Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako
3.Palachichi (avocado)
Hili ni katika matunda yenye fat (mafuta). Itambulike kuwa si kila mafuta ni hatari ndani ya miili yetu. Tunahitaji vyakula vya fat yaani mafuta kwa ajili ya kutupatia joto kwenye miili yetu. Pia fati husaidia kuipa miili yetu nguvu. Katika tunda hili palachichi mafuta yake ni aina ya oleic acid yaani yapo katika aina flani ya asidi ambayo husaidia katika kupunguza uvimbe mwilini na kusaidia kuboresha afya ya moyo.
Palachici pia hutambulika kitaalamu kuwa lina lina madini ya potassium na magnesium kwa wingi sana. Pia ni katika vyakula vyenye kambakamba yaani fiber. Vyakula hivi vyenye fiber husaidia katika kuweka usalama wa tumbo yaani kuhakikisha chakula kinatembea ipasavyo ndani ya tumbo kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine mpaka kufika kwenye njia ya haja kubwa.
Pia tunda hili husaidia kupungusa hatari za kupata maradhi ya stroke yaani kupalalaizi kutokana na kiwango kikubwa cha madini ya magnessium ambayo husaidia katika kupunguza shinikizo kubwa la damu. Hivyo palachichi husaidia katika kudhibiti afya ya moyo. Palachichi moja linaweza kutoa 28% ya mahitaji ya mwili ya madini haya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula biringanya eggplant)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukujulisha hatari za kupaliwa na asali ama kitu kingine kama muulizaji alivyouliza.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula njegere, kunde, mbaazi, njugu mawe na maharage
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula asali
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha utaratibu wa lishe kwa wagonjwa wenye kisukari pamoja na vyakula salamakwao.
Soma Zaidi...