Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a.
Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a.s) naye kwa kuzingatia mazingira ya watu wake, alitumia mbinu zifuatazo katika kuulingania Uislamu:
Kwanza, alijieleza kwa uwazi kuwa yeye ni Mtume wa Allah(s.w)
“Bila shaka mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.” (26:143)
Pili, aliwakumbusha watu wake neema za Allah(s.w) zilizo juu yao ili waone umuhimu wa kumshukuru na kumuabudu ipasavyo:
“Na kumbukeni (Mwenyezi Mungu) alivyokufanyeni makhalifa baada ya ‘Ad na kukuwekeni vizuri katika ardhi mnajenga majumba makubwa ya kifalme katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika majabali (yake). Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu, wala msifisidi katika ardhi kwa kufanya uharibifu.” (7:74)
“Je (mnafikiri kuwa) mtaachwa salama katika haya yaliyopo hapa (kwenu):” “Katika mabustani na chemchem, (mito).” “Na mimea na mitende yenye makole mazuri.” “Na mnachonga milimani majumba mkistarehe tu basi.” (26:146-149)
Tatu, aliwanasihi na kuwasisitiza watu wake wamche Allah(s.w)
na kumtii yeye badala ya kuwatii watu:
“Mcheni Allah na mtiini. Wala msitii amri za wale maasi (wenye kupindukia mipaka ya Allah). Ambao wanafanya uharibifu tu katika ardhi wala hawaitengenezi.” (26:150-152)
Nne,alisisitiza kutohitajia ujira kwa watu wake, kama walivyozoea kutoa ujira kwa viongozi wao kwa ajili ya manufaa na starehe zao binafsi.
“Wala sikutakini ujira juu yake, ujira wangu hauko ila kwa Mola wa walimwengu wote.” (26:145)
Tano, alionyesha muujiza wa jabali kuzaa ngamia jike kama dalili za Utume wake baada ya watu wake kumtaka afanye hivyo kwa uwezo wa Allah(s.w).
Akasema: “Enyi watu wangu! Mnaonaje, kama ninazo dalili zilizo wazi zitokazo kwa Mola wangu (za kunionyesha ukweli wa haya), naye amenipa rehema kutoka kwake, basi ni nani atakayeninusuru kwa Mwenyezi Mungu kama nikimuasi? Basi hamtanizidishia kwa hayo mnayonitakia ila khasara.(11:63)
Enyi watu wangu! Huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ni Ishara kwenu (mliyoitaka kwangu ili kuonyesha ukweli wa Utume wangu). Basi muacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu; wala msimguse kwa ubaya isije ikakuangamizeni adhabu iliyo karibu (na kukufikieni).” (11:64)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 ai web app 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.
Soma Zaidi...Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.
Soma Zaidi...Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Makubaliano ya Mkataba wa Al Fudhul
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.
Soma Zaidi...