Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini.
Mtoto wa Tajiri na maskini .
1.watoto hawa walikuwa majirani, na walikuwa wanasoma shule moja , kila siku mtoto wa tajiri alikuwa anaamshwa anaoshwa, anasaidiwa kupiga mswaki anavalishwa anaangaliwa cha na baadae anawekwa kwenye gari mpaka shuleni na kufungiwa juice na maanda kwenye begi kwa ajili ya kula baadae , na mda wa saa nne alikuwa anafuatwa shule anaenda kunywa maziwa nyumbani na kurudishwa kuendelea na masomo na baada ya kumaliza masomo mtoto alifuatwa kwa gari mpaka nyumbani baada ya kufika nyumbani alibadilisha nguo akala chakula alichokuwa ameagizwa kupokwe mara nyingi zilikuwa ni Chipsi.
2. Baada ya kumaliza kula aliwekewa tv akaanza kuangalia katuni na michezo mingine na alipokuwa anachoka anaenda kuogelea kwenye swimming pool na baadaye alikula kila alichopenda kula na baadae alikwenda kulala hata bila kukumbushwa kufanya home work hiyo ndiyo iliyokuwa ratiba ya mtoto wa tajiri.
3. Kama nilivyotangulia kusema kwamba palikuwepo pia mtoto wa maskini, yeye ratiba yake ilikuwa tofauti kabisa na mtoto wa tajiri yeye kila siku alijiamsha mwenyewe akanawa uso akajipaka sabini kwa sababu mafuta yalikuwa shida ,akasafisha nyumba kwa kufagia huku akisubiria chai aliyoweka kwenye mafiga akimaliza kufagia anakunywa chai bila sukari pamoja na kiporo kidogo cha ugali kilichobaki na akikumbuka kumbakizia mdogo wake ambaye bado amelala na akimaliza anaosha vyombo anavaa uniform na kuacha amekunja shuka lake maana alikuwa na Moja la kulalia Kisha anawaaga wazazi anakimbia shuleni kugonga kengere kwa sababu alikuwa time keeper .
4. Akifika shuleni anawasimamia darasa la kwanza na la pili kwa sababu yeye na mtoto wa tajiri waliokuwa darasa la tano, na baadae anaingia darasani na kuanza kusoma na alikuwa anabaki shuleni mpaka saaa na zikifika saa nane anaenda nyumbani akifika nyumbani ana Kuta wazazi wake bado wako shamba anabadilisha nguo anachukua ndoo anaenda kisomani kuchota maji anayaleta anachemsha maji na kusonga ugali na kupika mboga kwa ajili ya kulisha ugali, akimaliza anakula anawabakizia wazazi wake ila yeye anakula na ndugu yake akimaliza kabla ya jua kuisha anafanya homework mapema na kujisomea kidogo kabla ya giza kuingia kwa sababu hawakuwa na umeme.
5, giza likiingia tu anawaosha ndugu zake na yeye anaoga na akimaliza asaidiana kuandaa chakula cha jion na Mama yake na baadae wanawasha tochi wanaenda kula na kulaa na hayo ndiyo maisha na ratiba ya mtoto wa maskini.
Itaendelea.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, baada ya kijana wa kiume wa binti mfalme kuoa yule ndugu yake baba anafanya sherehe kubwa na wake wenza wamepata habari kwamba kijana wa kiume wa mfalme ameoa ndugu yake wakaamuru kunyamaza il
Soma Zaidi...NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku
Soma Zaidi...Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambao walipoteana katika hali za kukimbizwa na wazazi Ili waweze kutimiza ndoto zao na siku wakakutana wakiwa watu wazima.
Soma Zaidi...Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki.
Soma Zaidi...Mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya.
Soma Zaidi...Hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi habari za Mama mmoja aliyekuwa mchoyo akampa mkate mwehu na kuutia Sumu ila kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu sana aliutunza mkate na kuwapatia watoto wa yule mama waliokuwa wakitoka shule na njaa kali
Soma Zaidi...