Ismail(a.
Ismail(a.s) ni mtoto wa kwanza wa Mtume Ibrahim(a.s.). Alizaliwa wakati uzee umekwishamfikia Ibrahim(a.s). Kama Qur’an inavyobainisha, katika umri huo wa uzeeni, MtumeIbrahiim(a.s) alimuomba Mola wake ampe mtoto mwema atakaendeleza harakati za Kiislamu.
“Ee Mola wangu! Nipe (mtoto awe) miongoni mwa watenda mema.” Ndipo tukampa habari njema ya (kuwa atapata) mtoto mpole. (Basi akapata. Naye ndiye Nabii Ismail).” (37:100-101).
Mtume Ibrahim(a.s.) aliletewa mitihani migumu miwili juu ya mtoto huyu. Mosi ni kule kuamriwa kumwacha yeye pamoja na mama yake katika bonde kavu lisilo na watu wala maji. Hilo lilikuwa bonde la Makka. Maji ya kisima zamzam yaliyo katika Msikiti wa Makka, aliyabubujisha Allah(s.w) kwa ajili ya Ismail na mama yake. Chem-chem hiyo imedumu hadi leo. Aidha, vilima vya Safa na Marwa vimepata umaarufu na kuwa miongoni mwa alama muhimu katika Uislamu, kutokana na kitendo cha mama yake Ismail Hajirah, kukimbia baina ya vilima hivyo katika jitihada za kumtafutia mwanae Ismail maji.
Mtihani mwingine alioupata MtumeIbrahiim(a.s) juu ya Ismail(a.s) ni kule kuamrishwa amchinje. Huu haukuwa ni mtihani kwa baba tu, lakini pia mtoto Ismail(a.s). Hebu fikiri ungekuwa katika hali gani, kama ungekuwa mahali pa Ismail(a.s). Baba yako anakwambia ameamrishwa na Allah(s.w.) akuchinje! Hakika ni mtihani mgumu ila kwa wale wanaonyenyekea kikweli kweli kwa Muumba wao.
Qur’an yatufahamisha kuwa Ismail alikuwa mpole na mnyenyekevu kwa Mola wake. Kwa hiyo hakusita kutoa nafsi yake kwa ajili ya Muumba wake. Bali alimhimiza baba yake amchinje kama Allah(s.w) alivyomuamrisha.
Basi alipofikia (makamu ya) kwenda na kurudi pamoja naye akamwambia: “Ee mwanangu! Hakika nimeona katika ndoto ya kwamba ninakuchinja. (Na ndoto ya Mitume ni Wahayi). Basi fikiri,waonaje?”Akasema:“Ee baba yangu! Fanya unayoamrish wa, utanikuta Inshallah miongoni mwa wanaosubiri”.(37:102).
Utii na unyenyekevu huu wa Nabii Ismail(a.s) ni kielelezo muhimu kwetu. Kwamba, amri ya Allah(s.w) ni lazima itiiwe kwa gharama yoyote ile ikiwa ni pamoja na roho zetu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2556
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitabu cha Afya
Imam Muhammad Idris al-Shafii
Soma Zaidi...
Nabii Yunus(a.s) Amuomba Allah(s.w) Msamaha
Ndani ya tumbo la samaki, Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...
MASWALI MUHIMU KUHUSU HISTORIA NA MAISHA YA MTUME (S.A.W)
1. Soma Zaidi...
Mjadala juu ya ndoa ya Mtume Muhammad s.a.w na bi Khadija.
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 16. Hapa utajifunza maandalizi wa mjadala wa ndoa hizi. Soma Zaidi...
MTUME(S.A.W) KULINGANIA UISLAMU MAKKA
Historia ya harakati za Mtume(s. Soma Zaidi...
HISTORIA YA KUUMBWA KWA NABII ADAMU (A.S)NA HADHI YAKE NA HADHI YA WANAADAMU DUNIANI
Adam(a. Soma Zaidi...
Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...
Hatua mbili kuu za kushuka kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII SULEIMAN
Soma Zaidi...
Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi
Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri. Soma Zaidi...
KAZI ALIZOFANYA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KABLA YA UTUME
KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S. Soma Zaidi...
Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki
Soma Zaidi...