Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku
1. Ni asubuhi Moja nzuri iliyokuwa na upepo kidogo na jua kuanza kujitokeza huku ndege wakiimba nyimbo nzuri na watu wakijiandaa kwenda makazini, ila kwa sababu Frank siku hiyo hakuwa na picha atatokea wapi kwa sababu yeye kupata kazi kwa siku ilikuwa ni majaliwa ya mwenyezi Mungu kwa sababu alitegemea vibarua Ili mkono uweze kuingia kinywani kwa hiyo siku hiyo alikuwa Hana picha na hata hajapata mtu wa kumwita kumpatia kibarua. Frank aliendelea kuvuta shuka ghafla akasikia simu ikiitia kupokea anasikia maneno makali kutoka kwa mpenzi wake Amina, ni maneno ya kusikitisha yakisema.
2. "Wewe ni mpenzi gani maskini naona huwezi kunitunza kwa hiyo chukua zako hamsini na mimi nichukue zangu hamsini kwa sababu siwezi kuishi na mvulana maskini Kama wewe" maneno haya yalimchoma sana Frank na yalimfanya ahamke kutoka usingizi na kukimbia kwenda dukani kutafuta vocha kwa ajili ya kuongea na mpenzi wake Amina, lakini Amina alimjibu hivi, " yaani wewe maskini hujanielewa sikutaki na usinifatilie na koma kwa sababu mimi sio wa kiwango chako, baada ya Frank kusikia maneno kama hayo aliumia sana na kuwa na uchungu sana kwa sababu alitegemea sana Amina kama faraja kwake, alifikilia sana akajipigapiga kichwa ,akajishauri na akaamua kwenda kwa rafiki yake James kuomba ushauri Ili kumbembeleza Amina kuendelea kuwa karibu na frank.
3 Basi frank aliamua kujiandaa vizuri kwenda kwa rafiki yake James kumwambia yaliyo moyoni, ingawa Frank alikuwa na uchungu aliamua kuwa mkakamavu Ili asiweze kuonyesha uchungu kwa watu aliokutana nao kwa sababu ilimpasa kupanda daladala kwa sababu Kuna mwendo kama saa moja hivi, Frank alikuwa kwenye kituo cha daladala anmesubiri daladala ghafla akaja gari linaendeshwa na msichana mlembo sana yule msichana akamwambia frank aingie kwenye gari ampe lift akihaidi kumfikisha pale anapoenda basi frank akakubali akapanda lile gari na alifurahi kwa sababu na nauli kwake ilikuwa ni shida.
4. Basi frank alipokuwa kwenye gari alikuwa na uzuni, ila yule msichana aliamua kusimamisha gari Ili kujua yaliyompata Frank, basi frank akapaswa kumwambia msichana yaliyompata yule msichana akaumia sana akaamua kumpa Frank moyo na kumpatia frank number za simu Ili waje kuongea baadae basi frank akafikishwa kwa rafiki yake wakaagana na yule msichana wakapeana number za simu basi frank alipofika kwake na James akabisha hodi hakufunguliwa akazunguka nyuma ya nyumba hakuona mtu baadae aliamua kuingia ndani mpaka chumbani kwa James ndipo aliposhutuka kuwakuta James na Amina wako kitandani wamekumbatiana.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme.
Soma Zaidi...Post hii ni mwendelezo wa hadithi ya safari yenye muujiza ,ni pale mtoto ya Mungu mengi anafika kwenye kituo Cha ntonga na kuona yake mazingira na kufahamu njia ya kwenda kule.
Soma Zaidi...Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo
Soma Zaidi...Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mitihani inaisha na wanaanza kuhukumiwa mmoja baada ya mwingine.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha.
Soma Zaidi...