image

USALITI (sehemu ya pili)

Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara.

USALITI ( sehemu ya pili)

Basi Moses alifunga ndoa na msichana mmoja aloyekutana naye huko Arusha katika maisha yake alikuwa msichana wa pili kuingia naye kwenye mapenzi kwa sababu mda mwingi alikuwa na Rhoda, basi ndoa ilifungwa kanisani na pia wakaanza kuishi pamoja na mke wake mpya, ila kwa sababu Moses alikuwa na tabia ya kuongea na Rhoda kila siku alibadilisha mda wa kuongea na Rhoda kwa sababu ya kuogopa mke wake kwa hiyo alikuwa anaongea naye mwisho saa tatu jioni akidai kwamba anachoka anapaswa kulala mapema, kwa hiyo kila siku saa mbili na nusu alitafuta mda na kuongea na Rhoda akidai kwamba anaenda kulala mapema na baadae Rhoda alidhani ni ukweli na akazoea kumtafuta mda huo.

 

Kwa kuwa hakuna Siri chini ya jua Kuna mtu mmoja alikuwa ameshakutana na akina Rhoda na Moses alikuwa anafanya kazi Arusha aliona Moses anafunga ndoa na alipokutana na Rhoda  siku Moja alimuuliza kuhusu Moses huyu akamjibu kwamba yuko Arusha na wanategemea kuoana Mungu akijalia, huyu akashutuka sana na kusema kwamba mbona Moses kaoa mda, Rhoda aliumia sana akafunga safari kwenda Arusha mpaka sehemu anapofanya kazi Moses na kuonana na boss wa Moses na kumuuliza kama Moses ameona na ikaonekana kaoa kweli, yule dada Rhoda tangia mda huo akachanganyikiwa akawa anatembea ovyo ovyo mjini Arusha na akaanza kuishi kwenye dampo yaani kwa ujumla akawa mwehu.

 

Kadri ya siku zilivyoenda pale singida hawakumwona Rhoda kwenye sehemu yake ya kazi pia na pale alipokuwa anaishi hawakumwona hali iliyomfanya kuwataarifu wazazi wake walikuwa mkoa wa Mwanza na walimtafuta mwaka mzima na hawakufanikiwa, basi kwa sababu baba yake na Rhoda alikuwa na pesa nyingi watu wakaanza kusema kwamba amemtoa Binti yake kafara hali ambayo ilimfanya baba kuishiwa na Amani na hata uchumi wake ulianza kushuka kwa sababu ya mawazo ya mtoto na maneno ya watu kwa sababu na ndugu walianza kuwatenga wakidhani kwamba mtoto katolewa kafara kumbe hapana alikuwa amepotea tu,

 

Siku Moja mdogo wake na Rhoda alikuwa anasafili kuelekea Arusha kwa ajili ya kikazi , basi gari lilisimama wakashuka na kuanza kula hotelini akaja Binti mwehu akiwa na matope na haeleweki , kuangalia kwa makini akaona ni dada yake yule kijana akalia kwa sauti kubwa na watu walishangaa sana na kumuuliza amekuwaje ndipo akawasimulia kuhusu dada yake aliyepote ni kama mwaka mmoja na nusu sasa hivi na akasema ni huyu ila Rhoda alikuwa Hana mda na yeye ila alikuwa anaomba omba chakula kwa watu, kwa sababu watu wa pale walimfahamu yule mwehu Rhoda wakamwita taratibu na mdogo wake akampa chakula akala hata hakumtambua mtu yeyote alipomaliza kula akaondoka yule mdogo wake akamfuata wakamwambia muache kwa sababu hatoki mazingira haya .

 

Mdogo wa Rhoda akapiga simu nyumbani na kumwambia kwamba Rhoda kapatikana na mazingira aliyomo , kwa hiyo safari ya mdogo wa Rhoda iliishia hapo akaanza taratibu za kumtafuta kumpatia dada yaka na baba yao akiwa njiani kutoka mwanza kuelekea Arusha, kwa kuwa yule Mzee kiuchumi alikuwa vizuri mda kidogo tu alikuwa ameshuka kwa ndege, basi baba alipofika alimwona mwanae alilia sana na baadae akamshukuru  Mungu kwa kumwona tena mtoto wake, basi baba mtu akakodi chumba akanunua chakula akamwita akamfuata alikuwa hamfuati kwa kuwa ni baba yake Bali kwa sababu ya chakula kwa sababu alikuwa hatambui mtu yeyote,

 

Hatimaye aliwafuata na wakafanikiwa kumfungia ndani ingawa alikuwa anapiga kelele sana akiita Moses, kwa sababu ya zile kelele watu kwenye hotel wakaanza kulalamika ndipo baba yake akachukua dawa ya usingizi akamwekea kwenye chakula akala na akasinzia wakachemsha maji wakampangusa pangusa akiwa amelala fofofo wakamvalisha nguo nzuri wakamfunga na wakakodi gari kuanzia Arusha mpaka Mwanza kwa wazazi wake, wakiwa njiani akaamka akaanza kupiga kelele tena ila hawakujali walimsafitisha hatimaye akafika  nyumbani,alipofika nyumbani aliweza kuita mama ila alipoona jinsia ya kiume alipiga kelele nyingi na kuanza kuwafukuza Ili watoke ndani ila hatimaye alifungiwa ndani kwenye chumba chake kwa sababu vituko viliongezeka kila siku.

 

Kwa hiyo baba yake akaanza kuwatafuta madaktari na kuja kumpima hawakuona kitu chochote isipokuwa minyoo, typhoid na magonjwa mengine ya Kawaida kwa sababu ya mazingira alivyokuwa anaishi na walifanya matibabu na akapona kabisa magonjwa hayo ila kwa upande wa magonjwa ya akili hali ilibaki Ile Ile, kwa hiyo wakaamua kuwaleta madaktari wa magonjwa ya akili ila Kazi ilikuwa Bure Binti hakutulia hata kidogo alikuwa anapiga makelele kila siku na kufukuza watu na kuwapiga kwa mawe au kitu kingine chochote kile hali hii iliwafanya watu waache kutembelea familia Ile na walimlalamikia baba wa familia kwamba kamtoa mtoto kafara hali iliyomfanya familia Ile kukosa amani.

 

Kama kawaida hali ikiwa ngumu ya maisha mwanadamu ujaribu njia nyingine Ili kuangalia kama atapata msaada, kwa sababu yule baba alikuwa mcha Mungu alimpeleka Binti kwenye maombi mbalimbali ndani na nje ya nchi hata kukanyaga mafuta ila hali ilibaki kuwa Ile Ile na akaamua kumpeleka kwa waganga wa kienyeji na mganga alikuwa wa kiume huyo alimpiga viboko na mganga akakimbia mgonjwa kwa sababu ya kile kipigo , baba akakata tamaa akaamua kumrudisha nyumbani kwa sababu kila kitu kilikwama na maisha yakaendelea kuwa magumu kwa sababu hawana furaha na watu wamewatenga ingawa hali ya kiuchumi ilikuwa nzuri

 

Siku Moja baba alikuwa anasoma kitabu cha mwana saikolojia mmoja jinsi anavyosaidiwa watu hasa walioadhirika na magonjwa ya akili na number yake ilikuwepo pale kwenye kitabu, akaamua kupiga na kumwambia hali ya Binti yake na yule baba akaja akaongea na yule Binti kwa siku ya kwanza ila binti hakuwa na ushirikiano kwa sababu alikuwa hapendi kumwona yule mwanaume kwa sababu yeye wanaume wote aliwalinganisha kama Moses basi siku nyingine yule baba alikuja na Binti amevaa nguo kama alivyokuwa anampenda kuvaa, yule Rhoda alifurahi sana na akamkumbatia yule dada akampeleka kwenye chumba chake alimokuwa anaishi ingawa kilikuwa na harufu mbaya Ila kwa kuwa ni kazi yake alivumilia tu.

 

Kwa hiyo mahojiano yalianza na Rhoda akawapa ushirikiano na kusema kila kitu kilichokuwemo moyoni mwake na wakafahamu chanzo ni nini?  Basi wakamhakikishia kwamba atapona ila shida ni kwamba hakuwa tayari kumsamehee Moses, kwa kuwa alikuwa muumini wa kanisa katoliki walimwambia atubu kwanza kwa sababu ya mimba alizotoa na matibabu ya kisaikolojia yataendelea mbele kwa hiyo wakaanza kumfundisha namna ya kutubu kwa sababu kila kitu kilishapotea kwenye akili yake akaja padre akaungama ila shida ni kwamba alikuwa hapendi kumsamehee Moses yaani matibabu ya kisaikolojia yalitumia miaka mitatu ila kikwazo kikubwa ni kukataa kusamehe.

 

Baada ya msombi makali na kufunga Rhoda alikubali kumsamehee Moses hapo matibabu ya kisaikolojia yataendelea Ili kuweza kumrudisha kwenye hali ya Kawaida, kwa hiyo siku Moja wakampeleka beach huku amefungwa wakampigia simu Moses na kumuuliza alikuwa anampenda kumwita majina gani Moses akawaambia, kwamba alikuwa akimwita Roho yangu,baby na R, Badi palikuwemo na kaka akaja akamshika mkono akamwita majina hayo akamnongoneza sikioni na kumwambia hakuna mwanamke mzuri kama wewe duniani yule dada alilia masaa mataono mfululzo bila kunyamaza,

Itaendelea           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023/02/06/Monday - 05:29:59 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 916


Download our Apps
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara. Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku Soma Zaidi...

Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake. Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha. Soma Zaidi...

Hadithi katika kijiji cha burugo
Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii . Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI (sehemu ya sita)
Post inahusu zaidi hadithi ya NIMLAUMU NANI ambayo ni sehemu ya sita, katika kipengele hiki tunaenda kumwona msichana Amina anapambana na hatimaye anafunga ndoa ya kiserikali na Frank Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita
Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya. Soma Zaidi...

Hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi habari za Mama mmoja aliyekuwa mchoyo akampa mkate mwehu na kuutia Sumu ila kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu sana aliutunza mkate na kuwapatia watoto wa yule mama waliokuwa wakitoka shule na njaa kali Soma Zaidi...

Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme (sehemu ya nne)
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya. Soma Zaidi...