picha

Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme

Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu.

Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme.

1. Fundisho la kwanza ni kwamba ukipata watoto wakiwa kwenye jinsia tofauti, watoto wote ni sawa.

Kwa mfano kuna mama anaweza kupata watoto wa kiume tu au wa kike tu mshukuru Mungu kwa sababu huwezi kujua nani atakusaidia kwa sababu tumeona jinsi mke mdogo wa mfalme alivyokuwa na wasiwasi sana baada ya kuona tatizo lake linagundulika la kumtupa Mtoto wa kike na kubakiza wa kiume ingawa alichokipenda alikipata ila kwa kutumia nguvu na mda hata kama angejifungua wote wawili me sioni shida bali mmoja angerithi ufalme na mwingine angebaki kawaida.

 

2. Pia fundisho la pili kutokana na hadithi hii ni kwamba wasichana acheni tabia ya kutupa watoto kwa sababu ujui unayemtupa ndiye atakufa upoteze amani baadae , kwa mfano unaweza kutoa mimba ukaitoa vibaya na kizazi kikapitiwa kwa hiyo utaumia maisha yako yote , kama mke mdogo alivyoangaika kwa kitendo cha kutomtambulisha mtoto wa kike kwa mfalme.

 

3 fundisho la tatu ni kwamba tunapaswa kuachana na usaliti katika maisha kwa sababu mtoto wa kiume wa mfalme baada ya kuona yule binti kwa mzee aliweza kushawishika na kuamua kumwacha mkewe mpandwa aliyepigania na kukosa uhusiano mzuri na mama yake akaona msichana wa kwa mzee.

 

4. Fundisho la nne ni kwamba wivu ni mbaya kwa sababu wake wenza walimwonaea wivu mke mdogo akaamua kutoroka na kuzaa watoto wawili msichana na mvulana , mmoja akamwacha kwa bibi, labda hasingeonewa wivu na kutoroka angezalia kwa mumewe hasingemtupa kwa bibi yule msichana.

 

5.  Katika maisha yetu tuache kuwa ndumila kuwili kama bibi mara yuko kwa mtoto wa kiume wa mfalme, mara kwa mke mdogo wa mfalme, mara yuko kwa mke mkubwa wa mfalme, mara yuko kwa mzee lengo lake ni kupata maslahi yake na alifanikiwa.

 

6. Fundisho la mwisho wanaume wanapaswa kuwa na msimamo mkubwa kwenye familia zao bila kuendesha na wanawake sawa ingawa kushauriana ni kuzuri ila kuna mambo mengine makubali tu bila kuchunguza kama mfalme alivyokuwa anakubali kila kitu kutoka kwa mke mdogo.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jamvini Main: Post File: Download PDF Views 2244

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 ai web app     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu, kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu alichukua ule mkate akawapstia watoto wa yule mama wakiwa wanatoka shule kwa hiyo tutaona kilichotokea kwa wale watoto.

Soma Zaidi...
USALITI (sehemu ya pili)

Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara.

Soma Zaidi...
SAFARI YA MUUJIZA sehemu ya tatu

Post hii inahusu Zaidi hadithi ya safari ya muujiza ambapo ya Mungu mengi anaenda kwao na kuomba kufahamu history yake ili afahamu kuhusu wazazi weo walipo na ndugu zao walipo.

Soma Zaidi...
Hadithi ya Mama mchoyo na mwehu

Posti hii inahusu zaidi habari za Mama mmoja aliyekuwa mchoyo akampa mkate mwehu na kuutia Sumu ila kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu sana aliutunza mkate na kuwapatia watoto wa yule mama waliokuwa wakitoka shule na njaa kali

Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)

Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya.

Soma Zaidi...
Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 3)

Posti hii inahusu zaidi hasara za kuwa na wivu na kutokuwa wazi, sehemu hii inahusu zaidi maendeleo ya Lisa shuleni yanakuwa mabaya zaidi na lina anaendelea kumtunzia siri lengo lake lina ni kuendelea kuwa wa kwanza darasani.

Soma Zaidi...