Masharti ya Swala ya Maiti
Masharti ya swala ya maiti ni yale yale ya swala ya kawaida kwa wenye kumswalia maiti bali kwa maiti mwenyewe kuna masharti yafu atayo:
(i) Maiti awe Muislamu kwani Allah (s.w) amesema:“Wala usimswalie abadan mmoja wao (makafiri na wanafiki) yeyote akifa”. (9:84)
(ii)Maiti awe ameshaoshwa.
(iii)Maiti awekwe mbele ya wanaomswalia. Lakini pia inajuzu kumswalia maiti ambaye hayupo,swala ya ghaibu. Maiti zikiwa nyingi zitapangwa mbele za kiume zikiwa karibu na Imamu, kisha zitaswaliwa swala moja tu.
(iv)Maiti asiwe shahidi.Kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (s.a.w) watu waliokufa katika vita vya kupigania dini ya Allah (s.w) hawaoshwi wala kuswaliwa.Mtume (s.a.w) aliamuru Mashahidi katika vita vya Uhud wasioshwe wala wasiswaliwe. (Abu Daud).
Nguzo za Swala ya Maiti
Nguzo za swala ya maiti ni tofauti kidogo na zile za swala ya kawaida. Tofauti na swala ya kawaida, swala ya maiti ina kusimama tu, hakuna rukuu, sijda wala vikao. Nguzo za swala ya maiti ni hizi zifuatazo:
1. Nia.
2. Takbira ya kuhirimia
(Takbira ya kwanza) anavyoswaliwa katika swala ya
kawaida
3. Kusoma suratul fatiha
4. Kuleta takbira ya pili
5. Kumswalia Mtume(s.a.w) kama
6. Kuleta takbira ya tatu.
7. Kumuombea dua maiti
Kuleta takbira ya nne
8. Kutoa salaamu
Sunnah za Swala ya Maiti
Nguzo za swala ya maiti ni hizi zifuatazo:
1.Kusoma Audhubillah kabla ya Al-fatiha.
2.Kusema Amin baada ya Al-fatiha.
3.Kuyasema yote yanayosemwa katika swala hii kimya kimya, ila Imamu atatoa Takbira Nne naSalam kwa sauti. Iswaliwe jamaa na safu ziwe witri; 1, 3, 5, 7, 9, n.k 4.Kuwaombea Waislamu wote dua pamoja na maiti. Baada ya Takbira ya Nne na kabla ya Salaam kuomba dua ifu atayo:
“ Alahumma laatahrimn aa ajrahu, walaataftinaa ba’adahu”
“Ewe Mwenyezi Mungu, usitunyime malipo yake na usitujaribu baada yake.”
5.Kutoa Salaam ya kwanza na ya pili kwa ukamilifu wake.
6.Imamu kusimama karibu na kichwa cha maiti ya kiume na kusisima karibu na kiuno (nyonga) ya maiti ya kike.
Namna ya Kutekeleza Swala ya Maiti
Utaratibu wa kusimamisha swala ya maiti ni kama ifuatavyo:
1. Maiti iwekwe mbele.
2. Imamu asimame katikati ya mwili wa maiti kama maiti ni ya kike na asimame sawa na mabega kama maiti ni ya kiume.Iwapo maiti zinazoswaliwa ni zaidi ya mmoja zipangwe moja mbele ya nyingine .Maiti za kiume zikiwa karibu na Imamu.
3.Wanaomfuata Imamu wasimame kwenye mistari yenye idadi ya witri; 1, 3, 5, 7, n.k.
4.Baada ya kusimama hivyo swala itaanza na kuendelea kama ifuatavyo:
(i)Nia - nia ya kumswalia maiti iliyo mbele huwekwa moyoni (si lazima kutamka).
(ii)Kisha nia hii huambatanishwa na Takbira ya kwanza - Takbira ya kawaida ya kuanzia swala - nayo ni kusema: Allahu Akbar.
(iii)Imamu na Maamuma watasoma Suratul Fatiha kimya kimya.
(iv)Baada ya kuimaliza Suratul- Fatiha Imamu atasema tena Allahu Akbar na Maamuma watafuatisha hivyo hivyo - bila ya kuinua mikono.
(v)Imamu na Maamuma watamswalia Mtume (s.a.w) kimya kimya kama ilivyo katika tahiyyatu ya mwisho ya swala ya kawaida.
(vi)Baada ya kumswalia Mtume, Imamu atasema tena - Allahu Akbar na Maamuma watafuatisha hivyo hivyo kimya kimya bila ya kuinua mikono.
(vii)Kisha kimya kimya maiti huombewa dua yoyote ile katika zile alizotufundisha Mtume (s.a.w). Moja kati ya dua hizo ni hii iliyosimuliwa na Abu Hurairah na kupokelewa na Maimamu wa hadith - Ahmad, Abu Daud, Timidh na Ibn Majah.
(viii) Baada ya dua hii imamu atasema tela Allahu Akbar na maamuma watafanya vivyo hivyo bila ya kunyanyua mikono.
(ix) Waombewe dua waislamu wote dua ifuatayo inaweza kutumika:
"Rabbana ighfir lanaa wali-ikhwaaninal-lladhiina sabaquuna bil-iiman, walaa taj-'al fii quluubinaa ghilal-Lilladhiina aamanuu, Rabbanaa in-naka ra-ufur-rahiim"
“... Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia (kufa) katika Imani (ya Kiislamu). Wala usijaalie katika nyoyo zetu uadui kuw afanyia Wa is lamu wenzetu. Mola wetu! Hakika wewe ni Mpole sana, mwenye Rehma mno”. (59:10)
(x) Baada ya dua hii itatolewa Salaam ya kumaliza swala na ni bora kuirefusha kidogo kuliko ile ya swala ya kawaida kwa kusema: "As-salaamu 'alaykum warahmatulllahi wabarakaatuh.
Amani iwe juu yenu na Rehma za Allah na Baraka zake.
Swala ya maiti pia inaweza kuswaliwa kwa ghaib, yaani bila ya kuwa na jeneza mbele. Mtume (s.a.w) mara kadhaa katika maisha yake, aliongoza swala ya maiti wa mbali na karibu waliokwisha zikwa kama tunavyofahamishwa katika Hadith zifu atazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuw a Mtume wa Allah (s.a.w) alitoa habari za kifo cha Najashi (Mfalme wa Uhabeshi) kwa watu katika siku aliyokufa, akaenda nao katika sehemu ya kuswalia, akafanya mistari pamoja nao kisha akapiga takbira nne (yaani akaongoza swala ya Jeneza). (Bukhari na Muslim).
Ibn Abbas (r.a)amesimulia kuw a Mtume wa Allah alipita karibu na kaburi alimozikwa maiti usiku uliopita. Akauliza: Ni wakati gani alizikwa? Walijibu: Usiku uliopita. Akauliza: Kwa nini hamkunifahamisha? Walijibu: Tulizika katika giza la usiku. Kwa hiyo hatukupenda kukuamsha usingizini. Kisha alisimama na tukaunda mistari nyuma yake akaiswalia maiti ile. (Bukhari na Muslim).
Kusindikiza Jeneza
Baada ya maiti kuswaliwa jeneza litaongozwa kuelekea kaburini. Inatakiwa Waislamu walisindikize jeneza; wasiliweke mpaka likalishwe chini. Pia Mtume (s.a.w) ametuamrisha kusimama tutakapoona jeneza likipitishwa:
Jabir (r.a) amesimulia: Wakati Jeneza lilipokuwa linapita, Mtume (s.a.w) alisimama nasi pia tukasimama pamoja naye. Tukauliza: Ewe Mtume wa Allah! Hakika huyo ni Myahudi. Akasema: “Hakika kifo ni tishio. Kw a hiyo w akati wote mtakapoona Jeneza likipita simameni”.(Bukhari
Maandamano ya mazishi yawe kimya kimya.Kumsindikiza maiti kwa muziki na vilio ni haramu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 14830
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitabu cha Afya
hizi ndio nguzo za swala, swala za faradhi na suna
Soma Zaidi...
Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii
Soma Zaidi...
Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s. Soma Zaidi...
Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir Soma Zaidi...
Ni ipi hukumu ya kutoa talaka hali ya kuwa umelazimishwa au ukiwa umerukwa na akili
Endapo mtu atamuacha mke pasi na ridhaa yake yaani amelazimishwa ama amemuwacha wakati amerukwa na akili. Je ni ipo hukumu yake. Soma Zaidi...
Haki za mwanamke katika uislamu
Soma Zaidi...
Msimamo wa uislamu juu ya utumwa
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa. Soma Zaidi...
umuhimu wa swala katika uislamu
Soma Zaidi...
Aina ya biashara zilizo haramu kwenye uislamu
Hapa utajifunza aina za biashara ambazo ni haramu. Soma Zaidi...
Mirathi Katika Uislamu, nani anarithi na ni mambo gani ya kuzingatia kabla ya kirisisha
Soma Zaidi...
Jinsi uislamu ulivyokomesha biashara ya utumwa wakati na baada ya mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...