haki na wajibu kwa watumishi wa nyumbani (house boy and house girl)

haki na wajibu kwa watumishi wa nyumbani (house boy and house girl)

Wajibu kwa Watumishi wa Nyumbani



Mara nyingi katika familia panakuwa na watumishi wanaoajiriwa kusaidia kufanya kazi mbali mbali za nyumbani kama vile uyaya, upishi, utunzaji bustani, udobi, na kadhalika. Uislamu umetukumbusha kuwa mtu kupata wasaa wa kuweka mtumishi wa nyumbani au katika sehemu yeyote ile, sikuwa yeye ni bora kuliko huyo mtumishi, bali ni katika utaratibu wa Allah (s.w) kuwa amewafadhilisha baadhi ya watu juu ya wengine ili wapate kutegemeana. Kama hivi, tajiri anamuhitajia mtumishi na mtumishi anamuhitajia tajiri. Kila mmoja ni muhimu kwa mwingine. Ni katika msingi huu tunawajibika kuwatendea wema watumishi kama ndugu zetu kama inavyohimizwa katika Hadith zifuatazo:
Abdullah bin Omar (r.a) ameeleza kuwa alikuja mtu mmoja kwa Mtume wa Allah na kuuliza, "Ee Mtume wa Allah ni mara ngapi tutamsamehe mtumishi? Mtume alinyamaza kimya. Kisha akamuuliza tena swali lile lakini Mtume (s.a.w) alibaki kuwa kimya. Lilpoulizwa swali lile kwa mara ya tatu Mtume al/ibu: "Msamehe mara sabini (70) kila si/cu." (Abu Daud)



Abu Dharr ameripoti kuwa Mtume wa Allah amesema: "Allah (s.w) amewajaalia ndugu zenu kuwa chini ya mikono (mamlaka) yenu. Yeyote yule atakayejaaliwa kuwa na mamlaka juu ya ndugu yake, basi na amlishe chakula anachokula yeye, na amvishe kivazi anachovaa yeye na asimpe kazi zinazomzidi kimo (uwezo). Kama atampa kazi zilizo nje ya uwezo wake basi na amsaidie." (Bukhari na Muslim)



Hadithi hizi zinatufundisha kuwa tuishi vizuri na watumishi wetu na wale tunaoishi nao katika familia walio chini ya milki yetu. Tunafundishwa kuwa wakitukosea tusiwanyanyase na kuwapatiliza bali tuwasamehe na kuwaongoza. Vile vile tunawajibika kuwalipa watumishi wetu kwa uadilifu kwa mujibu wa mkataba wa kazi na tusiwaongezee kazi nje ya zile zilizo katika mkataba. Kwa ujumla, tunawajibika kuishi kindugu na wale walio katika miliki zetu katika familia kwa kuwapa kazi zinazolingana na uwezo wao, kuwapa msaada katika kazi zilizo wazidi kimo na kuwahudumia kwa chakula, mavazi na malazi katika kiwango kile kile tunachojihudumia wenyewe na watoto wetu.



Kuwanyanyasa na kuwafanyia ukatili watumishi wetu na wale tunaokaanao chini ya milki zetu ni katika makosa makubwa mbele ya Allah (s.w) na ni mkosi kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo: Abu Bakr Siddiq (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Hataingia peponi yule anayewatendea vibaya (anayewafanyia ukatili) wale walio chini ya mamlaka yake." (Tirmidh, Ibn Majah).



Raafi 'I bin Makiith (r. a) arneeleza kuwa Mturne wa Allah am eserna: "Kuwatendea wema watu waliochini ya mamlaka yako huleta baraka(fortunes) na kuwafanyia ukatili vi urn be chini ya mamlaka yako, huleta rnikosi (misfortunes)" (Abu Daud). Pamoja na kuzingatia mafundisho ya Hadithi hizi hatunabudi kumuangalia Mtume (s.a.w) ambaye ni kiigizo chetu, namna alivyokuwa akiwatendea wema watumishi wake, katika Hadith zifuatazo:



Anas (r. a) ameeleza: "Nilianza kumtumikia Mtume wa Allah nilipokuwa mvulana wa miaka tisa. Nilimtumikia kwa miaka kumi. Hakunigombeza kwa chombo chochote nilichovunja. Pale yeyote katika familia yake alponigombeza kwa hili au lile alikuwa akimwambia: Mwache kwa sababu, kila kitu kimekadiriwa mwisho wake, ni lazima kiondoke." (Baihaqi).


Vile vile katika Hadithi nyingine Anas (r.a) anaeleza:
Mtume wa Allah alikuwa mbora wa watu katika tabia. Siku moja alinituma mahali. Kwa jina la Allah nilisema, 'Sitaenda' lakini, katika mawazo yangu nikaona sinabudi kwenda aliponituma Mtume wa Allah. Kisha nilitoka kwenda. Njiani nikakutana na watoto waliokuwa wakicheza katika maeneo ya sokoni.Nikiwa pale, Mtume wa Allah alikuja nyuma yangu na kunishika mkono.Nilipogeuka na kutazama nikaona ni Mtume wa Allah Akaniuliza, huku akitabasamu, "Ee mpendwa Anas! Umeshakwenda kule nilikokutuma?" Nil j/ibu: "Ndio Ee Mtume wa Allah, ninakwenda" (Muslim)



Tunajifunza kutokana na Hadith hizi kuwa hatunabudi kuwatendea wema watumishi wetu na wale wote waliochini ya mamlaka yetu katika familia. Katika kusisitiza hili turejee tena Hadithi aliyosimulia Aysha (r.a) kuwa amemsikia Mtume (s.a.w) akisema:
Mbora miongoni mwenu ni yule aliye mbora katika (kuwatendea wema) familia yake na (mimi) ni mbora wenu katikafamilia yangu..." (Ibn Majah)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1143

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 web hosting    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Jinsi ambavyo msafiri anatakiwa aswali akiwa safarini

Postvhiibinakwenda kukufundisha kuhusu swala ya msafiri na jinsi ya kuiswali.

Soma Zaidi...
Taratibu za kumuona mchumba katika uislamu

Hspa utajifunza taratibu za kuonana na mchumba katika uislamu.

Soma Zaidi...
Adhabu ya mzinifu katika jamii ya kiislamu

(iii) Adhabu ya UzinifuKatika Sheria ya Kiislamu mtu haadhibiwi mpaka atende kwa uwazi matendo yenye kuvuruga utaratibu na amani ya jamii.

Soma Zaidi...
Sifa nyingine za kuchaguwa mchumba ambazo watu wengi hawazijui

Hizi ni sifa za ziada za mchumba katika uislamu. Sifa hizi wengi hawazijui ama hawazingatii.

Soma Zaidi...
Shart kuu nne za swala

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu masharti ya swala.

Soma Zaidi...
Umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu

Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nguzo za kufunga ramadhani

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...