image

SAFARI YA MUUJIZA sehemu ya tatu

Post hii inahusu Zaidi hadithi ya safari ya muujiza ambapo ya Mungu mengi anaenda kwao na kuomba kufahamu history yake ili afahamu kuhusu wazazi weo walipo na ndugu zao walipo.

SAFARI YA MUUJIZA

Kwa hiyo mtoto au msichana ya Mungu mengi alirudi kwao akiwa na mawazo kuhusu yule dada rafiki yake ambaye alikutana naye kwenye kituo Cha watoto yatima, na pia aliamua kupata ukweli kuhusu yule rafiki yake mpya, Kwa hiyo akakusudia kumwambia Mama yake mlezi yote  yaliyo moyoni mwake, basi kesho yake mama mlezi wa ya Mungu mengi alimwambia mwanae kwamba waende shambani kulima na ukizingatia shamba lilikuwa mbali na nyumbani, basi ya Mungu mengi alifikilia kwamba huu ndio wakati wa kuongea yaliyomo moyoni mwake.

 

 

 

Kesho yake ikafika ya Mungu mengi akabeba jembe, maji ya kunywa na vyakula vichache vya kutumia huko shambani, basi walipokuwa njiani kuelekea shambani, mama mlezi wa ya Mungu mengi akaanza kumuuliza mwanae, Kwa nini siku hizi una huzuni sana, ya Mungu mengi akaanza kufikilia jinsi ya kumjibu ikabidi alie sana ndipo mama akaanza kuhisi kwamba huyu mtoto ana tatizo fulani ambalo linamsumbu, basi mama mlezi wa ya Mungu mengi akabembeleza huyo mtoto ili aweze kusema kinachomsumbua, basi mtoto ya Mungu mengi akaanza kuongea Kama ifuatavyo.

 

Mama yangu nashukuru sana kwa msaada mlionipa Mimi nimeishi Kwa furaha na deko sana nikijiona ni mtoto wa pekee wa kike kwenye familia,nilipewa Kila kitu nilichokipenda na kuonyeshwa upendo wa dhati kabisa ila Cha ajabu ni kwamba baada ya kukosa akili darasani ndipo nikaambiwa hadharani kwamba sio mtoto wa pale nyumbani hali ambayo ilinifanya  nijisikie vibaya Cha Zaidi ni kwamba sijui ndugu zangu sijui damu yangu, nami ningependa kufahamu damu yangu hata kama ni mtoto yatima Kuna walau damu yangu sehemu ilipo, baada ya mtoto ya Mungu mengi kumaliza kuongea hivyo alilia sana ,na akaendelea kusema kwamba mama naomba kujua historia yangu Kwa sababu wewe ndiye uliyebaki upande wangu ili niweze kutafuta damu yangu na pia naona hata na ndugu zangu baada ya kufahamu Hilo hawanijali hata kidogo Kwa upande wa baba huko Sina hamu kabisa.

 

Basi baada ya mtoto ya Mungu mengi kushusha ujumbe mzito mama mlezi wa ya Mungu mengi akainama chini akatoa machozi akaanza kumwambia mwanae Kwa kusema.

Mwanangu nakushukuru sana kwa kuwa wazi,ila na Mimi ningependa kukwambia ukweli, Mimi na baba yako mlezi baada ya kukaa mda mrefu bila mtoto wa kike tuliamua kwenda kwenye kituo Cha watoto yatima ntonga kutafuta mtoto wa kike baada ya kufika tu tulimkuta watoto wawili wa kike mapacha walikuwa wamefiwa na mama yao baada ya kujifungua Kwa sababu baba yao hakuwa na uwezo na alikuwa muamiaji kwenye mazingira Yale ikabidi waletwe ntonga Kwa malezi Zaidi,Kwa sababu baba yako mlezi alikuwa anakaa anasafiri na pia malezi ya mapacha ni shida aliamua tuchukue mtoto mmoja na mwingine tumuache pale kituoni na tukafanya hivyo,basi Kwa sababu tulitaka watoto wetu wasijue hiyo siri nilisafiri na wewe baada ya kukutoa kituoni Kwa mwezi mzima ili ionekane kwamba nimejifungua na watoto waliamini hivyo.

 

 

 

baada ya mama mlezi wa ya Mungu mengi kumaliza kusema hivyo yule mtoto akaelewa na akaanza kufikilia sana kuhusu yule Binti ndipo mama yake akamuuliza una shida gani mwanangu? , Akainama chini akasema, mama nimepata uhakika wa kike nilichokiona kule tulipoenda kituo Cha watoto yatima kilichoitwa ntonga, Kuna rafiki yangu ambaye tulionana tukaongea na kuelewana na amesema nikipata mda nitaenda kule kumsalimia, ndipo mama akajibu na kumwambia mwanangu usiende uko mpaka niongee na baba yako,Kwa sababu ya Mungu mengi alikuwa hampendi tena baba yake mlezi Kwa sababu alikuwa anampinga Kwa Kila kitu akainama chini na kulia, na kuanza kuongea Kama ifuatavyo.

 

 

Mama nashukuru sana kwa kufahamu hayo ila Sasa naomba ushirikiano wako wewe kama mama ili niweze kumpata ndugu yangu na kujitambulisha kwake Kwa sababu bila kufanya hayo hatutaweza kupata damu yetu maana damu ni nzito kuliko Maji,na pia Mimi napenda kuwa huru kutoka kwenye familia hii ambayo umenisaidia sana ingawa Kwa Sasa napata shida kubwa sana Kwa sababu ya mabadiliko makubwa kwenye familia haka kukosa upendo kwangu.

 

 

Mama yake mlezi baada ya kusikia maneno hayo ya ya Mungu mengi aliinamisha kichwa na kuanza kulia Kwa sauti na baadhi ya watu walishangaaa na walikuja hapo kufatilia na mama mlezi wa ya Mungu mengi alijifanya  yeye kama ni mgonjwa akaomba msaada ili apelekwe nyumba iliyokuwa karibuna pale shambani,basi wakaenda nyumbani napia  wale watu waliomleta mama wa ya Mungu mengi,Kwa hiyo mama wa ya Mungu mengi akaanza kumwambia mwanae kwamba wanapaswa kwanza kwenda nyumbani Kwa baba yao ili kutoa taarifa ya kukaa mashambani Kwa mda Kwa sababu Wana mambo mengi ya kufanya ila lengo lao ni kutaka kufatilia ukoo wa ya Mungu mengi.Ya Mungu mengi alikataa akasema yeye hawezi kurudi home labda mama aende mwenyewe na atamkuta.

 

 

Kwa Sababu yule mama alimpenda sana ya Mungu mengi aliamua kushirikiana vizuri na ya Mungu mengi na kabla hajaondoka aliacha ameezeka nyumba yao vizuri Kwa sababu ila nyumba karibu na mashamba Kuna wanyama wakati wa usiku na pia Kwa sababu kulikuwepo na vijana wengi Kwa mazingira hayo na ukizingatia ya Mungu mengi alikuwa msichana mlembo kweli alikuwa anamezewa na mate na vijana wengi ila mama yake mlezi alimsimamia sana na kujaribu kumshauri na kumwambia ukweli kuhusu maisha.

 

 

 

 BasI mama mlezi wa ya Mungu mengi akafunga safari akaenda Kwa Mme wake na Mme wake alipomuona Hana ya Mungu mengi alisema walau nakushukuru hujaja na yule mpuuzi hali ambayo ilimfanya mama mlezi wa ya Mungu mengi kuchukua sana na kujisikia vibaya,Basi watoto walipomuona mama yao walifurahi sana ila hakuna aliyeulizia kuhusu habari za ya Mungu mengi hali hii ilimfanya mama mlezi wa ya Mungu mengi kugundua kwamba baba ya watoto amwwapa simu kubwa kuhusu ya Mungu mengi. Basi baadae kidogo alikuja kijana WA pili alipoona mama yake alifurahi mno Kwa sababu alikuwa machingani ndiye pekee aliyeuliza habari za ya Mungu mengi.

 

 

 

Basi mama mlezi wa ya Mungu mengi akamwambia Mme wake kwamba amekuja kufuata chakula na maji Kwa ajili yao Kwa sababu watakuwa na kipindi kirefu Cha kulima basi baba mlezi wa ya Mungu mengi akasema hakuna shida na mfundishe huyo mpuuzi alimee sana Kwa sababu Hana ​​​​​​aKili za darasani,Kwa hiyo mama mlezi wa ya Mungu mengi akaongea vizuri na mtoto wake wa pili kuhusu Jambo hili,Kwa sababu kati ya watoto waliokuwa wanazaliwa na mlezi wa ya Mungu mengi ni mtoto wa pili ndiye aliyekuwa anampenda ya Mungu mengi peke yake na ni Kwa sababu ya Mungu mengi alikuwa msichana mlembo na alipofahamu ya kwamba sio ndugu yake alipanga kumwoa ki siri siri Kwa hiyo baada ya kupewa hii insue alitaka kuteka akili za mama yake ili aweze kupata ya Mungu mengi.

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 765


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, kuhusu hadithi hii ni pale Jackie anaandikiwa barua na Julius ili apotezwe akili na wavulana wengine kwa sababu Jackie aliwapita darasani. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambao walipoteana katika hali za kukimbizwa na wazazi Ili waweze kutimiza ndoto zao na siku wakakutana wakiwa watu wazima. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Post hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mitihani inaisha na wanaanza kuhukumiwa mmoja baada ya mwingine. Soma Zaidi...

Hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi habari za Mama mmoja aliyekuwa mchoyo akampa mkate mwehu na kuutia Sumu ila kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu sana aliutunza mkate na kuwapatia watoto wa yule mama waliokuwa wakitoka shule na njaa kali Soma Zaidi...

NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki. Soma Zaidi...

Hadithi za alif lela u lela
Haya ni masimulizi ya Hadithi za alif lela u lela Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu, kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu alichukua ule mkate akawapstia watoto wa yule mama wakiwa wanatoka shule kwa hiyo tutaona kilichotokea kwa wale watoto. Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku Soma Zaidi...

Chemsha bongo na bongoclass
Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi. Soma Zaidi...

WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 2
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ambayo Kwa jina inaitwa wakati wa Kufumbuka, ni mwendelezo wa pale maria anawekwa mbele ya wazee Ili akili kwamba John sio mtoto wa Mzee maganga ila maria akikumbuka wazi kwamba John ni mtoto wa Mzee maganga anakataa kuki Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...