Fahamu vyakula vya nyuzinyuzi
Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga.
Moja kwa moja tuone matunda yanayokuwa na nyuzinyuzi na huwa na Faida gani;
1. Parachichi; hili Ni tunda lenye nyuzinyuzi na linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye Matatizo ya Vidonda vya tumbo, Na nyuzinyuzi hizo Ni muhimu kukinga kuta za utumbo,. Pia husaidia watu wenye maradhi ya upungufh wa damu, kisukari, Matatizo ya mfumo wa Neva na maradhi mengine mengi watu hawa wanatakiwa kula tunda hili kwa wingi ili kuboresha Kinga ya mwili.
2.chungwa: nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye chungwa huwa na vitamini C pia husaidia kuponesha Vidonda hivyo tunda hili ukilila kula pamoja na nyuzinyuzi zake tafuna mapaka zile kamba zake kwasababu zinasaidia usagaji wa chakula tumboni ( digestion) japo kuwa watu wengi hunyonya maji yalliyopo kwenye chungwa na kutupa nyuzinyuzi haishauriwi kula hivyo.
3.Embe; tunda hili hiwa na nyuzinyuzi nyingi Sana ambazo huweza Kuzuia Saratani, pia huborasha Uwezo wa kumbukumbu na kufikiria kwa wingi hivyo watu tusipuuzie kula embe.
4. Nanasi: Ni tunda ambalo Lina sukari na Ni tamu Sana tunda hili Lina nyuzinyuzi ambazo Zina virutubisho vingi na vingine vinauwezo was kuupa mwili wAko Kinga dhidi ya Magonjwa tunda hili Lina vitamini C na madini ya chuma.
5. Ndizk mbivu; nyuzinyuzi za kwenye ndizi mbivu husaidia Sana Katika usagaji wa chakula tumboni,pia tunda hili Lina Uwezo wa kuimarisha nishati ya mwili. Mwili kuwa na nguvu na pia huweza kuongeza uzito. Hivyo hushauriwa kwa wale wenye uzito kupitiliza waepuka kutumia ndizi.
6. Papai; Hilo Ni tunda ambalo husaidia vitu vingi mwilini Kama vile kuua minyoo na kuondoa mazalia ya minyoo tumboni, na husaidia kwa wale wenye Vidonda vya tumbo Na kuboresha Kinga ya mwili.
Mboga mboga hasa za majani husaidia tumbo kusukuma uchafu wote tumboni hasa kwa wale wanaopenda kula vyakula vilivyokobolewa na vigumu kwani Magonjwa yote yanaanzia tumboni ndipo yanasambaa mwilini;.
1. Kabeji; ni mojawapo ha mboga yenye nyuzinyuzi ambayo hutibu Matatizo ya choo kigumu, na husaidia kuponesha haraka Vidonda vya tumbo vile vile husaidia kupunguza uzito uliozidi pamoja na kuondoa sumu mwilini.
2.Mchicha Hii pia Ni mboga ya majani ambayo Ina nyuzinyuzi nyingi na zinazosadia kuboresha mwili, Kinga ya mwili pia husaidia kwa wale wasioona endapo watatumia kwa wingi mboga hii.
3. Matembele; Ni mboga ambazo hupatikana kwenye majani ya viazi ambayo pia hutoa nyuzinyuzi matembele Yana vitamini A na vitamini C ambazo huimarisha Ngozi na fizi, endapo fizi zako zinatoa Damu Ni vyema kutumia matembele kwa wingi kwani husaidia kuponesha na pia mboga hii huwa na protini pia.
4. Spinachi; mboga hii pia Ina nyuzinyuzi ambayo Ina potassium kwa wingi, vitamini C na vitamini E ambazo zinasaidia kuimarisha afya ya Ngozi na pia kuimarisha Ngozi da Damu kuganda pia.
Mwisho; hizi Ni baadhi ya mboga mboga na matunda yenye nyuzinyuzi Ila vyakula hivi Ni muhimu Sana endapo vikizingatiwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 ai web app 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Kazi kuu tatu za Vitamini C mwilini
Vitamini C tunaweza kuvipata kwenye matuinda kama machunwa vina kazi kuu tatu ambazo ni hizi hapa
Soma Zaidi...VYAKULA VYA PROTINI, FATI NA MAFUTA
Je! unatambuwa madhara ya vyakula vya protini na mafuta? ungana nasi kwenye somo hili
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula panzi, senene na kumbikumbi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula panzi senene na kumbikumbi
Soma Zaidi...Fahamu virutubisho vya wanga na kazi zake, vyakula vya wanga na athari za upungufu wake
Hapa tutaona kuhusu virutubisho vya wanga, kazi zake na athari za upungufu wake
Soma Zaidi...Faida za kula apple (tufaha)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha
Soma Zaidi...Sababu zinazoweza kusababisha kukosa choo (kinyesi)
Kukosa choo aina ya kinyesi ni kutoweza kudhibiti kinyesi, hivyo kusababisha kinyesi kuvuja bila kutarajiwa kutoka kwenye puru. Pia huitwa kutoweza kudhibiti utumbo, Upungufu wa kinyesi hutoka kwa kuvuja mara kwa mara kwa kinyesi huku ukipitisha gesi had
Soma Zaidi...