image

Fahamu vitamini C na kazi zake, vyakula vya vitamini C na athari za upungufu wake.

kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.

Fahamu vitamini C na kazi zake, vyakula vya vitamini C na athari za upungufu wake.



VYAKULA VYA VITAMINI C

Vitamini C ni katika vitamini muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Vitamini hivi vina sifa ya antioxidant. Antioxidant zenyewe ndani ya mwili ndizo ambazo husaidia kuupa mwili nguvu na kinga ya kupamba na na sumu, na vijidudu shambulizi. Vvitamini C ina pendelewa kuwepo ndani ya miili yetu kwa wingi muda wowote. Wapo wataalamu wa afya wanapendekeza kutumia vitamini C kwa ajili ya kupunguza uwezekeno wa kupata mafua na homa ya mafua mara lkwa mara. Katika makala hii nimekuandalia somo zima kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.



YALIYOMO:

  1. Maana ya vitamini C
  2. Vyakula vya vitamini C
  3. Kazi zake mwilini
  4. Dalili za upungufu wa vitamini C
  5. Maradhi yaletwayo na upungufu wa vitamini c
  6. Athari za kuwa na vitamini C kupitiliza
  7. Ugonjwa wa Kiseyeye


Maana na Historia ya vitamini C

Vitamini C kitaalamu pia hufahamika kama “ascobic acid” ama ascorbate. Vitamini C ni katika water soluble vitamini ambayo husaidia kukinga mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeyee au kitaalamu scurvy. Ni maradhi hatari sana yanayodhurua afya. Kwa maelezo zaidi ya maradhi haya enelea kusoma makala hii.



Vitamini C vimegunduliwa miaka ya 1920 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Albert von Szent Györgyi. Pia itambulike kuwa hapo mwanzo mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Kazimierz Funk yeye alieleza kuwa kuna maradhi yanasababishwa na upungufu wa virutubisho mwilini. Katika maradhi hayo aliyoyataja ugonjwa uitwao scurvy yaani kisehehe aliupa virutubicho kwa herufi C.



Baada ya ugunduzi wa Albert von Szent na haworth wakaipa herufi C kemikali iitwayo ascobic acid. Na hii ndiyo vitamini C. hivyo herufi C kwenye vitamini C ina maana ascobic acid hii ni tindikali. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa wanyama katu hawawezi kuishi bila ya vitamini C mwilini mwao.Vitamini C ndio vitamini vya kwanza kuweza kutengenezwa na binadamu kikemikali.



VYAKULA VYA VITAMINI C

Kwa kuwa tumeshajuwa sasa maana na historia ya vitamini C hapa nitakwenda kukueleza chanzo cha vitamini C na je ni katika vyakula vipi tunapata vitamini C. kwa ufupi wa somo ni kuwa vitamini C unaweza kuvipata kwenye matunda yenye ladha ya uchachu uchachu (citrus) na matunda vyenye rangi ya njano na kwenye mboga za majani



Vyakula vya vitamini c

  1. Pera
  2. Pilipili
  3. Papai
  4. Chungwa
  5. Limao/ndimu
  6. Zabibu
  7. Nanasi
  8. Pensheni
  9. Kabichi
  10. Embe
  11. Nyanya
  12. Tunguja
  13. Palachichi
  14. Kitunguu
  15. Karoti
  16. Epo


Tofauti na mboga za majani na matunda ya uchachu na yenye rangi ya njano pia tunaweza kupata vitamini C kwa kula maini, maziwa na mayai. Pia unaweza kupata vitamini C kwa kumezaa vidonge vya vitamini C.



KAZI ZA VITAMINI C MWALINI

Kama tulivyowkisha kuona kuwa vitamini C hulunda mwili dhidi ya mashambulizi na sumu za vyakula. Pia basi vitamini C husaidia katika kulinda mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali kma kiseyeye, magonjwa ya ngozi, mifupa na moyo. Katika kipengele hiki utakwenda kuona kwa undani zaidi kuhusu kazi hizi za vitamini c mwilini:



Kazi kuu tatuza vitamini C

  1. Husaidia katika utengenezwaji wa collagen hizi ni protini ambazo huhusika katika utengenezwaji wa tishu kitaalamu zinazotambulika kama connective tissue na pia husaidia katika uponaji wa vidonda na majeraha. Mtu mwenye upungufu wa vitamini C vidonda vyake vitachelewa sana kupona ukilinganisha na mwenye vitamini C vya kuatosha.


Tishu hizi ndizo ambazo zilitupa umbo letu, kwa lugha nyepesi hizi nyama zinazoonekana kwenye miili yetu, zilizofunika mbavu, mifupa, magoti, kichwa na maeneo yote ya mwili. Tishu hizi pia zinapatikana kwenye viungio vya miili yetu. Mifupa laini ya kwenye viungio vyetu pia ni katika tishu hizi. Hivyo protini huhusika katika utengenezwaji wa hizi tishu.



  1. Vitamini C ni antioxidant katika miili yetu antioxidanti hufanyakazi ya kulinda miili dhidi ya mipambano ya kikemikali ya melecule ndani ya miili yetu.. Antioxidant ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika uuguzwaji wa oksijeni mwilini. Husaidia kuzui antioxidant hupunguza sumu za vyakula wilini. Miili yetu inahitaji antioxidant ili iweze kujilinda na kuwa madhubuti. Zipo antioxidant nyingia mbazo tunaweza kuzipata kwa vyakula. Mifano hiyo ni:-


  1. Husaidia katika uupa mfumo wa kinga nguvu na uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi na uvamizi dhidi ya maradhi.


Kazi nyingine za vitamini C

  1. Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye (scurvy):


Ugonjwa wa kiseyeye (scurvy)

Ugonjwa wa kiseyeye husababishwa na upungufu wa vitamini C na kutibiwa kwa kupata vitamini C aidha kwa kutumia vyakula ama vidonge vya vitamini C. dalili za ugonjwa huu huanza kutokea mwezi mmoja toka upungufu wa vitamini C uanze kutokea mwilini.



Dalili za ugonjwa wa kiseyeye:

  1. Kushindwa kuhema vizuri
  2. Maumivu ya mifupa
  3. Mafinzi kutoka damu
  4. Uponaji ulio hafifu wa vidonda
  5. Homa
  6. Mwili kukosa nguvu
  7. Maumivu ya misuli na viungio
  8. Kifo




  1. Kulinda mwili zidi ya maambukizi na mashambulizi:

Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.



Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.



  1. Kulinda miili yetu dhidi ya saratani (cancer):

Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:

  1. Vitamini C husaidia kuborsha afya na kuishi vyema kwa wagonjwa wa saratani
  2. Vitamini C inaweza kuuwa seli zinazotengeneza uvimbe wa saratani


  1. Husaidia kulind miili yetu dhidi ya maradhi yanayohusu mishipa ya damu na moyo (cardiovascular)
  2. Husaidia kulinda miili yetu dhidi ya maradhi ya ubongona kusahasahau


UPUNGUFU WA VITAMINI C

Endapo kutatokea upungufu wa vitamini C mwilini kuna athari kubwa itakayotokea mwilini ikiwemo:



ATHARI ZA KULA VITAMINI C KUPITILIZA

Kila kirutibisho kinahitajika ndani ya miili yetu kwa kiwango maalumu. Endapo kirutubisho kitakuwa kingi kupitiliza athari zinaweza kutokea katika afya ya mtu. Miongoni mwa athari za kuwa na vitamini C kupitiliza ni kama zifuatazo:-



Mwisho

Kwakuwa sasa unatambua umuhimu wa vitamini C ndani ya mwili wako. Hakikisha kula vyakula vyema ili kusaidia katika kuboresha afya yako. Endelea kuwa pamoja na si kwa makala nyingine za Afya.



MAKALA NYINGINE ZINAZOHUSU:

  1. Vyakula vya Vitamini na faida zake
  2. Afya ya uzazi
  3. magonjwa na Afya
  4. Kitabu cha matunda
  5. Dondoo 100 za Afya


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1868


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

VYAKULA VYA VITAMINI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kabichi
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula kabichi Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu maji, kazizake mwilini na athari za upungufu wake mwilini
Hpa utafahamu faida za maji mwilini pamoja na athari za upungufu wa maji mwilini na dalili zake Soma Zaidi...

Vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin D
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin D Soma Zaidi...

Vyakula vya kuoambana na mafua
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua Soma Zaidi...

Faida za kula Ndizi
Kuna faida kubwa za kiafya kwa kula ndizi, soma makala hii mpaka mwisho Soma Zaidi...

Faida za kula Tango
Matunda ya zamani na ya asili, zijuwe faida za kiafya za tango Soma Zaidi...

Matunda yaliokuwa na vitamini C vingi
Hii ni orodha ya matunda yenye vitamini C kwa wingi sana ikiwemo machungwa, mapera na mapapai Soma Zaidi...

Yafahamu magonjwa nyemelezi kwa watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,. Ni magonjwa yanayowapata watoto wadogo kwa sababu kinga Yao bado ni ndogo. Soma Zaidi...