Navigation Menu



image

Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia, sababu zake na dalili zzake

Hapa utajifunza sababu za kupatwa na maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia

Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia, sababu zake na dalili zzake

MAUMIVU YA TUMBO KWA CHINI UPANDE WA KULIA




Sehemu ya tumbo kwa chini upande wa kulia ndipo ambapo baadhi ya viungo kupatikana kama utumbo mkubwa, appendix, na kwa baadhi ya wanawake ni ovari hupatikana maeneo haya.katika hali za kawaid maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia huwa yanaondoka yenyewe ndni ya siku mbili ama tatu. Ila kwa baadhi ya nyakati kama yanahusiana na shida za afya zaidi matibabu ni lazima yafanyike.



Maumivu haya yatahidaji uangalizi wa karibu wa daktari endapo yatafungamana na dalili zifuatazo:
1.Maumivu na mkandamizo kwenye kifua
2.Homa
3.Damu kwenye kinyesi
4.Kuendelea kwa kichefuchefu na kutapika kwa masiku kadhaa.
5.Ngozi kuwa na rangi ya njano
6.Kukaza kwa tumbo sana unapoligusa
7.Kujaa kwa tumbo




Sababu za maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia
1.Ugonjwa wa Appendix:
Appendix ni sehemu ndigo ambapo utumbo mkubwa hukutana na utumbo mdogo. Sasa sehemu hii hutokea kuathiriwa hivyo hujaa na kuvimba ugonjwa huu unaitwa appendicitis. Hii ni katika sababu kuu za maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia. Tofauti na maumivu haya ugonjwa wa appendix hufungama na na dalili zifuatazo:-
1.Kichefuchefu
2.Kutapika
3.Homa
4.Kuharisha
5.Kukosa hamu ya kula
6.Kujaa kwa tumbo
7.Kukosa hamu ya kula.



2.Kujaa gesi tumboni. Kikawaida ndani ya tumbo kuna gesi, ambayo husababishwa na vuakula tunavyokula. Sasa kila chakula mbacho hakijamengโ€™enywa kinapoongezeka tumboni, yaani unapokula gesi zaidi hujitengeneza tumboni. Wakati gesi inapoongezeka inapelekea kujaa kwa tumbo na maumivu ya tumbo.



Pia mgonjwa atahisi kucheua gesi kwa sauti kutoka mdomoni, pia kujamba mara kwa mara ili kupunguza gesi.endapo tatizo hili litakuwa ni kubwa na endelevu linaweza kuashiria shida nyingine kama kisukari



Sababu nyingine za gesi tumboni:-
1.Kumeza gesi
2.Kula zaidi kupitiliza
3.Kutafuna bigjii
4.Kuvuta sigara




3.kukosa choo
Kukosa choo huleta maumivu baada ya kula ama kunywa kitu. Maumivu haya kikawaida yanatokea sehemu ya juu ya tumbo lakini unayahiisi sehemu ya chini kwa upande wa kulia.



Dalilo za kukosa choo:-
Tofauti na maumivu haya ya tumbo lakini yanaambatana na dalili zifuatazo:-
A.Kiungulia
B.Kujaa tumbo
C.Kushiba mapema
D.Kujuhisi mgonjwa
E.Kucheua gesi mdomoni
F.Kujamba
G.Kucheua chakula ama majimaji machungu




4.Kuwa na henia hutokea pale shehemu ya ya ndani ya tumbo inaponasa kwenye misuli nsani ya tumbo na kupelekea maumivu. Dalili za henia ni pamoja na:-
A.Kuvumba kwa sehemu husika
B.Kuongezeka kwa maumivu
C.Mamivu wakati unaponyanyua kitu, unapocheka, unapolia ama unapokohoa
D.Kuhisi tumbo kushiba, ama kukosa choo.



5.Kuwa na vijijiwe kwenye figo.
Hutokea pale vijichpe vijidogo vigumu vilivyotengenezwa kwa chumvi vikijikusanya kwenye figo. Hali hii ikitokea huleta maumivu mgongoni, chini ya mbavu na chini ya tumbo upande wa kulia.



Dalili nyingine za vijiwe vya kwenye figo
A.Maumivu wakati wa kukojoa
B.Mkojo wenye rangi ya kahawia, nyekundu ama damu ya mzee
C.Mkojo wenye mawinguwingu na unatoa harufu kali
D.Kichefuchefu
E.Kutapika
F.Kuhisi kukojoa mara kwa mara
G.Homa na baridi.



Sababu zinazoathiri wanwake tu
1.Tumbo la hedhi
Maumivu haya yanaweza kutokea kabla na baada ya kubata hedhi. Yanaweza kutokea pande zote yaani kulia na kushoto kwa chini. Maumiv haya yana dalili kama:
A.Maumivu endelevu
B.Maumivu ya chini mgongoni na mapajani
C.Kichefuchefu
D.Kupata kinyesi kilaini
E.Maimivu ya kichwa
F.Kizunguzungu



2.Kuota kwa tishu za tumbo la uzazi mje ya tumbo la uzazi. Kitaalamu hufahamika kama endometriosis. Hali hii inapelekea maumivu ya tumbo kkwa chini, pia huandamana na yafuatayo:
A.Maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada
B.Maumivu unapokojoa
C.Maumivu makali ya umbo la hedhi
D.Hedhi yenye damu nyingi
E.Kutokwa na matone ya damu



3.Matatizo katika ovari au ovarian cyst. Mara nyingi maumivu yanayosabavishw ana atizo hili huondaka yenyewe. Yanaweza kuonyesha dalili kama kujaa kwa tumbo, kuhisi kujaa sana. Kuhisi kushiba sana, maumivu makali ya tumbo kwa chini. Muone daktari kama maumivu yatakuwa na:-
A.Makali sana kupiitiliza
B.Homa
C.Kutapika
D.Baridi kwenye ngozi
E.Kuhema mbiombio
F.Uchovu



4.Ujauzito uliotungia nje (ectopic pregnancy). mgonjwa ataona dalili kama kutokwa na damu ukeni, maumivu mwisho wa mabega na mwanzoni mwa mikono, maumivu wakti wa kukojoa.



5.Ugonjwa wa PID
Dalili za PID
A.Homa
B.Kutokwa na uchafu ukeni
C.Maumivu makali ya chango
D.Kuhisi kama kuunguwa wakati wa kukojoa
E.Kutokwa na damu wakati wa hedhi





                   








           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 16617


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰3 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰5 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula zaituni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula zaituni Soma Zaidi...

Fahamu Fati na kazi zake, vyakula vya fati na athari za upungufu wake
Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu fati, vyakula vya fati, kazi zake na athari za upungufu wake Soma Zaidi...

Boga (pumpkin)
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula maboga Soma Zaidi...

Je ulaji wa boga unafaa kwa mgonjwa wa kisukari?
Je ulaji wa boga unafaa kwa mgonjwa wa kisukari? Soma Zaidi...

Faida za ubuyu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ubuyu Soma Zaidi...

Vyakula vya kuoambana na mafua
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua Soma Zaidi...

vitamini B na makundi yake
Makala hii inakwenda kukuletea kazi za vitamini B, pia tutajwenda kuona makundi ya vitamini B na kazi za kila kundi. Pia makala hii inakwenda kukufundisha vyanzo na vyakula vya vitamini B. Utajifunza pia kazi kuu za vitamini B kw Soma Zaidi...

KITABU HA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

VYANZO VYA VYAKULA VYA FATI, PROTINO NA WANGA NA FAIDA ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

VYANZO VYA VYAKULA VYA VITAMINI NA FAIDA ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kitabu cha Afya 02
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kunywa chai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa chai Soma Zaidi...