picha

Zijue kazi za madini ya chuma mwilini

Posti hii inahusu zaidi kazi za madini ya chuma mwilini,Ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini na pia utokana na vyakula mbalimbali ambavyo upatikana kwenye wanyama na mimea. Zifuatazo ni kazi za madini ya chuma.

1. Madini ya chuma usaidia kusafilisha gasi ya oxygeni kutoka sehemu mbalimbali za mwili na kwenda sehemu nyingine za mwili ambapo oxgeni inahitajika.

 

2. Madini ya chuma usaidia katika kazi za haemoglobini ambayo ubeba gasi ya oxygeni kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na pia haemoglobini hiyo ubeba carbon dioxide kutoka kutoka kwenye sehemu mbalimbali za mwili mpaka kwenye mapafu kwa ajili ya kutafuta oxgeni kwa hiyo kazi ya kusafilisha hizi gasi mbili usaidia na madini ya chuma.

 

3. Madini ya chuma usaidia kusafilisha damu ya oxgeni kwenye misuli ambapo kitendo hiki kwa kitaalamu huitwa myoglobin ambayo ni sehemu ya protein kwenye misuli,kwa hiyo myoglobini asili yake ni protini ambayo inaweza kusafilisha gasi ya oksijeni kwenye misuli, hii kazi usaidiwa na madini ya chuma.

 

4. Madini ya chuma yanasaidia katika upumuaji kwa sababu ya kuwepo kwa cytochrome ambayo ni sehemu ya madini ya chuma, cytochrome usaidia katika kusafirisha hewa wakati wa kupumua, kwa sababu cytochrome imetengenezwa na madini ya chuma, ndo maana tunaaweza kusema kuwa madini ya chuma usaidia katika upumuaji.

 

5. Madini ya chuma usaidia katika kuzalisha protini hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa baadhi ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa madini ya chuma ambayo usaidia kutengeneza protein kwa kitaalamu huitwa xanthine oxidase - enzyme ambayo ni sehemu ya madini ya chuma.

 

6.Madini ya chuma ni sehemu ya enzyme, tunajua kuwa enzyme ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili, kwa hiyo madini ya chuma ni sehemu ya enzyme ambazo kwa kitaalamu huitwa peroxide, catalase na enzyme nyingine nyingi ambazo ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.

 

7.Madini ya chuma usaidia katika kuzalisha homoni ambazo utumika kufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama vile kuhakikisha kiwango Cha sukari kipo sawa kwenye mwili, kutengeneza protini kwenye mwili, kukua na kuzaliana na kazi zote mwilini ambazo utengenezwa na homoni.

 

Wapi tunaaweza kupata madini ya chuma?

1. Madini ya chuma tunaaweza kuyapata katika sehemu mbalimbali kama vile nyama, samaki, vyakula kama vile njegere, maharage,soya beans, njugu Mawe na vyakula vyote ambavyo ni jamii ya kuunde hivi vyote tunaviita kwa kitaalamu heme - iron .Kuna vyakula vingine ambavyo tunaviita non- heme iron kama vile vyakula vinavyopatikans kwenye mboga za majani, mayai na maziwa.

 

Nini madhara ya kukosa madini ya chuma mwilini.

1. Madini ya chuma yakikosa mwilini mtu anaweza kupata upungufu wa damu mwilini ambapo kwa kitaalamu huitwa Anaemia, ambayo upelekea mwili kuchoka, kizunguzungu, kichwa kuuma na mwili una kiss kinga mwilini  kwa hiyo unaweza kupata magonjwa nyemelezi .

 

2. Madini ya chuma yakikosa mwilini mtu anaweza kupata ugonjwa wa kuvimba matezi ambao kwa kitaamu huitwa goitre yaani ni kuvimba kwenye shingo ambapo ugonjwa huu usababisha madhara makubwa kwa watu wengi, kwa hiyo tunapaswa kula vyakula vyenye wingi wa madini ya chuma usaidia sana katika shughuli mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.

 

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 5649

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Faida za kula mayai

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kula mayai

Soma Zaidi...
Naombakujua kujua Kama huu uyoga unasaidia kansa Kama kwawazee

Mpaka sasa hakuna dawa ya kuponyesha saratani wala kinga ya saratani. Hata hivyo vipo vyakula ambavyo vinakadiriwa kuwa hupunguza hatari ya kuweza kupata saratani. Je unadhani uyoga ni moja ya vyakula hivyo?

Soma Zaidi...
Kitunguu saumu

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kitunguu saumu

Soma Zaidi...
Karanga (groundnuts)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha

Post hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo ni vizuri kwa mwanamke anayenyonyesha ili kumsaidia kupata maziwa kwa wingi.

Soma Zaidi...
VYAKULA VYA VITAMINI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...