Faida za kula Nazi
Nazi ni katika matunda bora sana kiafya, Soma faida zake kwa afya yako
18.Nazi (coconut oil)
Kunatafiti zaidi ya 1500 zinathibitisha kuwa nazi ni katika matunda yenye afya kuliko matunda yote. Nazi ni katika vyakula vya fati na hutambulika kama medium-chain fatty acids (MCFAs). Ambapo mafuta ya nazi yapo katika aina tatu za fatty asidi ambazo ni Caprylic acid, Lauric acid na Capric acid. Asilimia 62 za mafuta ya nazi yametokana na aina hizi tatu.
Tafiti zinaonesha kuwa mafuta yaliyopo kwenye nazi ni salama kabisa na pia mwili unachukuwa muda mchache kuyameng’enya kuliko mafuta yanayopatikana kwenye minea mingine. Tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya nazi yanapitia hatua kuu tatu tu katika kumeng’enywa wakati huo mafuta yatokayo kwenye mimea mingine yanapitia hatua 26 mpaka kumeng’enywa.
Ulaji wa nazi unasaidia katika kutibu afya ya ubongo pamoja na kuzuia ugonjwa kusahau (Alzheimer’s Disease). Tafiti zinaonesha kuwa ulaji wa aina hizi tatui za mafuta (fatty acid) hupelekea ini kutengeneza ketones. Ketones husaidia katika kuupa ubongo nguvu na afya na uwezo wa kufanya kazi vyema. Pia tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya nazi hulinda mwili kupata magonjwa ya moyo na shinikizo la damu la juu (high blood pressure)
Nazi hutibu UTI, ini na mashambulio kwenye figo. Tafiti zinaonesha lkuwa maji ya nazi yanaweza kutumika kuondoa vijiwe kwenye figo (kidney stones). Pia mafuta ya nazi yanaweza kuondoa na kuuwa bakteria waliop kwenye njia ya mkojo. Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa mafuta ya nazi yanasaidia katika kulinda afya ya ini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kunywa chai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa chai
Soma Zaidi...Faida za kiafya za peaz/ peas
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi
Soma Zaidi...Vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito
Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito, mama mjamzito ni mama ambaye amebeba kiumbe ndani kwa hiyo anapaswa kutumia vyakula vyenye virutubisho mbalimbali vitakavyomsaidia mtoto kukua vizuri.
Soma Zaidi...