image

Mateso waliyoyapata waislamu wa mwanzo Maka, na orodha ya waislamu walioteswa vikali

Pili, Maquraish walimuendea Mtume(s.

Mateso waliyoyapata waislamu wa mwanzo Maka, na orodha ya waislamu walioteswa vikali

Mateso waliyoyapata waislamu wa mwanzo Maka, na orodha ya waislamu walioteswa vikali

Pili, Maquraish walimuendea Mtume(s.a.w) na kumpa masharti kuwa kama anataka Maquraish wasilimu, alete ujumbe mwingine usiwe ule wa Qur-an anaowasomea au abadilishe aya za Qur-an zilandane na matashi yao. Mtume(s.a.w) aliwakatalia ombi hili kwa kuwasomea Qur-an:



Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiogopa kukutana nasi husema: “Lete Qur-an isiyokuwa hii (ambayo haitatukataza haya tunayoyapenda), au ibadilishe (kidogo hii).” Sema “Siwezi kuibadilisha kwa khiari ya nafsi yangu; sifuati ila yanayofunuliwa kwangu (ninayoletewa Wahyi). Hakika mimi naogopa-nikimuasi Mola wangu, - adhabu ya siku (hiyo) iliyo kuu.” (10:15)



(v) Kuwatesa na Kuwaua Waislamu


Maquraish walipoona wameshindwa kuzima Uislamu usiendelee kwa kutumia diplomasia, waliamua kutumia mbinu ya mabavu ya kuwapiga waumini, kuwatesa mateso ya kila namna, kuwatenga kijamii na kuwaua baadhi yao. Hebu turejee historia tuone mifano michache ya mateso kwa ajili ya Uislamu waliyopata Maswahaba na Mtume mwenyewe.




Mtume(s.a.w) mwenyewe


Mtume mwenyewe alifanyiwa kila aina ya mateso. Pamoja na kutukanwa na kuitwa muongo, mwendawazimu, mchawi, mkiwa na kuzomewa mitaani, alipigwa mawe (rejea safari yake ya Taif), Abu Jahl (adui yake mkubwa) alimbandika shingoni mwake kinyesi cha ngamia wakati alipokuwa katika sijida (katika swala), Utbah bin Abi Mu’it alimniga Mtume shingo na shuka iliyosokotwa, n.k.



Abu Bakar(r.a)
Mara tu Mtume(s.a.w) alipodhihirisha utume wake hadharani, Abu Bakar alikwenda kwenye Ka’bah akatoa khutuba juu ya Uislamu. Watu wote waliokuwa pale walimvamia na kuanza kumpiga. Baada ya kuanguka chini, ‘Utbah bin Rabi’ah alimpiga kwa viatu mpaka akazirai. Hakupata fahamu mpaka jamaa zake wakampeleka nyumbani kwake, na alikaa kitandani kwa masiku kutokana na kipigo. Mtume(s.a.w) alipokuwa kwenye Ka’bah, Abu Jahl alikuja na kumtia shingoni kamba ya nguo iliyosokotwa. Aliinyonga ile kamba na kuikaza ili kumniga Mtume mpaka afe. Abu Bakar(r.a) alipoona kitendo kile anafanyiwa Mtume alienda mara moja kumuokoa kwa kumsukumiza Abu Jahal pembeni na kuitoa ile kamba shingoni mwa Mtume, kisha akasema: “Unataka kumuua mtu mzuri kama huyu ambaye ni Mtume wa Allah anayemtangaza Allah kwa sifa zake tukufu? Kisha Abu Jahl na maadui wengine wa Uislamu walimgeuekia Abu Bakar na kumpiga kikatili.



Bilal(r.a)

Bilal alikuwa Muhabeshia na mtumwa wa Umayyah bin Khalaf, adui mkubwa wa Uislamu. Umayyah alikuwa akimpiga sana Bilal kisha alikuwa akimfunga kamba za mikononi, miguuni na shingoni kisha kuwaambia watoto wamburure njiani. Mara nyingine alikuwa akimshindisha na kumlaza njaa, kisha siku ya pili yake alikuwa akimtoa nje na kumlaza chali uchi katika jua kali juu ya mchanga wa moto na kumuwekea jiwe kubwa la moto juu ya kifua chake na kumwambia, “Utasalia vivi hivi mpaka ufe au uache Dini ya Muhammad”. Bilal alikuwa akisema, “Ahad”, “Ahad” – yaani Naabudu Mungu mmoja tu. Alitaabishwa hivyo hivyo mpaka Abu Bakar alipomkomboa. Abu Bakar aliwakomboa watumwa wengi waliokuwa wakiteswa kwa ajili ya Uislamu wao.



Abu-Fukayha(r.a)
Alikuwa akitaabishwa na kuteswa na mtoto wa Umayyah kwa namna ile ile alivyokuwa akitaabishwa Bilal(r.a).



Bibi Anira(r.a)
Abu Jahl alikuwa akikiunguza chuma motoni kisha akimgandamiza nacho machoni mpaka akapofuka.



Khabbab(r.a)
Alikuwa mtumwa wa mwanamke katili kweli kweli, alikuwa akinyolewa nywele kisha akichomwa kwa bapa la chuma chenye moto juu ya kichwa. Akawa na madonda mengi kichwani.




Ammar bin Yasir(r.a)
Baba yake na ndugu yake walikuwa wakipigwa kwa majani ya mitende kila siku mpaka wakajaa madonda mwili mzima. Baba yake na ndugu yake waliuliwa katika mateso hayo na akabakia Ammar.



Mama yake Ammar(r.a)
Pamoja na mateso mengi aliuliwa kikatili mno. Alichomwa mkuki tumboni.



Amir bin Fuhayra(r.a)
Aliadhibiwa kikatili mno mpaka akarukwa na akili.



Bibi Lubayna(r.a)
Alikuwa akiadhibiwa kwa ukatili mno na ‘Umar bin Khattab kabla hajasilimu. ‘Umar alikuwa akimchapa bakora mpaka achoke.



(vi)Kuwasusia Waislamu na Banu Hashim
Ni katika kipindi hiki cha mateso, Mtume(s.a.w) aliwashauri waumini hasa wale wanyonge waliokuwa wakipata mateso makubwa zaidi, kuwa wa hajiri kwenda Uhabeshi (Ethiopia) ili kusalimisha maisha yao kwa Mfalme muadilifu, Najash. Najash alikuwa Ahlal-Kitaab (Mkristo) na baadaye alisilimu.



Maquraish walipong’amua kuwa baadhi ya Waislamu wamehamia Uhabeshi na Mfalme anawapokea, walifanya jitihada za kuwarudisha lakini ilishindikana. Hii iliwapandisha hasira zaidi na kuamua kuzidisha mateso kwa Mtume na Waislamu waliobakia Makka. Katika kuzidisha mateso, Maqurash waliamua kuwasusia Waislamu na watu wa ukoo wa Mtume (Banu, Hashim na Banu Muttalib) kiuchumi na kijamii. Banu Hashimu na Banu Muttalib walichanganywa na Waislamu kwa kuwa walipinga rai ya kuuliwa ndugu yao, Muhammad(s.a.w). Mkataba wa kuwasusia Waislamu na ukoo wa Mtume(s.a.w) uliwakataza Maquraish kufanya yafuatayo:


(1) Kusema na Banu Hashimu yeyote wala banu Muttalib akiwa
Muislamu au si Muislamu.

(2) Kuwauzia chochote wala kununua kitu kwao.

(3) Kuoana nao.


(4) Kuwasaidia kwa njia yoyote ile.

(5) Kukaa pamoja nao.





Baada ya mkataba huu kupitishwa, ilibidi Waislamu, Banu Hashim na Banu Muttalib watoke Makka na kuhamia kwenye bonde moja lililokuja julikana kwa jina la Shi’b Abu Talib (Makazi ya Abu Talib). Waislamu na watu wa ukoo wa Mtume(s.a.w) walikaa pale bondeni kwa dhiki kubwa ya chakula kiasi cha watu kula majani na ngozi, kwa muda wa miaka mitatu baada ya mkataba kuvunjwa na baadhi ya Maquraish kwa misingi ya ubinaadamu. Baadhi yao waliona si sahihi kuwatesa watu kiasi kile kwa sababu tu ya itiqadi yao.

Pamoja na mateso haya, Mtume(s.a.w) na wale waliomuamini walibakia na msimamo wa Dini yao pasina kutetereka hata chembe. Ni katika mazingira haya Allah(s.w) anatunabahisha:




Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, na hali hamjajiwa na mfano wa (yale yaliyowajia) wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara na wakatetemeshwa sana hata Mitume na walioamini pamoja nao wakasema: “Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini?” Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu. (2:214)



(vii)Kuazimia Kumuua Mtume(s.a.w)
Mtume(s.a.w) baada ya mikataba ya

‘Aqabah, aliwaamuru Waislamu wahamie Yathrib (Madinah). Maquraish waling’amua kuhama kwa Waislamu na walimtarajia Mtume(s.a.w) naye kuhama. Wakuu wa Maquraish waliona kuwa wakimuachia Mtume(s.a.w) kuhamia Madinah, Uislamu utapata nguvu na itakuwa ni hatari kwa maslahi yao ya kiitiqadi, kisiasa na kiuchumi. Hivyo wakuu wa Maquraish walikutana “Dar-al-Nadwa” na kupitisha uamuzi wa kumuua Mtume(s.a.w) kama Qur-an inavyotukumbusha:



Na (kumbuka Ee Nabii Muhammad) walipokufanyia hila wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe (kwa hali mbaya katika Makka)“(8:30)

Mbinu hii nayo ilifeli pale Allah(s.w) alipomnusuru Mtume wake, alipokuwa na sahibu yake, Abubakar, katika pango la Jabal

Thaur, kituo cha mwanzo cha safari yao ya kuhajiri kwenda
Madinah.




Kama hamtamnusuru (Mtume), basi Mwenyezi Mungu alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru; alipokuwa (mmoja tu na mwenziwe) wa pili wake, (peke yao) walipokuwa wote wawili katika pango; (Mtume) alipomwambia sahibu yake; “Usihuzunike, kwa yakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.” Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona, na akafanya neno la wale waliokufuru kuwa chini; na neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeshinda na ndiye Mwenye hikima. (9:40)




Mafunzo:
Kutokana na upinzani dhidi ya ujumbe wa Mtume(s.a.w) katika kipindi cha Makka, tunajifunza yafuatayo:

Kwanza, hatunabudi kukumbuka kuwa upinzani dhidi ya Uislamu haukutokea tu wakati wa Mtume(s.a.w) bali hii ni katika Sunnah ya Allah(s.w), kuwa amejaalia Uislamu uwe na upinzani katika zama zote.


Na namna hii tumemfanyia kila Nabii maadui; (nao ni) mashetani katika watu na (mashetani katika) majini. Baadhi yao wanawafunulia wenziwao maneno ya kupambapamba ili kuwadanganya. Na kama Mola wako angalipenda wasingalifanya hayo, (angewalazimisha kwa nguvu kutii). Basi waache na uwongo wao. (6:112)



Hivyo, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuwa tayari kupambana na wapinzani wa Dini ya Allah(s.w).



Pili, mbinu walizozitumia Makafiri wa Kiquraysh, katika kutaka kuuhilikisha Uislamu, zinafanana mno na hizi wanazozitumia makafiri wa leo.



Tatu, siri ya mafanikio ya Mtume(s.a.w) na Maswahaba zake, ya kubakia katika Uislamu, kuulingania na hatimaye kuusimamisha kule Madinah pamoja na upinzani mkubwa kiasi hicho, ni kule kufuatilia kwao kwa makini mafundisho ya awali waliyopewa katika A’laq (96:1-6), Muzzammil (73:1-10) na Muddaththir (74:1-7).



Nne, wakati wowote Waislamu watakapojitahidi kulingania na kusimamisha Uislamu kwa kadiri ya uwezo wao wa mali na nafsi, pamoja na upinzani mkubwa dhidi yao, nusura ya Allah(s.w) itakuwa pamoja nao alimradi tu wamtii Allah(s.w.) na Mtume wake ipasavyo. Ahadi ya Allah(s.w) iko wazi



Wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu (ya Uislamu) kwa vinywa vyao; na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukiwa. (61:8)



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1435


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Hatua mbili kuu za kushuka kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s. Soma Zaidi...

Wapinzani wa Ujumbe wa Hud(a.s)
Waliomuamini Mtume Hud(a. Soma Zaidi...

Chanzo cha Mapato katika serekali ya Kiislamu wakati wa Makhalifa
Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Isa(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)
Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a. Soma Zaidi...

Vipengele vya Mikataba ya ‘Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina
Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A. Soma Zaidi...

Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi. Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...

Waliomuamini Nabii Nuhu(a.s)
Waliomuamini Nuhu(a. Soma Zaidi...

Bara la Arabu Zama za Jahiliyyah
Wakati Mtume(s. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUNUS
Soma Zaidi...