutojizuilia na mambo maovu, machafu, laghawi, upuuzi, n.k.
Wengi wafungao hawatekelezi nguzo na sunnah za funga ipasavyo.
Pamoja na waislamu wengi kufunga, lakini wengi wao hawaswali kabisa swala za faradh na sunnah na kubakia kufuata mkumbo kwa kushinda na njaa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya jamaa na taratibu zake.
Soma Zaidi...Nguzo za imani, maana ya sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha
Soma Zaidi...Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kuona jinsi ya kuzitathmini swala zetu.
Soma Zaidi...