Posti hii inahusu zaidi vitamini mbalimbali na kazi zake kwenye mwili,vitamini ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama ifuayavyo.
Vitamini na kazi zake
1.Vitamini A
Hii ni Aina ya vitamini ambapo kazi yake kubwa usaidia kwenye kuona, kutengeneza Ute, kuungarisha mifupa na meno pia, kuzaliana na kuongeza kinga mwilini.kwa hiyo kazi ya vitamini A ni kubwa sana mwilini kama tulivyoona hapo juu.
vitamini A upatikana kwenye wanyama mfano nyama, maini, na maziwa, tena upatikana kwenye matunda na mamboga mboga ya majani, pia kwenye mafuta ya mawese na mizeituni tena upatikana kwenye mahindi ya njano, na kwenye viazi vya njano na vyakula vingine mbalimbali.
Ukosefu wa vitamin A usababisha mtu kuwa kopofu, matatizo kwenye lymp node na kwenye ngozi maambukizi ya kila ugonjwa na kukua kunaleta sihida hasa kwa watoto kudumaa, kwa hiyo tunaona hatari iliyopo kwenye kukosa vitamini A kunavyoweza kuleta matatizo mengi na ya hatari kw hiyo tunapaswa kula vyakula vyenye vitamini A kwa wingi.
2. Vitamini D
Vitamini D usaidia katika shughuli mbalimbali kama ifuayavyo, katika kutengeneza na kuimarisha mifupa na meno, kazi ya vitamini D ni kubwa sana hasa kwa mifupa bila vitamini D mifupa uweza kuwa laini na hali hii usababisha magonjwa ya viungo na mgongo kwa sababu ya kuishiwa Vitamini D mwilini.
Vitamini D utokana na mwanga wa jua kwenye mwili hasa hasa jua la asubuhi Lina wingi wa vitamini D kuliko jua lingine kwa hiyo ndo maana watu upenda sana kuota jua la asubuhi Ili kuongeza vitamini D mwilini.na samaki,maini,mayai,nyama, cheese na maziwa navyonuongeza kiasi Cha wingi wa vitamini D mwilini.
Ukosefu wa vitamin D usababisha mifupa kuwa milaini hali ambayo usababisha maambukizi kwenye mifupa kwa hiyo hali hii upelekea maumivu kwenye kiuno, mgongo na sehey nyingine nyingi za mwili, na pia Ukosefu wa vitamini D usababisha meno kuoza na kusababisha madhara makubwa kwenye kinywa na Maambukizi mbalimbali ujitokeza.
3.Vitamini E
Ni vitamini ambavyo usaidia kazi mbalimbali kwenye mwili kama ifuayavyo,usababisha watu kuwa na uwezo wa kuzaliana, tena usaidia kutengeneza haemoglobin ambayo usaidia kubeba damu kutoka sehemu Moja kwenda nyingine na pia usaidia kama Antioxidant kwenye mwili.
vitamini E upatikana kwenye mamboga mboga ya majani kama vile kabeji, mchicha, chainizi,na mboga zote za majani,pia pengine ambapo upatikana kwenye maharage, kunde,njegere, njugu Mawe, karanga na kwenye soya beans pote tunapata vitamini E kwa hiyo kwenye vitu ambapo vitamini E utoka tumeona kwa hiyo tunapaswa kutumia vyakula hivyo.
kwa hiyo tusipopata vitamini E tunaaweza kupata magonjwa ya macho ambayo yanaweza kuleta shida katika maisha yetu hasa kwa watoto wadogo wanapaswa kupata vitamini E Ili kuzuia uharibifu wa macho ambao unaweza kuleta shida kwenye maisha yetu.
4,Vitamini K
Ni vitamini ambavyo usaidia katika mwili wa binadamu kama ifuayavyo, kusaidia damu kuganda pale mtu akipata jeraha damu utoka kama Kuna upungufu wa vitamini K damu uendelee kutoka na kusababisha magonjwa nyemelezi kama Vile Anaemia lakini kama Kuna vitamini K damu utoka na baadae vitamini K usaidia damu hiyo kuganda na Mtu hawezi kupata Anaemia.
vitamini K upatikana kwa wingi katika vyakula mbalimbali kama vile kwenyemboga za majani na Vitamini K utengenezwa na bakteria kwenye utumbo mkubwa na mdogo Aina hii tunaaweza kusema kwamba mwili ujitengenezea vitamini K kutokana na bakteria kwenye mwili. Kama hakuna vitamini K mtu kwenye mwili wa binadamu mtu ana hatari ya kupoteza damu kwa wingi na kusababisha Anaemia.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Kitunguu thaumu ni katika viungo vya mboga na chakula.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kungumanga
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za matumizi ya vyakula vya asili, kama tunavyojua kwamba mababu na mabibi zetu walitumia vyakula vya asili wakaishi miaka mingi kweli.
Soma Zaidi...Zitambue aina zote za vyakule na ufanye maamuzi yaliyo kuwa sahihi katika uandaaji wa chakula chako
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mayai
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin B
Soma Zaidi...