Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
		UPUNGUFU WA PROTIN
		Ugonjwa wa kwashiakoo ni katika yanayoletwa na upungufu wa protini. Pia ukuaji hafifu wa mtoto na kupelekea kudumaa ni katika upungufu wa vyakula hivi. Kiriba tumbo hasa kinachotokea kwa sbabu ya kuvimba kwa ini. Hii huweza kupelekea ini kushindwa kufanya kazi. Misuli na nyama za mwili kushindwa kujaa kwa ufasaha. Wataalamu wanahusisha uimarikaji wa mifupa kuwa unategemea pia vyakula hivi. Hivyo upungufu wa protini huweza kusababisha udhaifu wa mifupa.
		
UPUNGUFU WA FATI
		Kama hautapata fat ya kutosha kuweza kutengeneza omega-3 fat acid unaweza kupata upungufu wa vitamin A, D, E na K hivyo magonjwa yanayohusiana na upungufu wa madini haya hayatakuwa mbali nawe. Vyakula vya fati vina saidia katika kuiweka ngozi kuwa katika afya njema. Kama utakosa fati ya kutosha ngozi yako itashindwa kupata majimaji ya kutosha na hivyo kupelekea afya dhaifu ya ngozi.
		
		Omega-3 fat acid ipo katik aina kuu mbili ambazo ni  eicosapentaenoic acid na docosahexaenoic acid hizi husaidia katika ukuaji na maendeleo mazuri ya ubongo. Pindi ukikosa aina hizi za fat acid unaweza kupata matatizo ya kusahau na ukuaji hafifu wa ubongo. Omega-3 fat acid inaweza kupatikana kwenye samaki, nyama na vyakula vingine lakini si kwenye matunda wala mboga a majani. Fat acidi inasaidia katika kutengebezwa kwa pigment rhodopsin hizi husaidia katika kuboresha afya ya macho. Husaidia katika kuufanya ubongo uweze kutafasiri mwanga kuwa kitu unachokiona. Husaidia sana kwa wazee dhidi ya matatizo ya kutokuona.
		
		
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Soma Zaidi...Je umesha wahi kujiuliza kuwa ni vinywaji vipi mwenye presha ya kupanda anafaha kutumia, Unadhani ni maji, mvinyo wa pombe, chai na kahawa. Bila shaka ungependa kujuwa zaidi kuhusu jambo hili. Makala hii ni kwa ajili yako
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula parachichi
Soma Zaidi...Somo hili linalenga kukujuza juu ya umuhimu wa tikiti kwenye afya ya mwili
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya protini
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukieleza kuhusu vyakula vya madini na kazi zake mwilini
Soma Zaidi...