Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Maana.
Maana ya funga kisheria ni kujizuia na vyenye kufunguza toka kuchomoza kwa alfajiri mpaka kuzama kwa jua pamoja na kuwa na niya ya kufanya ibada kwa ajili ya Allah. Fadhila za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Kwa hakika hiyo funga ni yangu, na mimi ndiye ninayeilipa ( thawabu) na funga ni ngome. Basi atakapfunga mmoja wenu asizungumze maneno ya upuuzi, wala asifanye mambo machafu na ya kijinga. Basi ikitikea mtu amemtukana au kumpiga yeye (asilipize) bali amwambie “nini mimefunga”. Na akasema Mtume (s.a.w) “na ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo kwenye mkono wak: hakika harufu ya mdomo wa mwenye kufunga inapendeza zaidi mbele ya Allah siku ya kiyama kuliko harufu ya mafuta ya misk. Na ana mwenye kufunga furaha mbili: atakapofutari na atakapokutana na Mo;a wake atafurahia funga yake. (Bukhari na Muslim) Amesema Mtume kuwa Mwenye kufunga ramadhani akiwa na imani na na kutarajia malipo kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.(Bukhari na Muslim) Amesema Mtume kuwa: hakika kuna peponi mtango unaitwa BABU RAYAAN watauingia mlango huo wenye kufunga siku ya kiyama. Na hatauingia mlango huo yeyote isipokuwa watu hao tu na itasemwa “waku wapi wenye kufunga” basi hapo watasimama na hataingia yeyote isipokuwa wao, na pindi watakapoingia utafungwa na katu hataingia yeyote. (Bukhari na Muslim) Mgawnyiko wa funga.
Basi jua ewe ndugu kuwa funga zimegawanyika katika makundi makuu mawili nayo ni :
1.funga za wajibu (lazima)
2.Funga za sunnah (zisizo za lazima) 1.funga za wajibu
Hugawanyika funga hizi katika makundi makuu matatu ambayo ni:
1.funga ambazo ni wajibu kwa kuingia wakati maalum. Nayo ni funga ya ramadhani
2.Funga amabzo ni wajibu kutokana na ‘ila nayo funga za kafara
3.Zilizo wajibu kwa kujiwajibishia mtu mwenyewe. Nazo ni funga za nadhir
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali.
Soma Zaidi...Hapabutajifunza endapp mwanamke anahitaji kuachwa ni nini anatakiwa afanye.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh
Soma Zaidi...