Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kijahili
i. Wanawake walikuwa na kazi na nafasi ya kuwastarehesha wanaume tu, yaani ukahaba na umalaya.
ii. Wanawake walikuwa watumishi kwa ajili ya kutunza na kuangalia sifa (afya)
za mabwana zao.
iii. Wanawake pia walikuwa na jukumu kubwa la kuzaa na kulea watoto kwa ajili ya mabwana zao.
iv. Wanawake walinyimwa na kunyanyaswa haki zao kiuchumi na kijamii na kufanywa amtegemee mume moja kwa moja.
v. Talaka haikuwa na nafasi yeyote, mwanamke alilazimika kuishi na mumewe mpaka afe hata kama hawaelewani.
vi. Ndoa za kuolewa mwanamke baada ya kuachwa hazikuwa na nafasi, zilichukuliwa kama uzinzi wa aina yake, (civilized adultery).
vii. Heshima na usawa katika ya mwanamume na mwanamke haikuwepo, heshima ilizingatia maumbile na hadhi ya mwanamke ndani ya jamii.
viii. Mwanamke alikuwa huru kuchanganyikana na wanaume jambo ambalo lilichochea umalaya, ukahaba na kuharibika maadili.
Hifadhi ya Mwanamke na Hekima yake Katika Uislamu
i. Wanawake wana uhuru wa kutoka majumbani mwao kwa kutekeleza haja maalum ili kuchunga heshima yao na kuepusha uchochezi wa zinaa, n.k.
Rejea Qur’an (33:59)
ii. Wanawake kulingana na umbile lao na jukumu lao la kuzaa na kulea, wana haki ya kulindwa heshima yao na kuhifadhiwa majumbani.
Rejea Qur’an (33:33)
iii. Wanaume kuwa viongozi wa wanawake, si kuwa wao ni bora kuliko wanawake, bali wanaume wana kuwa ni walinzi, wahifadhi na viongozi wao.
iv. Kutokana na fursa ya vipaji na vipawa alivyonavyo mwanaume juu ya mwanamke, analazimika kusimamia na kuongoza majukumu mengi zaidi.
v. Kulingana na asili ya maumbile, wanawake hawawezi kuwa sawa kikazi, kimajukumu, kimavazi, kimahusiano, n.k.
Rejea Qur’an (33:36), (24:31), (24:60)
Haki za Mwanamke Katika Uislamu
i. Haki ya mwanamke kupata elimu
- Kujielimisha ni amri kwa wanaume na wanawake, sio wanaume pekee.
Rejea Qur’an (96:1-5)
ii. Haki ya mwanamke katika sitara
- Ni haki kwa mwanamke kupata kulingana na asili ya maumbile yake.
Rejea Qur’an (33:59), (24:31)
iii. Haki ya mwanamke katika uchumi
- Kama ilivyo kwa mwanamume ana haki ya kuchuma na kumiliki uchumi, mwanamke pia ana haki hiyo.
Rejea Qur’an (4:32), (4:4)
iv. Haki ya mwanamke katika jamii (ndoa, mirathi na talaka)
- Mwanamke ana haki ya kuolewa na mwanamume anayemridhia kwa kuzingatia sheria za Kiislamu kwa hiari.
- Mwanamke ana haki ya kumuacha mume atakayeshindwa kuishi naye na kufikia lengo la ndoa. Mfano talaka ya I’laa, Khul’u, Mubaarat, n.k.
- Haki ya mwanamke mjane au aliyeachwa kuolewa tena na wanaume wanaowapenda kisheria.
- Mwanamke ana haki na fungu la kurithi kama alivyo mwanamume pindi mmoja wapo atakapokufa.
Rejea Qur’an (4:7)
v. Haki ya mwanamke katika sheria
- Mwanamume na mwanamke wana haki sawa mbele ya sheria katika kuhukumiwa, kuadhibiwa, kudai haki, n.k. bila ya ubaguzi wowote.
Rejea Qur’an (5:38), (24:2)
- Mwanamke kama mwanamume, ana haki ya kutoa ushahidi mahakamani pale inapobidi.
Rejea Qur’an (2:282)
vi. Haki ya mwanamke kushiriki katika uongozi na siasa
- Jukumu la kuendesha maisha ya jamii liko kwa mwanamume na mwanamke katika kuamrisha mema na kukataza mabaya.
- Suala la uongozi wa kifamilia na kijamii ni la wote, mwanamume na mwanamke isipokuwa mwanamke haruhusiwi kuwa kiongozi wa nchi.
Rejea Qur’an (9:71), (58:1-4)
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi.
Soma Zaidi...Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali.
Soma Zaidi...Swala ya Dhuha ni swala ya sunna inayosaliwa wakati wa asubuhi baada ya jua kuchomoza na kupanda angalau kiasi cha mkuki (takribani dakika 15 baada ya jua kuchomoza) mpaka kabla ya adhuhuri. Ingawa hakuna sura maalum zilizowekwa kisheria, Mtume ﷺ alisoma baadhi ya sura zenye maana ya kuhimiza kheri na shukrani.
Soma Zaidi...Haki za UchumiKuwa imara kiuchumi ni sababu mojawapo kubwa ya kumpa mtu hadhi katika jamii.
Soma Zaidi...Kustawi kwa Kampeni ya Kudhibiti UzaziMiongoni mwa sababu zilizosaidia kustawi kwa kampeni hii ni matokeo ya mapinduzi ya viwanda (Industrial revolution) ya huko Ulaya.
Soma Zaidi...