Tukirejea Qur’an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.
Tukirejea Qur’an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.s). Pamoja na Nabii Nuhu(a.s) kuahidiwa kuwa watu wake wa nyumbani watakuwa miongoni mwa watakaookolewa na gharka, mtoto wake alikataa kuingia kwenye jahazi(safina) na akawa ni miongoni mwa wenye kuangamia kama tunavyo jifunza katika aya zifuatazo.
Na akasema(Nuhu):”Pandeni humo, kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwe kwenda kwake na kusimamma kwake. Hakika Mola wangu ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu.
Ikawa hiyo (jahazi) inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe aliyekuwa mbali amekataa kuingia jahazini: “Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi wala usiwe pamoja na makafiri”. Na akasema (huyo mtoto)” “Nitaukimbilia Mlima utakaonilinda na maji” Akasema(Nuhu): “Hakuna leo wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule atakayemrehemu (Mwenyezi Mungu).” Mara mawimbi yakaingia baina yao na akawa miongoni mwa waliogharikishwa. (11:41-43)
Baada ya gharika kuisha, Nabii Nuhu(a.s) Ilibidi amuelekee Mola wake kutaka kujua ni vipi mwanawe amekuwa miongoni mwa walioangamia.
Na Nuhu alimuomba Mola wake (alipomuona mwanawe anaangamia) akasema: Ewe Mola wangu! Mwanangu ni katika watu wa nyumbani kwangu (mbona anaangamia)? Na hakika ahadi Yako ni haki; nawe ni mwenye haki kuliko mahakimu (wote).”Akasema (Mwenyezi Mungu): “Ewe Nuhu! Huyu si miongoni mwa watu wako. Yeye ni (mwenye) mwenendo usiokuwa mzuri. Basi usiniombe ambayo huyajui. Mimi nakunasihi usiwe miongoni mwa wajinga.” (Nuhu) Akasema: Ee Mola wangu! Mimi najikinga kwako nisije kukuombatena nisiyoyajua; na kama hutanisamehe na kunirehemu nitakuwa miongoni mwa watakaopata khasara.”(11:45-47)
Pia tunahamishwa juu ya kuangamia mke wa Nuhu(a.s) katika aya ifuatayo:
Mwenyezi Mungu amepiga (anapiga)mfano wa wale wabaya waliokufuru, ni mkewe Nuhu na mkewe Luti. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili hao miongoni mwa waja wetu (wema)’ lakini(wanawake hao), waliwafanyia khiana (waume zao watukufu hao) na (waume zao hao) hawakuweza kuwasaidia
chochote mbele ya Mwenyezi Mungu na ikasemwa: “Uingieni
Moto pamoja na hao wanaouingia.” (66:10)
Kuangamia kwa mtoto na mke wa Nuhu(a.s) pamoja na mke wa Lut(a.s) tunajifunza kuwa mtu hataokoka na ghadhabu ya Allah(s.w) kutokana a unasaba alioonao na watu wema na wala hata faidika na malipo ya amali njema walizofanya wengine. Kinyume chake hataadhibiwa mtu mwema kwa kuwa na unasaba na watu waovu maadamu anawafikishia ujumbe na wakamkanusha kama tunavyopigiwa mfano wa mke wa firaun,aliyekuwa mcha-mungu.
Na Mwenyezi Mngu amepiga, (anapiga) mfano wa wale walioamini kweli, ni mkewe Firauni, aliposema; “Ee Mola wangu! Nijengee nyumba Peponi karibu yako na uniokoe na Firauni na amali zake (mbovu), na Niokoe na watu madhalimu”(66:11)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.
Soma Zaidi...(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s.
Soma Zaidi...Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi.
Soma Zaidi...Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:- (1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo.
Soma Zaidi...