Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 3)

Posti hii inahusu zaidi hasara za kuwa na wivu na kutokuwa wazi, sehemu hii inahusu zaidi maendeleo ya Lisa shuleni yanakuwa mabaya zaidi na lina anaendelea kumtunzia siri lengo lake lina ni kuendelea kuwa wa kwanza darasani.

Hasara za wivu na kutokuwa wazi.

1. Basi Lisa akawa jambazi kabisa na siku nyingine akawa anatoka nyumbani usiku na kwenda kwa mpenzi wake na akigunduliwa na mama yake anamdanganya kwamba kuna mtu alinipeleka usiku,kweli mama Lisa akaumia kweli  na akaamua kwenda kwa mganga na waganga walivyo waongo, yule mganga akamwambia kwamba ni rafiki yako yaani mama lina ndiye anayemchezaea  mtoto wako, kwa hiyo mama Lisa akakumbuka na neno alilolisema lina siku Lisa anakuja aliumia mno kwa hiyo mama Lisa akaamua kwenda kwa mama lina akiwa na hasira kubwa na kulalamika kuhusu yote anayotendewa mwanae.

 

 

 

 

 

2. Basi mama lina akaumia sana na akaamua kumuuliza mwanae lina kwa nini Lisa anafeli darasani na lina alikosa jibu la kumpa mamae ila mama yake alipombana zaidi ndipo akaamua kumwambia kila kitu kwamba lisa aendagi darasani na anashinda na mvulana, kwa hiyo mama lina aliumia sana akataka kumwambia mama Lisa ila alikosa jinsi na baadae aliamua kumwambia ila mama Lisa alikataa kabisa, basi hali ya Lisa ikawa mbaya zaidi, na walipofanya mtihani wa kuingia darasa la saba alikuwa mtoto wa tisini na tano kati ya mia moja ila Lina alikuwa wa kwanza, mama Lisa akaongeza chuki zaidi juu ya lina na mamaye.

 

 

 

 

 

3. Basi mama Lisa akaenda kwa watu mbalimbali akitangaza kuwa mama lina ni mchawi na amemfundisha mwanae lina naye ni mchawi kwa hiyo watu wakachukia wakataka kumfukuza mama lina kwenye nzengo yao ila wakampa mwaka mmoja kusudi mtoto amalize shule na akimaliza hawataki kumwona pale, kwa sababu baba yake  lini alifariki lina akiwa mdogo kwa hiyo ilikuwa ni shida kubwa kwa mama lina kuhama pale kwa hiyo alitafuta sehemu kila kona na hakufanikiwa kwa sababu alikua hana kipato kikubwa cha kununua kiwanja kwa hiyo aliamua kumpigia mama wa kambo wa Lisa ili kumwambia kila kitu jinsi mke mwenza alivyofanyia .

 

 

 

 

4. Basi kwa sababu mama wa kambo wa Lisa lengo lake ni kuharibu maisha ya Lisa alipata nafasi nzuri ya kuharibu, kwa hiyo yule mama wa kambo wa Lisa alikuwa na pesa na alichokifanya ni kuhakikisha kujua ukweli kupitia kwa mama lina na kuhakikisha kwamba Lisa anaharbiwa kila kitu, kwa hiyo mama lina alipatiwa kiwanja na mama wa kambo wa Lisa na pia akamjengea nyumba nzuri na akasubiri mtoto wake amalize la saba wahamie huko, basi kwa sababu mama wa kambo wa Lisa alijua ukweli wote na tatizo la Lisa ,akaamua kumwambia mkewe kwamba wamlete tena mtoto nyumbani wamtafutie mwalimu awe anamfundishia nyumbani na baba Lisa akakubali.

 

 

 

 

5. Kwa hiyo mama wa kambo wa Lisa akamwambia nitamtafuta mwalimu na baba lisa akakubali, kwa hiyo mama wa kambo wa Lisa akamwendea  mama lina wakamtafuta yule mwalimu anayempenda Lisa wakaongea naye na kuhaidi kumlipa hela kubwa na kumpatia sehemu ya kuishi, na yule mwalimu akakubali kazi ile na Ela ilikuwa kubwa na kufika kuanza kazi akakuta mwanafunzi ni Lisa akafurahi sana kwa sababu alikuwa anatafuta alipo hakufanikiwa kumpata kwa sababu Lisa hakuwa na simu, basi yule mama wa kambo akamwambia baba Lisa kwamba Lisa anapaswa kuwa na chumba chake karibu na mwalimu ili akipata shida kimasomo mwalimu anafundisha, na baba Lisa akakubali lile ombi.

 

 

 

 

 

6. Basi maisha ya kusoma yakaanza siku zote Lisa alikuwa analala kwa yule mwalimu wake yaani walikuwa kama mke na mme na yule mama wa kambo wa Lisa alifahamu hilo akafurahi sana akatamani yule Lisa ababeshwe mimba na kuharibikiwa maisha ila kaka alikuwa makini, sasa ikafika siku ya kufanya mtihani wa robo muhula, kwa sababu yule kaka alikuwa anafundisha pale akaiba mitihani akasolve yote na Lisa na Lisa alipokuja kufanya mtihani akawa mtu wa tano ila lina alikuwa wa kwanza,baba yake akafurahi sana akampa yule kijana zawadi ila mama wa kambo wa Lisa hakufurahi kwa hiyo akaanza kumfanyia yule mwalimu visa na kuamua kumfukuza yule mwalimu na kumtafuta mwalimu mwingine kijana ambaye atamfundisha Lisa, ila Lisa kwa sababu alikuwa ni binti wa kuvutia alipendwa na yule kijana ila Lisa alikataa kwa sababu hisia zake zote zilikuwa kwa mwalimu wake.

 

 

 

 

 

7. Basi kwa sababu  ya hisia za Lisa  kwa mwalimu wake akamwambia yule mwalimu kijana kama utanisumbua nitamwambia baba, basi yule kijana akaanza kumfundisha kwa kumtugia mitihani migumu na Lisa anafeli na baba yake anamtukana kwamba hana akili ila yale maswali magumu yalimsaidia kuona maswali ya shule ni marahisi sana,kwa kipindi hicho maisha ya Lisa yakabadilika na akaanza kusoma na yule mama baada ya kuona juhudi za Lisa akaamua kumnunulia simu nzuri sana na kumwekea Salio la kutosha, hapo Lisa akafurahi sana na akaanza kuchati na yule mwalimu na akili zikaanza kupotea tena ila yule kijana siku moja akagundua hilo akapaswa kumsema kwa baba yake na baba alipoona hayo akagundua kwamba tatizo la mwanae ni lipi na akaamua kuonge na mama mzazi wa Lisa kuhusu tabia yake na ndipo mama Lisa aliona aibu na kujifanya kwamba hajui lolote.

 

 

 

 

 

8. Kwa sababu baba Lisa alimpenda sana binti yake aliamua kumwamisha bila kumwambia mama wa kambo wa Lisa na akampeleka shule za private akamrudisha darasa la tano, kwa sababu Lisa hakuwa na kitu kinachomsumbua akasoma kwa bidii kubwa na akafahamu kingereza na baada ya mwezi mmoja walimpeleka darasa la sita na akasoma vizuri bila shida na akawa anawazidi wanafunzi wengine na kufanya vizuri sana, kwa hiyo mama wake wa kambo hakujua mtoto yuko wapi na mama Lisa hakujua kwa sababu baba Lisa aliona wote hawana uwezo wa kumwambia mtoto wake ukweli ila watampoteza, ila kwa sababu yule binti alivutia yule kijana aliyemfundisha mara ya pili akawa anamfatilia kwa mbali na ndiye aliyemwambia baba yake ampeleke mbali na akina mama hao wawili.

 

 

 

 

 

9. Basi ikafika siku ya likizo yule kijana akamwambia baba Lisa kwamba yeye ana sehemu nzuri na akampeleka Lisa akawa anaishi naye akamshauri vizuri kuhusu kusoma na kutimiza ndoto na yule Lisa akamwelewa kabisa akawa anasoma na yule kijana alikuwa mkali sana kwa Lisa ila lengo lake ni kwamba baada ya Lisa kukaa vizuri na kumaliza aje awe mke wake, kwa hiyo Lisa alikaa huko na kusoma ila mama yake na mama wa kambo hawakujua Lisa yuko wapi,ila baba yake alisema mtoto yuko kwenye mikono salama,

 

 

 

 

 

10. Basi Lisa akafanya mtihani wa darasa la saba akafaulu vizuri na baba akampatia yule mwalimu zawadi nzuri kwa sababu ya kumtunza binti yake, sasa swali linabaki kichwani mwa baba je huyu binti pamoja na uzuri wake na akili yake ataenda kusoma wapi?.

 

 

 

itaendelea baadae

 

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/23/Tuesday - 09:16:07 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 697


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Nje ya jumba la kifahari la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Safari ya tano ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Siri ya kifo yafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Dalili za fangasi ukeni
Post hii inakwenda kukujulisha dalili za kuwa huwenda una fangasi sehemu zako za siri. Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

Dalili ya mimba ya wiki moja(1)
Mwanaume na mwanamke wanapo kutana na kujamiina kama mwanamke yupo kwenye ferlile process ni rahisi kupata mbimba. Sparm Zaid ya million moja huingia kwenye mfuko wa lakin sparm moja ndio huweza kuingia kwenye ovum(yai)lakin nyingine hubaki kwenye follopi Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Dalili za U.T.I
'UTI (urinary tract infection) no ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya husababishwa na bacteria, fangasi,na virus. Pia unaweza athiri rethra, kibofu Cha mkojo na figo.lakini Mara nyingi UTI huathiri Hadi mfumo wa uzazi na w Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha. Soma Zaidi...