7.
7.3Mtume (s.a.w) Kuulingania Uislamu Makkah kwa siri.
- Mtume (s.a.w) alianza kulingania familia yake, kisha rafiki zake na jamaa zake wa karibu walio rafiki.
- Mtume (s.a.w) alianza kulingania Uislamu kwa siri kwa muda wa miaka mitatu kwa kukutana na waislamu waliosilimu mwanzo kabisa katika nyumba ya bwana Arqam bin Arqam β maarufu kama Darul-Arqam.
Mtume (s.a.w) kuutangaza Uislamu Makkah kwa jamii nzima.
- Baada ya miaka mitatu ya kuulingania Uislamu kwa siri, aliamrishwa kuutangaza sasa hadharani kwa jamii yote inayomzunguka.
- Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kuutangaza ujumbe wa Uislamu hadharani, alikumbana na Upinzani dhidi ya ujumbe wake huo kutoka kwa Makafiri wa Kiqureish wa Makkah.
Sababu za Makafiri wa Kiqureish kuupinga ujumbe wa Uislamu.
i.Walihofia kupinduliwa mfumo wao wa utawala kandamizi na kusimama mfumo wa Uislamu unao simamia haki na uadilifu.
ii.Walihofia kupoteza maslahi yao kupitia njia kandamizi, nyonyaji na haramu katika jamii zao.
iii.Walihofia kukosa wafuasi ambao ndio ilikuwa rasilimali pekee katika kuendeleza na kuimarisha unyonyaji wao.
iv.Walihofia kupoteza nafasi yao katika kuiongoza jamii kama fursa pekee ya kunyonya, kudhulumu na kulinda maslahi yao.
v.Walihofia kupoteza umaarufu na nafasi ya ibada (itikadi) zao za kishirikina ambazo ndizo nyenzo pekee za mapato yao.
Umeionaje Makala hii.. ?
Tukirejea Qurβan (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7
Soma Zaidi...Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma.
Soma Zaidi...Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri?
Soma Zaidi...