Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya.
1. Baada ya bibi kutoka kumpasha habari mke mdogo wa mfalme kwa kila kitu kinachoendelea alirudi kwa mke mkubwa wa mfalme na kumwambia kwamba binti yako ameharibu kwa kuolewa na yule kijana ila ni lazima tufanye mbinu ila upate mfalme kwenye ukoo wako kwa sababu nitaongea na mke mdogo wa mfalme aende kumtembelea kijana wake ilai siku akienda nenda ulale na mfalme utapata mimba ya mtoto wa kiume,kwa sababu bibi ashafanya mazindiko yake ili mama apate mtoto wa kiume.
2. Basi ilifika wakati yule mtoto wa Mzee na kijana wa kiume wakapata watoto wa kiume wawili mapacha, kwa hiyo yule mke mdogo akaenda kuwasalimia wajukuu wa kiume ili aje ampashe mfalme habari, yule Mke mdogo wa mfalme alipoondoka yule mke mkubwa akaenda kwa mfalme akalala na mfalme akabeba mimba ya mtoto wa kiume, baada ya mke mdogo wa mfalme kurudi bibi akamwambia kwamba mke mkubwa wa mfalme amebeba mimba na dalili ni mtoto wa kiume.
3. Basi yule mke mdogo akapanic sana akamuuliza bibi mjanja tufanyeje? Bibi akamwambia tumpeleke yule mke wa kwanza wa kijana wa mfalme mbali na mme wake amsindikize na pia tumwambie mfalme kuwa anapaswa kusimika mrithi wa ufalme, kwa hiyo wakapanga na mtoto wa kiume wa mfalme wakamwahidia mali nyingi kwa sababu ya kupenda mali akakubali kurudi nyumbani kutoka machimboni ila mke yule alimwacha, akamwambia mfalme kwamba niko tayari kurithi ufalme wako, mfalme akafurahi sana ila akampa mashariti kwamba hapendi sherehe anaomba akabidhiwe kadri ya sheria na watu wachache sherehe itakuwa baadae mfalme akakubali.
4. Basi kesho yake yule mtoto wa kiume wa mfalme akamwambia mke wake yule pacha wake waende kutembea kwenye ufalme mwingine yule binti akafurahi sana wakaenda walipofika akamwacha huko akampitia mke mwingine yule mwenye mapacha akamleta kwa baba yake mfalme, baba yake akafurahi sana akaandaa sherehe akampatia mtoto wake ufalme na bibi akaitwa kukaa ikulu na baada ya siku chache yule mama mkubwa akajifungua mtoto wa kiume . hadithi yangu imeishia hapo.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jamvini Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1655
Sponsored links
👉1
kitabu cha Simulizi
👉2
Simulizi za Hadithi Audio
👉3
Kitabu cha Afya
👉4
Kitau cha Fiqh
👉5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6
Madrasa kiganjani
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha Soma Zaidi...
USALITI (sehemu ya tatu)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi. Soma Zaidi...
Hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi habari za Mama mmoja aliyekuwa mchoyo akampa mkate mwehu na kuutia Sumu ila kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu sana aliutunza mkate na kuwapatia watoto wa yule mama waliokuwa wakitoka shule na njaa kali Soma Zaidi...
Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, baada ya kijana wa kiume wa binti mfalme kuoa yule ndugu yake baba anafanya sherehe kubwa na wake wenza wamepata habari kwamba kijana wa kiume wa mfalme ameoa ndugu yake wakaamuru kunyamaza il Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tano)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya Nimlaumu nani ambapo juma anapanga na madaktari wanaopima DNA ili kuweza kutambua kwamba mtu mimba ni ya kwake na sio ya Frank kwa hiyo tuendelee kusikiliza mpaka tutakapoona mimba itakuwa ya Frank au juma. Soma Zaidi...
Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Post hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mitihani inaisha na wanaanza kuhukumiwa mmoja baada ya mwingine. Soma Zaidi...
Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu. Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...