historia na maisha ya Mtume IS-HAQ(A.S.) NA YA‘AQUUB(A.S.)

Is-haq(a.

historia na maisha ya Mtume IS-HAQ(A.S.) NA YA‘AQUUB(A.S.)

IS-HAQ(A.S.) NA YA‘AQUUB(A.S.)


Is-haq(a.s) ni mtoto wa pili wa Nabii Ibrahiim(a.s), mama yake akiwa Sarah. Habari njema ya kumzaa Is-haq ilimjia Nabii Ibrahim(a.s.) mara tu baada ya kufuzu mtihani wa kumchinja mwanae mkubwa, Ismail(a.s). Alipongezwa kwa kubashiriwa kuzaliwa kwa Is-haq(a.s.):



Amani kwa Ibrahim. Hivi ndivyo tunavyowalipa watendao mema. Bila shaka yeye alikuwa miongoni mwa waja wetu walioamini (kweli kweli).Tena tukambashiria (kumzaa) Is-haq, Nabii miongoni mwa watu wema (kabisa). (37:109-112).



Maelezo ya kuzaliwa Is-haq na hatimaye Ya‘aquub(a.s.) yanapatikana katika kisa cha Malaika waliompa Nabii Ibrahiimu habari za kuangamizwa watu waovu wa Nabii Lut(a.s) na zile za yeye kupata mtoto katika uzee wake.




Na mkewe (Ibrahim - bibi Sarah) alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukampa habari njema ya (kuwa watazaa mtoto wamwite) Is-haq na baada ya I’shaq (watapata mjukuu wamwite) Yaaquub.(11:71)




(Mkewe Ibrahim) akasema: “Ee mimi we! Nitazaa na hali mimi ni mkongwe, na huyu mume wangu ni mzee sana? Hakika hili ni jambo la ajabu.”(11:72)



Wakasema (wale Malaika): Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye anayestahiki kusifiwa na kutukuzwa.” (11:73)



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 3140

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 web hosting    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

tarekh 02

FAMILIA YA MTUME (S.

Soma Zaidi...
Sababu ya uislamu kuwa ndiyo dini sahihi pekee

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Historia ya Vijana wa Pangoni

Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.

Soma Zaidi...
Historia ya vita vya Muta

hii ni historia ya vita vya Muta. Katika makala hii utajifunza sababu ya vita hivi na yaliyojiri katika uwanja wa vita.

Soma Zaidi...
Vita vya badri

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...