Waliomuamini Nabii Nuhu(a.s)


Waliomuamini Nuhu(a.s) walikuwa watu wachache tena wale waliokuwa wanyonge na dhaifu katika jamii. Uchache na udhaifu wa waumini ilitumiwa na makafiri wa wakati wake kama hoja ya kumkataa Nuhu kuwa si Mtume wa Allah(sw).
“Wakasema: Je, tukuamini wewe hali ya kuwa wanyonge ndio wanaokufuata? (26:111)Uchache wa waumini waliokuwa pamoja na Nabii Nuhu(a.s) unadhihiri vizuri pale walipo weza kuenea kwenye safina ndogo iliyosheheni mizigo yao na jozi za wanyama mbali mbali kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
“Hata ilipokuja amri yetu na ardhi ikaanza kufoka maji tulimwambia (Nuhu) Pakia humo (jahazini) jozi moja katika kila (nyama, jike na dume) na wapakie watu wako wa nyumbani kwako isipokuwa wale ambao imewapitia hukumu (ya Mwenyezi Mungu). Na (wachukue wote) walioamini.” Na hawakuamini pamoja naye ila wachache tu.” (11:40)
Wapinzani wa Ujumbe wa Nabii Nuhu(a.s) na Vitimbi Vyao


Waliokuwa mstari wa mbele katika kupinga ujumbe wa Nabii
Nuhu(a.s), ni viongozi wakuu wa jamii yake.Wakuu wa watu wake wakasema: Sisi tunakuona umo katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri (kwa kutukataza haya tuliyowakuta nayo wazee wetu)” (7:60)Katika kukataa ujumbe wa Nabii Nuhu(a.s), viongozi wa makafiri walitoa hoja dhaifu zifuatazo:

“Na hapa wakasema wakubwa wa wale waliokufuru katika kaumu yake. Hatukuoni ila ni mtu tu sawa nasi; wala hatukuoni ila wamekufuata wale wanaoonekana dhahiri kuwa ni dhaifu (wanyonge) watu, (wamekufuata) kwa fikira ya mawazo tu (bila kupeleleza vizuri) wala hatukuoneni kuwa mnayo ziada juu yetu; bali tunakuoneni kuwa ni waongo. (11:27)
Wakasema wale wakuu waliokufuru katika watu wake: “Hakuwa huyu (Nuhu) ila ni mtu kama nyinyi. Anataka kujipatia ubora juu yenu. Na kama Mwenyezi Mungu angependa (kukufundisheni), kwa yakini angateremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa wazee wetu wa mwanzo.” (23:24)Hakuwa huyu ila ni mtu mwenye wazimu. Basi mngojeeni hata muda (wake atakufa).” (23:25)Kwa mujibu wa aya hizi makafiri walikataa Utume wa Nabii
Nuhu(a.s) kwa Sababu:Alikuwa mtu kama wao. Walitarajia kutumiwa Malaika.

Waliomuamini walikuwa watu dhaifu kiuchumi na hadhi.

Kwa upande mmoja, hawakuona faida yoyote iliyopatikana

kwa waumini kutokana na kuamini kwao na kwa upande mwingine, hawakuona hasara yoyote waliyoipata kutokana na huko kukufuru kwao.

Walimuita Nabii Nuhu mwenda wazimu:Kabla yao watu wa Nuhu walikadhibisha nao. Walimkadhibisha mja wetu na wakasema ni mwendawazimu, na akawa anatolewa maneno makali”. (54:9)

Na walimtishia kumuua:“Wakasema: Kama hutaacha, Ewe Nuhu (nasaha zako hizi), bila shaka utakuwa miongoni mwa wanaorujumiwa (wanaopigwa kwa mawe mpaka wafe)”. (26:116)