Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini
NINI MAANA YA PROTINI
Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki ”proteios” likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe “nutrients” ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 1838 na Mkemia kutoka Swedih Jöns Jacob Berzelius.
Protini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng’enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)
Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes
Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika post hii utakwenda kujifunza aina 20 za vitamini. Utajifunza kazu zake mwilini, vyanzo vyake na madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wake.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua
Soma Zaidi...Zitambue aina zote za vyakule na ufanye maamuzi yaliyo kuwa sahihi katika uandaaji wa chakula chako
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula chungwa na chenza (tangarine)
Soma Zaidi...Je unajuwa kuwa majimaji yanayotoka ukeni yanatueleza mengi kuhusu afya yako, rangi za majimaji ya ukeni na damu ya hedhi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vitamini C mwilini
Soma Zaidi...Hivi ni vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo. mwenye vidonda vya tumbo hatakiwi kula vyakula hivi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fenesi
Soma Zaidi...