Mafunzo yatokanayo na vita vya uhudi

Mafunzo yatokanayo na vita vya uhudi

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Mafunzo yatokanayo na Vita vya Uhudi.

  1. Lengo la maadui wa Uislamu na waislamu kupigana ni kuwaangamiza wao, kuharibu miji yao na mali zao pia. Hivyo ni wajibu waislamu kuwa na tahadhari muda wote kupambana na maadui wao.

 

  1. Kushauriana katika kupanga mambo ni jambo la busara sana, kama alivyoshauriana Mtume (s.a.w) juu ya sehemu ya kupiganwa vita vya Uhudi.

Rejea Qur’an (3:159) na (3:166-167).

 

  1. Tunajifunza pia ni wajibu waislamu kutumia mbinu, ujuzi, uzoefu, na jitihada za kivita pamoja na kuwa wanapata msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (8:60).

 

  1. Msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa waislamu unapatikana pale tu waislamu watakapotii amri zake na wakapigania dini vilivyo.

Rejea Qur’an (3:151-152).

 

  1. Kuvunja na kutotii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake hupelekea kutofikia mafanikio hata kama watajizatiti na kufanya jitihada ipasavyo.

Rejea Qur’an (3:152), (3:165) na (33:36).

 

  1. Tunajifunza pia, makosa ya watu wachache yasipuuzwe na kufumbiwa macho bali yarekebishwe kwani athari yake itasibu jamii nzima.

Rejea Qur’an (8:25).

 

  1. Mwenyezi Mungu (s.w) anatukumbusha kuwa pepo haipatikani kwa kutamani, lele mama na ushabiki bali, kufanya jitihada ya kweli.

Rejea Qur’an (3:142-150), (3:156-160) na (3:169-171).  

 

  1. Msamaha na nusura ya Mwenyezi Mungu (s.w) upo karibu kwa waislamu pindi watakapotubia na kurejea kwake na kupambana na maadui ipasavyo.

Rejea Qur’an (3:152-154), (3:166-167) na (3:139-141).

 

  1. Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.

Rejea Qur’an (3:123-124), (8:42-45).

 

  1. Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views: 3046

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)

(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.

Soma Zaidi...
Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri

Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji.

Soma Zaidi...
Kusilimu kwa Wachawi wa Firaun

Mawaziri waliokuwa washauri wakuu wa Firauni wakataka wakusanywe magwiji waliobobea katika uchawi nchi nzima, kisha wapambanishwe na Nabii Musa(as).

Soma Zaidi...