Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)

8.

Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)

HISTORIA YA UISLAMU BAADA YA KUTAWAFU MTUME (S.A.W) HADI LEO.

8.1. Ukuaji na Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Wakati wa Makhalifa Wanne Waongofu

Makhalifa wanne wa Mtume (s.a.w) waongofu walioendeleza Dola ya Kiislmu ni;

1. Abu Bakar Sswiddiq (r.a) kutoka mwaka 11 A.H – 13 A.H.

2. Umar Ibn Khattab (r.a) kutoka mwaka 13 A.H – 24 A.H.

3. Uthman bin Affan (r.a) kutoka mwaka 24 A.H – 36 A.H

4. Ali bin Abu Twalib (r.a) kutoka mwaka 36 A.H – 41 A.H



Uchaguzi wa Makhalifa wanne waongofu

1. Kuchaguliwa Abu Bakar Sswiddiq (r.a) kuwa Khalifa

- Mtume (s.a.w) mpaka anatawafu, hakuusia nani awe khalifa baada yake.

- Abu Bakar (r.a) alipendekezwa na Umar Ibn Khattab (r.a), na Answar wengi walikubali pendekezo hilo kutokana na sifa zifuatazo:
i. Sifa zilizopelekea Abu Bakar (r.a) kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Dola ya Kiislamu ni pamoja na;

1. Ucha – Mungu



2. Ujuzi wa kutosha wa Qur’an na Sunnah

3. Tabia njema

4. Siha (afya) nzuri



ii. Alisilimu akiwa mtu mzima na alikuwa karibu sana na Mtume (s.a.w)

kuliko sahaba yeyote yule.

Rejea Qur’an (9:40)



iii. Mtume (s.a.w) alimteua kuongoza swala kwa niaba yake alipokuwa mgonjwa.
iv. Alikuwa mwenye msimamo, maamuzi, ikhlas na uoni mpana kwa kufuata ipasavyo nyayo na mwenendo wa Mtume (s.a.w)



2. Kuchaguliwa Umar Ibn Khattab (r.a) kuwa Khalifa baada ya Abu Bakar (r.a)

- Abu Bakar (r.a) alipokaribia kutawafu aliitisha shura na kumpendekeza

Umar Ibn Khattab (r.a) kuwa Khalifa baada yake kutokana na sifa zake.

- Walikuwepo wajumbe wengi miongoni mwao ni pamoja na;

1. Umar Ibn Khattab (r.a) o Uthman bin Affan (r.a) o Ali bin Abi Twalib (r.a) o Zaid bin Thabit (r.a)
2. Abdul – Rahman bin Auf (r.a)

3. Muadh bin Jabal

4. Ubay bin Ka’ab (r.a) na wengineo katika Muhajirina na Answaar.



- Baada ya shura, wajumbe wote walikubali pendekezo la Abu Bakar (r.a)

kuwa Umar bin Khattab (r.a) achukue nafasi ya kuongoza Dola ya Kiislamu.



3. Kuchaguliwa Uthman bin Affan (r.a) kuwa Khalifa

- Umar (r.a) alipendekekeza watu sita wenye sifa za kuongoza Dola ya

Kiislamu ambao ni;

1. Uthman bin Affan (r.a)

2. Ali bin Abu Twalib (r.a)

3. Saad bin Waqqas (r.a)

4. Talha (r.a)

5. Zubair bin Awwam (r.a) na

6. Abdul – Rahman bin Auf (r.a)



- Siku ya tatu baada ya kutawafu Umar Ibn Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a) alichaguliwa na jopo la masahaba baada ya Abdul – Rahman bin Auf (r.a) na wengineo kujitoa.


- Siku ya nne, Uthman bin Affan (r.a) alitangazwa rasmi na kupewa bai’at

kuwa ndiye kiongozi wa Dola ya Kiislamu.



4. Kuchaguliwa Ali bin Abi Talib (r.a) kuwa Khalifa

- Baada ya miaka sita tu ya uongozi wa Ali bin Abi Talib (r.a), fitna ilizushwa na Myahudi aliyesilimu kwa uongo, Abdallah bin Sabaa.


- Waislamu waligawanyika makundi mawili, moja linakubaliana na uongozi wa Ali bin Abi Talib (r.a) na jingine kupingana nao.

- Sababu za kugawanyika ni kudai kuwa Khalifa Ali (r.a) halipizi kisasi kwa wauaji wa Uthman bin Affan (r.a), makundi hayo yalikuwa ni;

i. Wafuasi wa Uthman – (Uthmanis);

- Wao walitaka Dola iwaadhibu wauaji wa Uthman bin Affan (r.a).



ii. Marafiki wa Ali – (Shian – Ali)

- Ndilo kundi la watu wa mji wa Kufa na Misr lililomuua Khalifa

Uthman (r.a)



iii. Mashibah

- Ni kundi la waislamu waliokwenda Jihad wakati Khalifa Uthman

(r.a) anauawa, hawakuwaunga mkono ‘Uthmanis wala Shian – Ali’



iv. Ahli – Sunnah Wal- Jama’ah

- Lilikuwa ndilo kundi lenye masahaba wengi katika Dola yote ya

Kiislamu.

- Takriban uongozi wote wa Khalifa Ali (r.a) ulikumbwa na migogoro iliyopelekea kuuawa kwake.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 3973

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Historia ya Vijana wa Pangoni

Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
KIKAO CHA KUMFUKUZA MTUME MUHAMMAD KUTOKA MAKKAH (MAKA), KIKAO ALICHOHUDHURIA IBLISI

KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKAHiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka.

Soma Zaidi...
Historia ya Dhulqarnain

Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: “Mwenye Pembe Mbili”.

Soma Zaidi...