image

WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 1

Post hii inahusu zaidi hadithi mpya na nzuri inayoitwa wakati wa Kufumbuka, ni hadithi inayohusu maisha ya kawaida ambapo watu ushindwa kudhamini watu wa karibu nao na kuona watu wa mbali ndio wenye maana ila shida zikifika ndipo wanaona umuhimu wao.

Wakati wa Kufumbuka.

Palikuwemo na familia Moja ya Mzee aliyejulikana kwa jina la Mzee maganga, huyu Mzee katika ujana wake alifanikiwa kuwa na Mali nyingi kwa wakati huo Mali hizo zilikuwa ni ngombe,punda, mashamba ya miwa, mbuzi,mashamba ya mpunga, katani, pamb, kuku,sungura, punda na mashamba makubwa sana ambavyo vili mwingizia kipato na kumfanya apate umaalufu na kupendwa na ndugu wa karibu na pia wa mbali,  kwa hiyo ndugu walikuja wengi kutafuta Makazi na kupata chakula na waliweza kuishi kwenye nyumba ya Mzee maganga bila shida na kupata mahitaji yote kwa sababu nyumba zilikuwemo za kutosha .

 

 

 

Ilitokea Mzee Maganga alifanikiwa kuoa  mke mmoja aliyeitwa maria ,kwa sababu Mzee maganga alikuwa muumini mzuri wa kanisa katoliki pamoja na utajiri wake wote alipaswa kuwa na mwanamke mmoja tu, kwa bahati mbaya mwanamke wake alitoka kwenye familia ambayo wazazi wake wote walikuwa wameshafariki kwa hiyo maria alikuwa mtoto wa kwanza kwenye familia akiwa na mdogo wake ambaye alikuwa na uwezo wa kawaida ila baada ya maria kuolewa na Maganga aliweza kumsaidia vitu vidogo vidogo kama vile chakula na nguo.

 

 

 

 

Kwa ujumla Tabia ya Mzee maganga ilikuwa na kuchapa kazi usiku na mchana na pia aliwafundisha watoto wake na ndugu zake walioishi pamoja naye kufanya kazi, na pia kipato chake kiliongezeka kila siku kwa sababu ya utajiri wake alipendwa na watu wengi ila changamoto moja kwa Mzee Huyu ni kwamba alikuwa anapendelea sana upande wa familia yake alikuwa hapendi upande wa mwanamke wake kwa hiyo ndugu wote wa upande wa kwake walisoma na kupata vyeo vya juu na pia maria alimwomba msaada ila aweze kumsaidia mdogo wake lakina Mzee maganga hakukubaliana naye ila alimfokea sana .

 

 

 

 

Na kwa wakati mwingine alitumia ela kubwa kuwasaidia ndugu kiasi cha kumaliza mtaji wake ila maria alijaribu kumwambia hakumsikiliza alimtukana sana na kudai kwamba yeye ni maskini Hana sauti kwenye Mali zake na wakati mwingine alifikia hatua ya kumwambia maria atoke kwenye nyumba yake kwa sababu yeye anaweza kuishi na ndugu zake bila shida na maisha yakaendelea, kwa sababu maria hakuwa na sehemu ya kwenda na mdogo wake ni maskini na kwa mda mwingi utegemea vitu vidogo kutoka kwake na kumsaidia mdogo wake aliendelea kuvumilia na kuendelea kuishi kwa maganga kwa kujikaza ila apate kidogo cha kumsaidia mdogo wake.

 

 

 

 

Maria na Maganga walifanikiwa kupata watoto wanane ,wa kiume watano na WA kike watu, watoto wote walifanikiwa kusoma na pia waliona kila kitu ambacho mama yao alikuwa anatendewa na baba yao alikuwa hapendi kabisa washirikiane na Mama yao, basi kijana mkubwa kwa jina aliitwa John alipomaliza chuo kikuu Baba yake alimpatia ngombe hamsini na mashamba kwa ajili ya kuanza maisha, kijana John alikuwa na uchungu mkubwa kuhusu maisha ya mama yake na mjomba wake ambao walikuwa maskini sana na hawakuwa na msaada kutoka kwa baba yao, basi alitafuta jinsi ya kuwasaidia, alimwomba baba yake kuhamia sehemu ya mbali Ili aweze kuchunga mifugo yake, Basi kwa sababu Mzee maganga alimpenda sana kijana wake na kumruhusu aende mbali na kuhakikisha kumpa kila kitu atakachopenda na kumwambia kwamba hasiwasahau ndugu pia hasimsikilize mke wake atakapooa , huo ushauri ulimuudhi sana John mpaka hakumwitikia baba yake.

 

 

 

 

Basi John alimchukua mama yake hata maganga hakuuliza kuhusu mke wake mahali alipoenda ,basi John akaenda akafuga, akalima kwa kuwa alikuwa msomi akafungua na viwanda mbalimbali vya kutengeneza vyombo, nguo na bidhaa mbalimbali,pia akamsaidia mjomba wake Ili aendelee kusimamia kazi zake na pia mama yake alikuwa anamshauri Sana John na pia John akawa tajiri sana akasifiwa kila mahali na Mzee maganga alifurahi kusikia sifa za kijana wake,  kw hiyo Mzee maganga alikusanya watu wengi yaani ndugu mbalimbali Ili waende kupata msaada na kazi kutoka kwa John,ila John aliwafukuza na kuwarudisha kwa baba yake kitendo ambacho hakikumfurahisha Mzee maganga.

 

 

 

Siku Moja Mzee maganga alisafiri Ili kuonana na mtoto wake John na kuona utajiri wake ambao watu wanasifia alipofika pale alishangaa kuona mke wake maria yuko kazini, msimamizi mkuu ni mjomba wake na John,na wahudumu wengi ni kutoka kwa upande wa mama hali ambayo ilimfanya Mr maganga kudai Mali yake yote aliyompatia John na John kwa sababu alikuwa kijana mpola na asiye na tamaa alichukua ngombe hamsini akampa baba yake na vitu vingine kadri ya madai ya  baba yake,kwa sababu kazi za John zilikuwa zimeshazaa sana ngombe hamsini kwake ilikuwa sio shida, Mzee maganga aliondoka akiwa na hasira kwa sababu John alimsaidia mama yake na mjomba wake kuliko kuwasaidia ndugu wa upande wa baba.

 

 

 

Basi Mzee maganga aliondoka akiwa na hasira alipofika kwake akawaita ndugu, jamaa na marafiki pamoja na watoto wake akawasimulia yote yaliyotokea na kwamba kijana John amekiuka maadili yake na kuwasaidia ndugu wa upande wa mama kuliko kuwasaidia ndugu wa upande wa baba,kwa sababu wazee wengine walikuwepo na waliona ukweli kwa sababu walitegemea matumizi na mambo mengine kutoka kwa Mzee maganga walianza kugomba wakidai kwamba John atengwe kwenye ukoo na kwamba hawamtambui labda maria alimzaa kwa mwanaume mwingine.mzozo ulikuwa na mkali mpaka wakaamua kwamba maria na John waitwae na wakaitwa kwenye mkutano wa ukoo.

 

 

 

 

Basi palikuwemo na mkutano mkubwa wa ukoo na ndugu pia wa baba bila kuhususha ndugu wa upande wa mama, wakamweka maria mbele na kumuuliza kama mimba ya John ilikuwa ni ya maganga au ilikuwa ni ya mwanaume mwingine,maria baada ya kusikia mambo kama hayo aliumia mno akakumbuka siku anajifungua mtoto John na jinsi ukoo mzima ulivyofurahi kwa kumpata mtoto kwenye ukoo na anashangaa sasa hivi anaulizwa mambo kama haya, basi kwa sababu kadri ya mila na desturi za wakati huo mwanamke akiwa mbele ya Baraza la wazee kila kitu alichokuwa anaulizwa alipaswa kukiri hata kama ni uongo.

 

 

 

 

Basi Maria aliisi uchungu akamwangalia Mme wake, watoto,ndugu na wale wazee aliangua kilio cha nguvu na watoto wake wote wakaanza kulia, wale wazee wakasema hata na watoto wako kwa upande wa mama ,hali iliyomfanya Mzee maganga kukasilika zaidi baada ya kuona watoto nao wanalia na mama yao,basi baada ya maria kushindwa kutoa jibu, hatua iliyofuata ilikuwa ni kuwauliza mizimu kama mimba ya John ilikuwa ni ya Mzee maganga au mwanaume mwingine kwa sababu mtoto amekiuka Mila kwa kumsaidia ndugu wa upande wa mama pamoja na kumdhamini Sana mama yak





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jamvini Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 547


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

SAFARI YA MUUJIZA ( SEHEMU YA PILI)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ya safari yenye muujiza ,ni pale mtoto ya Mungu mengi anafika kwenye kituo Cha ntonga na kuona yake mazingira na kufahamu njia ya kwenda kule. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Post hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mitihani inaisha na wanaanza kuhukumiwa mmoja baada ya mwingine. Soma Zaidi...

Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)
Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu, kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu alichukua ule mkate akawapstia watoto wa yule mama wakiwa wanatoka shule kwa hiyo tutaona kilichotokea kwa wale watoto. Soma Zaidi...

Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, tunajua kuwa mama yake na binti alimtorisha yule binti mbali kabisa ila kijana naye aliamua kutoroka na kumfuata binti mfalme na hatimaye akampata alipo. Soma Zaidi...

Kila kitu ambacho wanaume wanatakiwa kufahamu kuhusu wanawake.
Hii ni siri kubwa kuhusu wanawake. Hapa utajifunza jinsi ya kumfanya mwanamke asikuache. Soma Zaidi...

USALITI (sehemu ya tatu)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi. Soma Zaidi...