image

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija

Baada ya Mtume(s.

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija

Baada ya Mtume(s.a.w) kupewa amri ya kuutangaza Uislamu kwa wazi, alitumia kila fursa aliyoipata katika kufikisha ujumbe wa Allah(s.w) kwa watu. Alianza na jamaa zake wa karibu, Maquraish, wakasilimu wachache na wengi wao wakawa maadui wakubwa dhidi yake na Uislamu. Pamoja na upinzani mkubwa uliokuwepo, Mtume(s.a.w) na Waislamu hawakukata tamaa bali walijaribu kutumia kila fursa iliyopatikana kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa kila ambaye haujamfikia na kuendelea kuwaasa wale uliowafikia lakini hawajaukubali. Katika kutumia fursa, Mtume(s.a.w) aliamua kutumia msimu wa Hija, kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu wa mbali na Makka.



Tukumbuke kuwa Ibada ya Hija, pamoja na kupotoshwa mafundisho yake, ilikuwa utamaduni wa Waarabu uliodumu tangu wakati wa Nabii Ibrahim(a.s) pale alipoamrishwa:




Na (tukamwambia:) “Utangaze kwa watu habari za Hija, watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyekonda (kwa machofu ya njiani) wakija kutoka katika kila njia ya mbali; (22:27)



Hata hivyo, Maquraish hawakumuachia Mtume(s.a.w) kutumia fursa hii. Wakuu wa Maquraish walikutana “Dar-al- Nadwa” kuweka mikakati ya kuwazuia wageni (mahujaji) kukutana na Mtume(s.a.w). Waliamua kutuma wajumbe wasimame katika kila njia ya kuingilia Makka kuwatahadharisha wageni kuwa:



“Mabwana wa Kiquraysh wametutuma kuwaambia kwamba huko Makka kuna mtu jina lake, Muhammad ambaye amezua Dini mpya ambayo wao hawaikiri kuwa ni Dini; na mtu huyo kapewa ufasaha wa kuzungumza usiokuwa na mfano. Humvuta mtu mara moja kwenye Dini yake kiasi cha kumsikiliza tu. Basi Maquraish wanakuhadharisheni na kumsogelea, licha ya kumsikiliza maneno yake. Akitaka kukusemezeni, mfukuzeni na zibeni masikio yenu. Lau kuwa hayo anayosema yangelikuwa kweli, wao wangelikuwa wa kwanza kumfuata, kwani wao wanamjua zaidi kuliko nyinyi.”14



Kila mahujaji walipokuja Mtume(s.a.w) alichukua fursa ile na kuingia kila hema la kila kabila na kuwalingania Uislamu. Lakini hakupata mapokezi mazuri kutokana na ile ilani iliyotangulizwa na wajumbe wa Maquraish. Kila alipojaribu kuzungumza nao walimpuuza. Kila akisema humzomea, hujifunika nguo usoni na kuziba masikio yao ili wasimuone wala kumsikia ili wasije kutekwa na maneno yake yenye mvuto wa kichawi. Na anapofika mwisho wa mazungumzo yake humuambia:



“Jamaa zako wanakujua zaidi, nao hawakukufuata. Basi hii ni alama kubwa ya kuwa wewe ni mwongo. Wala sisi hatutaacha Dini ya wazee wetu kwa Sababu yako? Abdul-Muttalib mbona hakuwaambia watu kuwa Dini hii (ya wazee) ni uwongo? Ingekuwa kweli Allah anataka kuleta Mtume, angelipewa Walid bin al-Mughira, Bwana wa Maquraish wote au angelipewa Urwa, Bwana wa Banu Thaqif wote. Unafikiri angelikuletea wewe yatima wa Abdul-Muttalib?”15



Pamoja na mikakati hiyo ya makafiri wa Makka ya kuzuia watu wasiingie Dini ya Allah(s.w), palitokea watu ambao hawakutosheka na ile ilani ya Maquraish, bali waliamua kumsikiliza Mtume(s.a.w) na kujionea wenyewe ukweli wa mambo. Katika mwezi wa Rajab, mwaka wa 11 B.U. sawa na Oktoba 620 A.D walikuja kuhiji Makka watu sita (6) kutoka Yathrib (Madinah), katika kabila la Khazraj. Yathrib wakati huo ilikuwa ikikaliwa na Mayahud na makabila mawili ya Waarabu, Aus na Khazraj. Makabila ya Aus na Khazraj yalihasimiana na yalikuwa katika vita baina yao kwa muda mrefu. Kwa bahati nzuri Mtume(s.a.w) alipita Jamaratul-‘Aqabah, katika mji wa Minaa, akakutana na hao watu sita wa Yathrib. Baada ya Mtume(s.a.w) kuwafikishia ujumbe wa Uislamu na baada ya kuwajibu maswali yao waliyomuuliza, wale watu sita walisilimu wote na wakamuahidi Mtume(s.a.w) kuwa watajaribu wawezavyo kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa wenzao wa Yathrib. Walitekeleza ahadi yao na watu wengi wa Yathrib walisilimu.





                   



           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 192


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Darsa za sira (maisha ya mtume jaribio la 01
Soma Zaidi...

Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.
Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah. Soma Zaidi...

Hadhi na haki za Mwanamke Ulaya Wakati wa mapinduzi ya viwnda
Soma Zaidi...

Maadui wa uislamu na mbinu zao: wanafiki, makafiri, mayahudi, wakristo,
Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Madinah. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)
(i) Allah(s. Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 05
Soma Zaidi...

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Katika Mji wa Taif
Baada tu ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Imam Bukhari na Sahihul Bukhari
Soma Zaidi...

Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri
Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a. Soma Zaidi...

MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam). Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na maandalizi haya ya ki ilhamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Je waislamu walishindwa vita vya Uhudi?
Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri? Soma Zaidi...