Kupigwa vita Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki

Kupigwa vita Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki

Kupigwa vita Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki

i. Wamishionari wa kikristo waliona kuwa Uislamu ni kikwazo kwao, waliagiza machifu (viongozi wa kikabila) kuzuia Uislamu kuenea zaidi nje ya miji ya Pwani.
ii. Mkutano wa Berlin mwaka 1884, ulitoa kipaumbelea na fursa ya Ukristo kuwa na nguvu Afrika na kuweka mikakati ya kudhoofisha Uislamu na waislamu.
iii. Vyama vya Wamishionari, kikiwemo cha White Fathers chini ya Kardinali Lavingire, walianzisha mashule, vyuo na makanisa ilikueneza ukristo kupitia mbinu zifuatazo;
a. Kuficha uadui na uhasama wao dhidi ya waislamu na kujenga urafiki wa uongo na kinafiki.
b. Kujikita sana maeneo ya vijijini ndio ambapo waislamu wengi hawajui dini yao.c. Kuanzisha makanisha na huduma za kijamii kama vile; mashule na hospitali.

iv. Wamishionari wa kikristo kupitia serikali za Kijerumani na Kiingereza, walianza mashule zilizotumia mfumo wa silabi zisizokuwa za kiarabu ili kudhoofisha utamaduni wa wenyeji wanaotumia silabi za kiarabu.


v. Wamishionari wa kikristo kutokana na ustawi wa waislamu walioukuta, walimshutumu Gavana Von Soden kuwapendelea waislamu, hivyo ikawekwa sera rasmi ya kuwabagua waislamu kielimu.


vi. Serikali ilinyima kabisa au kutoa misaada kidogo (grant in aid) shule zote za waislamu huku ikielekeza makanisani.
Mfano mwaka 1957 serikali ilitoa paundi 1,338,925 kwa mashirika yanayotoa elimu kati ya hizo, waislamu walipewa paundi 6,848 tu


vii. Masharti magumu au kupigwa marufuku waislamu kuanzisha shule zao katika misikiti (Qur'anic schools) na kutakiwa kuendesha kwa maelekezo ya serikali. viii. Serikali za kikoloni zikishirikiana na wamishionari, zilitaifisha mali zote za
waislamu ikiwemo; mashule, maduka, majumba, mashamba, n.k ili kuwadhoofisha kiuchumi kupitia sare ya ujamaa.


ix. Serikali iliwaua au kuwafunga au kuwahamisha viongozi waislamu makini ili kudhoofisha harakati zao juu ya Uislamu.kama akina Tewa Said Tewa, Suleiman Takadr, Bi Titi Mohamed, n.k.

x. Wamishionari kwa kushirikiana serikali, walianza sera ya dini mseto na taasisi za kimagharibi zinazoshughulikia miradi ya waislamu mfano; mradi wa kuritadisha waislamu wa 'Islam in Africa Project' huko Nairobi.


xi. Serikali za kikoloni kwa kushirikiana na wamishionari na wenyeji wakristo, walitumia nguvu ya kuwateka na kuwaua machifu (viongozi waislamu wa kikabila) kama akina; Bushiri wa Pangani, Mkwawa wa Iringa, Isike wa Unyanyembe, Ali Songea Mbano, Suleiman Mamba, n.k ili kuvunja nguvu ya Uislamu.


xii. Chuki za serikali na mishionari dhidi ya machifu waislamu na waislamu, zilizidi na kuamua kupambana nao kivita kama vile vita vya maji maji, n.k.                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 146


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kuepuka mabishano na madhara ya kugombana
16. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII MUSA NA HARUNA
Soma Zaidi...

Mirathi Katika Uislamu, nani anarithi na ni mambo gani ya kuzingatia kabla ya kirisisha
Soma Zaidi...

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa
Soma Zaidi...

Vita vya Uhud na sababu ya kutokea kwake, Mafunzo ya Vita Vya Uhud
Vita vya Uhudi. Soma Zaidi...

AINA KUU ZA VYAKULA: vyakula vya protini, wanga, fat na mafuta, vitamini, madini na maji
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu
Soma Zaidi...

Njama za Mayahudi Kutaka Kumuua Nabii Isa(a.s)
Njama za kutaka kumuua Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

DUA 41 - 50
41. Soma Zaidi...

Hukumu za talaka na eda
Soma Zaidi...

Baada ya kumzika maiti nini kifanyike kumsaidia marehemu
Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo. Soma Zaidi...