picha

Khalifa na Uendeshaji wa Dola kwa ujumla, kulinda wasio waislamu na haki zao na mali zao.

Khalifa na Uendeshaji wa Dola kwa ujumla, kulinda wasio waislamu na haki zao na mali zao.

Khalifa na Uendeshaji wa Dola kwa ujumla



Khalifa ndiye mtendaji mkuu wa Serikali. Kwa hiyo jukumu lake la kwanza lilikuwa kuhakikisha kuwa maelekezo na amri za mamlaka kuu ya uendeshaji zinatekelezwa. Katika kuendesha shughuli za kila siku za Serikali alisaidiwa na shura – ambayo mfano wake katika Serikali za leo ni Baraza la Mawaziri au


Cabinet. Majlisi shura au Tume ya ushauri ilitumiwa na kila Khalifa katika makhalifa wanne wa Mtume(s.a.w). Hakukua na idadi maalumu ya wajumbe wa shura. Wajumbe hawa waliteuliwa na khalifa kwa misingi ya ucha Mungu na mchango wao katika Uislamu na kujitoa muhanga kwao. Miongoni mwao walikuwemo maswahaba maarufu wakiwemo Abubakar, Umar, Uthman, Ali Abdurahman bin Auf, Talha, Zubair, Saad Ibn Waqqas, Abu Ubaidah Ibn Jarrah na Said Ibn Zaid. Viongozi maarufu kutokana Muhajirin na Answar walijumuishwa kwenye shura.


Haki za wasiokuwa Waislamu chini ya uongozi wa Khalifa.


Uislamu una vumilia dini nyingine ingawa ni za kishirikina. Kwa hiyo wasio Waislamu, walitekeleza sheria zao kwa mujibu wa dini zao hasa katika masuala ya urithi, ndoa, talaka, namna ya kupata viongozi wao, uendeshaji wa ibada zao n.k. Kwa kweli walikuwa na uhuru kamili. Vile vile kama wangependa walikuwa na uhuru wa kupeleka kesi zao kwaKadhi(hakimu).Kesi inapopelekwa kwa hakimu haikuruhusiwa kuiondoa mahakamani.


Sheria ya makosa ya jinai, sheria ya ushahidi na mikataba iliwahusu Waislamu na wasio Waislamu. Katika kuwaadhibu wahalifu dhidi ya ubinaadamu kama uzinzi, mauaji, wizi, kupora, n.k. sheria ya Kiislamu ilitumika kwa Waislamu na wasio Waislamu.


Kama mzozo ulizuka baina ya Muislamu na asiye Muislamu kesi ya namna hii ilipelekwa mahakamani na utaratibu ulikuwa kama ifuatavyo: Katika masuala ya ubinaadamu asiye Muislamu alihukumiwa sawa na Muislamu. Kwa mfano kama asiye Muislamu amemuua Muislamu adhabu atayopewa ni sawa na ile, kama kosa lile lingefanywa na Muislamu.


Tukio la kihistoria lifuatalo linaonesha haki ilivyo katika Uislamu hata kama asiye Muislamu alimkosea Khalifa.


Wakati Khalifa Ali alipokuwa anaondoka kwenda katika vita vya Siffin - alipoteza zirah yake. Aliporudi toka vitani alimuona Myahudi mmoja na zirah yake. Khalifa alimuuliza yule Myahudi aliipataje ile zirah wakati ni yake na hajampa mtu wala hajaiuza. Yule Myahudi alijibu kijeuri: “Kwa kuwa ninayo mimi basi kiasili ni mali yangu”. Khalifa pamoja na kuwa ndiye mkuu wa Serikali hakuwa na jinsi isipokuwa kulikepeleka suala hili mahakamani. Kadhi Shurayb alimuuliza Khalifa aliyekuwa pamoja naye sababu ya kuwepo kwake pale mahakamani. Ndipo Khalifa akaeleza: “zirah aliyonayo huyu Myahudi ni yangu kwa vile sijampa mtu yeyote na sijaiuza”.


Yule Myahudi alipotakiwa kujieleza alieleza kuwa kwa kuwa zirah iko mkononi mwake basi ni mali yake. Hapo ndipo hakimu alipomtaka Khalifa atoe ushahidi, lakini alipotaka kuwaleta mwanae Hassan na mfanyakazi wake Qanbar kama mashahidi hakimu hakukubali ushahidi wao kutokana na uhusiano wao na Khalifa. Kwa hali hii Myahudi alishinda kesi na akaachiwa aende na ile zirah. Myahudi huyu alishangazwa na hali hii ya Khalifa kusimama mahakamani na raia wake tena wa dini nyingine na hata hivyo akashindwa kesi na akaridhika. Hali hii ilimfanya akiri kuwa ile zirah ni ya Khalifa akamrudishia na yeye akasilimu”.34




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1169

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Msonge wa uongozi na siasa katika serikali ya kiislamu mafinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
tarekh 07

KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na mkataba wa aqabah katika kuandaa ummah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtume kumuoa bi khadija

Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija.

Soma Zaidi...
Kibri cha Ibilis na Uadui Wake Dhidi ya Binadamu

Ibilis ni katika jamii ya majini aliyekuwa pamoja na Malaika wakati amri ya kumsujudia Adam inatolewa.

Soma Zaidi...