USALITI (sehemu ya tatu)


image


Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi.


Basi kama tulivyoona kwenye sehemu iliyopita kwamba Rhoda baada ya kuambiwa kwamba hakuna mwanamke mzuri duniani kama wewe alilia mno bila kunyamaza kama masaa matatu hivi na wakamwacha akalia hiyo ilikuwa ni dalili ya kuondoa maumivu yaliyompata, aliyemwambia maneno hayo alikuwa ameandaliwa kusudi amwambie ili kuona matokea au jinsi atakavyopokea neno hilo, wakaamua kuendesha gari huku Rhoda akilia mpaka nyumbani, baada ya kumaliza kulia alitumia siku nane bila kuongea na mtu yeyote  ila kwa siku hizo alikuwa na uwezo wa kuoga ,kufua ,kusafisha chumba chake na kufanya shughuli mbalimbali hapo nyumbani bila kuongea na mtu yeyote, na akaanza kuwasogelea hata watoto wa kiume kwa sababu hapo awali alikuwa hapendi kuona jinsia ya kiume na alianza kushiriki chakula na familia ila akiwa kimya.

 

Baada ya wataalamu wa saikolojia walikuja kuangalia maendeleo ya mgonjwa wao walikuta yuko kwenye hali ya usafi na alikuwa haongei,yule dada akavaa nguo alizokuwa anampenda kuvaa Rhoda akiwa bado yupo na akili nzuri,Rhoda alifurahi sana na yeye akavalishwa nguo ila akazivua akaenda nazo chumbani mwake akaoga akanawa akavaa na kupendeza basi wale wanasaikolojia wakamwambia apande kwenye gari akajipandisha mwenyewe wakaenda Rock City, walipofika pale akakutana na watu anaowafahamu akawasalimia wakaenda hotelini akaagiza chakula ambacho ni chips na kuku akakaa kwa heshima wakala akaanza kupiga story kama kawaida na walipomaliza kula wakaenda kwenye swimming pool akaogelea vizuri na ilipofika saa kumi na mbili akawaambia waondoke usiku umeingia.

 

Kabla hawajaingia kwenye gari aliwasihii wamnunulie nguo, alisema mda wote niliokaa nyumbani sikuwa na nguo kwa kuwa sasa nitaanza kutembea kwa watu naomba na mimi mnisaidie ni pate nguo nzuri, wakampigia baba simu wakamtaarifu kuhusu kinachoendelea baba alifurahi sana akatuma Hela ya kutosha wakampatia mwenyewe akaanza kununua alipomaliza akafunga vizuri akaweka kwenye gari wakaondoka akaomba mziki wakamwekea akaenda anaimba mpaka nyumbani, alipofika nyumbani akawasalimia, akamshukuru sana baba yake akachukua nguo akaenda kufua,akaoga na akaja kuongea na wanasaikolojia na walipotaka kuondoka akawasindikiza nje wakaenda na yeye akarudi ndani.

 

Kadri siku zilivyokuwa zinaenda akili yake ilirudi kabisa n mpaka sasa huyo dada yupo anaendelea na Kazi yake kwenye bank ila shida hapendi kutolewa , kwa hiyo wasomaji wote wa story hii ni ya ukweli kabisa na kama kuna mtu ambaye ameumizwa na tatizo lolote anione Ili kuweza kupata matibabu kutokana na wataalamu wa kisaikolojia, ila pia kutokana na story hii nawasihi sana watoto wa kike  kama mvulana au boyfriend wako ana mpango wa kukuoa na unaona Kuna nia kweli jaribu kujiwekea misimamo ya maisha kwa sababu Moses alimpenda Rhoda ila kwa sababu ya hali Ile ya kutoa mimba mara kwa mara ilimfanya  amwache kwa kuhofia kukosa watoto.

 

Vile vile na watoto wa kiume jaribu kuwa na huruma jamani hata kama msichana unaona hutaweza kumuoa usimwaribie maisha ,kama Moses angekuwa na moyo wa upendo na huruma kwa Rhoda pale walipobebeshana mimba wakiwa chuoni wangekubali kutunza hiyo mimba na kuendelea na masomo hatimaye baadae wangeoana, kwa sababu kitendo ambacho Moses alimfanyia Rhoda sio kizuri kwa sababu kimegharimu maisha yake na kufanya hata familia kutengwa na jamii,kwa hiyo inawezekana kitendo cha kumwacha Rhoda na kukimbilia mwanamke mwingine kwa wazo la kupata watoto inawezekana na kwa mwanamke aliyemuoa wasipate watoto kwa sababu damu ya zile mimba Bado unalia na pia Moses anapaswa kukumbuka machozi na mateso sliyoyapitia Rhoda ,kwa hiyo achana na tabia ya kuchezea maisha ya wenzenu miliojidai kwamba mnapendana.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    2 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    3 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Safari ya tatu ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Hadithi ya mfalme na waziri wake
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image USALITI (sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara. Soma Zaidi...

image Kutokana nyani mpaka kuwa chongo
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Kwanini dirisha moja?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Aladini na binti wa mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hatma ya kinyozi maishani mwangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...