image

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)

Mtume(s.

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)


Mtume(s.a.w) alipoanza kutangaza ujumbe kwa watu wote alipata upinzani mkali. Wapinzani wakuu walikuwa wakuu au watu maarufu wa jamii yake(wadau) miongoni mwa viongozi, matajiri na mamwinyi wa Kiquraysh. Upinzani wao ulisababishwa na hofu ya kuponyokwa na maslahi yao waliyokuwa wakiyapata kwa njia za batili kupitia mkondo wa siasa kandamizi, uchumi haramu na itikadi za kishirikina. Makafiri wa Kiquraysh waliongozwa na wakuu wa jamii yao, walifanya juhudi kubwa katika kuuzima Uislamu kwa kufanya vitimbi vifuatavyo:



(i) Kukatisha tamaa


Makafiri walitumia mbinu ya kumkatisha tamaa Mtume na waumini wachache aliokuwa pamoja nao kwa kumdhihaki Mtume(s.a.w) na kumuita majina mabaya. Walimuita muongo, mwenda wazimu, mtunga mashairi, mchawi, Abtar (mkatikiwa na

kheri), aliyepagawa na shetani, n.k. Mbinu hii haikusaidia kitu kwani Mtume na waumini walibakia na msimamo wao kwa kuzingatia agizo la Allah(s.w):


“Na subiri juu ya hayo wasemayo (hao makafiri) na uwaepuke mwepuko mwema.” (73:10)



(ii) Kumkataza Mtume kulingania kwa kumtumia Abu-Talib
Wakuu wa Maquraish, walimtaka Abu-Talib, ami yake Mtume(s.a.w) na mlezi wake, amkataze Mtume asiendelee na harakati zake za kuulingania Uislamu. Maquraish walipoona Abu- talib hamkatazi Mtume(s.a.w) walimuendea kwa vitisho na kumtaka achague moja katika matatu-amkataze Mtume kulingania Uislamu au akubali apewe kijana mbadala, ‘Umairah ibn Al-Walid; na wao wamchukue Mtume wamuue au akikataa mapendekezo hayo mawili wamshambulie pamoja na Mtume(s.a.w).Abu- Talib alipofikishwa hapo ilibidi amuendee Mtume(s.a.w) na kumnasihi:



“Ewe Muhammad! Uijutie nafsi yangu na nafsi yako, pia usinitwike mzigo nisiouweza, acha hii kazi yako.” ?



Mtume(s.a.w) alimjibu ami yake kwa majonzi makubwa:

“Ewe mpendwa Ami yangu! Sitaacha kazi hii hata kama wataliweka jua katika mkono wangu wa kulia na wakauweka mwezi katika mkono wangu wa kushoto. Ama Allah atanipa ushindi au nitakufa katika kazi hii.7?


Mbinu hii nayo haikufanikiwa, kwani Abu Talib baada ya kuguswa na yale maneno mazito ya Mtume (s.a.w), aliamua kumuunga mkono na kumuahidi:

“Ewe Mwana wa ndugu yangu, endelea na Dini yako na sema unalotaka. Naapa kwa jina la Allah, sitakutoa kwa maadui na hapana yeyote atakayekudhuru.8”



(iii)Kutaka kumhonga (kumrubuni) Mtume(s.a.w)


Makafiri wa Kiquraish baada ya vitimbi vya mwanzo kufeli walibuni mbinu nyingine ya kumzuilia Mtume(s.a.w) asiendelee na kazi ya kuulingania Uislamu. Safari hii walibuni mbinu ya kumnunua au kumhonga Mtume(s.a.w). Maquraish walimtuma mwanadiplomasia wao, ‘Utbah bin Rabiah, kuwa amrai Muhammad(s.a.w) aache kazi yake ya Utume na apokee malipo yoyote anayotaka ikiwa ni mali, Ufalme au mwanamke mzuri.


‘Utbah alipofika kwa Mtume(s.a.w) alimnasihi:

“Ewe Muhammad! Usiwagawanye watu katika nchi, waache Maquraish waendelee na mila zao na uchukue chochote unachokitaka badala yake. Kama ni fedha (utajiri) chukua kiasi chochote unachokitaka (tutakupa); kama ni mwanamke mzuri; chagua kigori mzuri kuliko wote miongoni mwa waarabu (tutakuoza); kama ni madaraka, basi tuko tayari kukufanya Mfalme – wetu. Chukua unachokitaka katika hivi (hata ukitaka vyote) lakini uache kazi yako hii ya kutangaza Uislamu.” 9?


Mtume(s.a.w) alimjibu ‘Utbah kwa kumsomea aya za Qur-an katika Surat Haamym Sajdah (41) na alipofika kwenye aya ya 37 isemayo:




Na katika alama zake (za Uungu wake Mwenyezi Mungu) ni (huku kupatikana) usiku na mchana na jua na mwezi; basi msilisujudie jua wala mwezi; bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba; ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye (basi fanyeni hivi). (41:37)

‘Utbah alitetemeka na kumuomba Mtume(s.a.w) asiendelee kusoma. Alirejea kwa wakuu wa Maquraish na kutoa ripoti:



“Naapa kwa jina la Allah, haya maneno (ya Muhammad) sio mashairi. Mwacheni na Dini yake. Kama akishinda hiyo itakuwa ni heshima yenu na akishindwa, basi huo utakuwa ndio mwisho wa kazi yake hiyo.”

Lakini Maquraish hawakutaka kusikiliza rai ya ‘Utabah, bali walimcheka na kumdhihaki kuwa amelogwa (amechawiwa). Hivyo, mbinu hii pia haikufanikiwa.



(iv) Kutaka Kumlaghai Mtume(s.a.w)


Walipoona mbinu zote zimefeli, walibuni mbinu nyingine ya kidiplomasia vile vile. Safari hii walikuja na mbinu mbili za ulaghai.



Kwanza, walimuendea Mtume(s.a.w) na kumuomba kuwa waondoe uhasama kati yao kwa kushirikiana katika Ibada. Wafanye makubaliano kuwa mwaka mmoja Mtume(s.a.w) pamoja na wao waabudu masanamu yao na mwaka unaofuatia washiriki pamoja na Mtume(s.a.w) kumuabudu Allah(s.w) pekee. Mtume(s.a.w) aliagizwa na Mola wake kuwa awajibu kwa kuwasomea Suratul-Kaafiruun:




Sema: Enyi makafiri. Siabudu mnachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Wala sitaabudu mnachoabudu.. Wala Nyinyi hamtaabudu ninayemuabudu. Nyinyi mna Dini yenu nami nina Dini yangu (109:1-6)



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 558


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII HUD
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MAISHA YA UTOTONI YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)
MAISHA YA UTOTONI YA MTUME S. Soma Zaidi...

HISTORIA YA WATU WAOVU WAKIOTAJWA KWENYE QURAN
Soma Zaidi...

Historia ya Al-Khidhri
Jina Al-Khidhri halikutajwa mahali popote katika Qur’an. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa Tawala za kifalme baada ya uongozi wa Makhalifa.
Kuanzishwa Ufalme. Soma Zaidi...

Yunus(a.s) Kulingania Uislamu kwa Watu Wake
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

HISTORIANA MAISHA YA MTUME ISA(A.S)
Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na kuanzishwa kwa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Waliomshambulia na kumuuwa Ali, makhawariji na si muawiya
Soma Zaidi...