picha

Vyakula salama na vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo

Kamala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

VYAKULA HATARI NA VYAKULA SALAMA KWA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo ni moja kati ya maradhi yanayosumbuwa watu kutokana na kuchelewa kwake kupona hata baada ya kutumia dawa nyingi. Hali hii husababishwa kutokana na kutofata masharti ya vidonda vya tumbo vyema. Mgonjwa anatakiwa kufata masharti, ajuwa ni vyakula vipi atumie na vipi asitumie. Kamala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Pia makala hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo hutumuka kama dawa kwa ajili ya kutibu maradhi hususan vidonda vya tumbo. Mwisho wa makala hii utaweza kujifyunza ni kwa nini vidonda vingine haviponi, na vidonda sugu vinatokeaje.



Vyakula salama kwa wenye vidonda vya tumbo
1.Kabichi
2.Maepo
3.Karoti
4.Mboga za kijani
5.Asali
6.Kitunguu thaumu



Vyakula salama kwa vidonda vya tumbo pia ni dawa
1.Juisi ya kabichi
Kabihi ni katika mboga ambazo zina vitamini C. vitamini hii pia ni katika antioxidant ambayo husaidia katika kupambana na bakteria aina ya H.pylori ambao ndio chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo.

2.Asali
Asali nikatika baadhi ya vyakula ambavyo huhusishwa na matibabu mbalimbali. Asali husaidia kuimarisha afya ya moyo, pia hutumika kama dawa kwenye majeraha na majeraha ya moto ili kuzuia bakteria. Asali inaweza pia kupambana na bakteria wa kusababisha vidonda vya tumbo

3.Kitunguu thaumu.
ni katika viungo vya mboga kama kinavyotumika.lakini pia ni katika tiba za asili ambazo hutumiwa maeneo mengi duniani. Tafiti zinaonyesha kuwa katika kitunguu thaumu kuna chembechembe ambazo husaidia katika kupambana na bakteria aina ya H.pylori ambao ndio chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo.

4.Shubiri
Shubiri si katika vyakula ila hutumika sana katika viwanda vya vyakula, urembo na viwanda vya kutengeneza madawa. Shubiri ni katika tiba asili ambazo hutumiwa maeneo mbalimbali duniani. Tafiti zinaonyesha kuwa shubiri lina uwezo wa kuzuia mashambulizi ya bakteria kwenye ngozi. Pia shubiri limeonekana kuwa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.



Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo:
1.Maziwa.
Wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanatambuwa kuwa akinywa maziwa maumivu yanapunguwa. Hii ni faida, lakini tafiti zinaonyesha kuwa maziwa yanaongeza uzalishwaji na utaji wa tindikali za tumboni. Tindikali hizi zina mchango sana katika kusababisha vidonda vya tumbo

2.Pombe
Unywaji wa pombe unaweza kuathiri na kuharibu kuta za tumbo na utumbo. Hali hii inaweza kuongeza hatari ya kuweza kupata vidonda vya tumbo. Ama inaweza kusababisha hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

3.Kahawa;
Kahawa inaweza kusababisha kuongezeka kwa uzalishwaji wa tindikali za tumboni (stomach acid). tindikal hizi zikizalishwa kwa wingi tumboni zinaweza kuchubuwa ukuta wa tumbo na hatimaye kusababisha vidonda vya tumbo

4.Vyakula vyenye mafuta na fati kwa wingi.
5.Pilipili kali vyema kupunguza kuzitumia
6.Vyakula vyenye chumvi nyingi
7.Vyakula vya kuoka
8.Vyakula vyenye uchachu
9.Wacha kuvuta sigara



SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO SUGU
Vidonda vya tumbo ambavyo haviponi na matibabu huitwa vidonda sugu. Kuna sababu nyingi kwa nini kidonda kinaweza kushindwa kuponya, pamoja na:
1. kutokuchukua dawa kulingana na maelekezo
2. Kuwepo kwa bakteria sugu. Ukweli kwamba aina fulani za H. pylori ni sugu kwa antibiotics (dawa).
3. Matumizi ya mara kwa mara ya tumbaku (sigara)
4. Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kupunguza maumivu - NSAIDs na aspirini ambayo huongeza hatari ya vidonda.
5.Matumizi ya dawa isiyo sahihi. Vidonda vya tumbo vitibiwekutokana na asili. Kama asili ni bakteria kwanz amtu apewe dawa ya kuuwa bakteria.



SABABU NYINGINE
Wakati mwingine, vidonda sugu vinaweza kuwa matokeo ya:
1. Uzalishaji mkubwa wa asidi tumboni,
2. Maambukizo mengine yasiyokuwa ya bakteria aina ya H. pylori
3. Saratani ya tumbo
4. matumizi ya vyakula na vinywaji visivyo salama

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 3106

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Matunda yenye Vitamin C kwa wingi

Vitamin C ni katika vitamin vinavyosaidia sana mfumo wa Kinga kulinda mwili dhidi ya vimelea vya maradhi. Hapa nitakuletea orodha ya matunda ambayo yana vitamini C kwa wingi.

Soma Zaidi...
utaratibu wa lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
Nini maana ya protini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha

Post hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo ni vizuri kwa mwanamke anayenyonyesha ili kumsaidia kupata maziwa kwa wingi.

Soma Zaidi...
Fahamu vitamini C na kazi zake, vyakula vya vitamini C na athari za upungufu wake.

kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.

Soma Zaidi...
Faida za kula viazi mbatata

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula viazi mbatata

Soma Zaidi...