Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo
USALITI.
kama tulivyotangulia kusema kwamba hadithi hii ni ya usaliti ila ni hadithi ya kweli kabisa ambayo imetokea miaka kama kumi hivi imepita, ni msichana aliyejulikana kwa jina la Rhoda na mvulana akijulikana kwa jina la Moses, Moses alikuwa kidato cha tatu kwenye shule moja ambayo nitaifadhi jina lake na palikuwepo na msichana mfupi mwembamba kidogo,mweupe , mwenye dimpozi na mwanya kwa ujumla yule Binti alikuwa mzuri kweli yaani kwa sura na kitabia pia kwa sababu ya uzuri wake alikuwa kawaida sana akisalimiana na kishirikiana na kila mmoja.
vile vile yule Binti alikuwa anajikaza kusoma ila alisumbuliwa sana na Vijana wengi ila kwa kuwa alikuwa mcha Mungu aliweza kukaa imara na kuendelea na masomo yake vizuri, ila pale shuleni wakati wa uchaguzi wa viongozi walimchagua Moses kama head boy wa shule kwa hiyo kauli yake ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi aliyeko pale shuleni anafikisha wastani wa hamsini na katika Kipindi chote cha uongozi wake wanafunzi walio wengi waliweza kufanikiwa kwenye masomo yao , kwa hiyo walichagua wanafunzi wale wanaofaulu Vizuri Ili kuweza kusimamia wanafunzi wengine kwa hiyo na Rhoda kwa kuwa alikuwa mwanafunzi Bora darasani alichaguliwa kusimamia kidato cha kwanza kama academic.
Basi katika kila kikao cha shule Rhoda hakukosa na alisimamia wanafunzi wenzake na kuwapa mbinu mpya za kusoma, kwa hiyo katika kwenda kwenye vikao Moses alitokea kumpenda Rhoda ila aliogopa ataanzaje kwa sababu yule alikuwa ni msichana mwenye misimamo yake, kwa sababu ya kazi nzuri waliyoifanya viongozi mkuu waa shule aliamua kuwapeleka beach Ili waweze kuogelea na kifurahi kwa hiyo ndiyo nafasi aliyoiona Moses kuweza kumwambia Rhoda yaliyomo moyoni mwake.
Basi Moses alimchagua Rhoda amsaidie kusimamia vinywaji na vyakula na kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaopaswa kwenda beach wanakwenda kwa wakati basi Moses na Rhoda walisimamia kazi hiyo vizuri kabisa na walipofika beach wanafunzi waliwekewa mziki wakacheza ila Moses na Rhoda walikuwa busy kuandaa chakula na maandalizi yote kwa ujumla, Badi walipoweka sawa kila kitu walianza kutembea ufukweni mwa bahari na Moses akaanza kumwambia yaliyomo moyoni mwake ila Rhoda alimwambia kaka nipe mda .
Kwa hiyo wakiendelea na shughuli nyingine nyingi na baadae wakala na wakaenda makwao kila mtu ila Moses alkaa anawaza yule Binti ila Rhoda kwa kuwa alikuwa amewazoe wavulana wengi wanamsumbua ila hajali anawapa majibu ya Kawaida na wanaondoka Wala hakufikilia chochote kuhusu Moses , basi jumatatu walirudi shule wakati wa mapumziko mosea alikuja kwa Roda na kumkumbushia ujumbe wake ila Rhoda alikuwa hata hakumbuki kitu ambacho kilimfanya Moses kukasilika na baadae kengere iligongwa wakarudi darasani.
Siku zilenda ila Rhoda alikuwa hatoi jibu hali iliyomfanya Moses kukasilika zaidi, basi kwa sababu Moses alikuwa anafahamu sana hesabu ilitokea mda pakawepo mashindano ya hesabu kutoka shule mbalimbali na wanafunzi kumi Bora walihaidiwa kupelekea nje kwa ajili ya kutembea kwa mwezi mmoja, Badi siku ya mtihani ikafika Moses akaingia kwenye chumba cha mtihani na wanafunzi wengine kutoka shule mbalimbali,ila shule ya akina Moses na Rhoda wanafunzi walikimbia kwa sababu ya kuogopa hesabu, basi walimu wakaangaika kutafuta wanafunzi ila kila mmoja alikataa kwenda, basi mtihani ukasimamishwa mpaka wanafunzi wafike, Basi waalimu wakampendekeza Rhoda aende na wakamwambia Moses awe anamsaidia.
Kwa kuwa Rhoda ni mwanafunzi ambaye hakuwa na makuu aliweza kwenda kwenye chumba cha mtihani na akakaa karibu na Moses,ingawa Moses alikuwa mchoyo lakini alipomuona Rhoda tu aliomba mtihani wake kisiri akafanya maswali yote vizuri yake ya Rhoda na baadae akaanza kufanya ya kwake ya Rhoda aliyemaliza mapema kwa sababu yalikuwa ya kidato cha kwanza na baadae akaendelea na maswali yake ya kidato cha tatu kwa sababu Moses alikuwa fundi wa hesabu alimaliza kabla ya mda na wakakusanya wote yeye na Rhoda.
Baada ya wiki Moja matokeo yalitoka na kwa kidato cha kwanza mwanafunzi wa kwanza alikuwa Rhoda na kwa kidato cha tatu mwanafunzi Bora alikuwa Moses, basa likizo ilikuwa inaanza ila Moses na Rhoda walipendekezwa kwenda kanada pamoja na wanafunzi wengine waliofaulu , Badi safari iliwadia wakapelekwa airport na wakapanda ndege kwa kuwa wote ilikuwa ni mara yao ya Kwaza walifurahi sana na pia ndio wakati ulipokuwa mzuri kwa Moses kumwambia Rhoda yaliyomo moyoni mwake tena.
Walipofika kanada walikaribishwa vizuri sana na pia kila mtu alipewa chumba chake kwa sababu Moses na Rhoda walikuwa wanafahamiana kwa sababu walitoka shule Moja mda mwingi walikuwa wote, basi pamoja na kuwa wote Roda alikuwa na mipaka yake,Basi kila jion walipaswa kwenda disko ila kwa sababu Rhoda alikuwa ni mzuri Hadi kwenye disko wazungu walimsumbua, ndipo akawa anakimbilia Moses na Moses anamkwepa kweli Binti aliangaika sana, ndipo Moses akaendelea kumwomba Rhoda wawe wote na hatimaye akakubali.
Basi mwezi uliisha wakapaswa kurudi Tanzania Basi walipofika shuleni mahusiano yakaendelea wakati Moses yupo kidato cha nne na Rhoda kidato cha pili, wakiwa kwenye mahusiano hayo hatimaye Rhoda akawa mjamzito , baada ya kumwambia Moses kwa sababu walipendana wakaamua kutoa hiyo mimba, basi wakaendelea na maisha kama kawaida hatimaye Moses akamaliza kidato cha nne tena akachaguliwa kidato cha tano na sita shule hiyo hiyo kwa sababu Ile shule ilikuwa na madarasa kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita.
Basi Moses akawa kidato cha tano na Rhoda kidato cha tatu katika mahusiano yao Rhoda akabeba ujauzito mwingine wakashauliana na mwenzake namna ya kufanya wakaamua kutoa tena ,Basi wakaendelea na masomo, Moses akiwa kidato cha sita Rhoda kidato cha nne, Rhoda akutangulia kumaliza na baadae akafuata Moses na matokeo ya Rhoda yalikuwa ni mazuri mno pia na matokeo ya Moses na yeye alifaulu vizuri kidato cha sita,basi Rhoda alipaswa kuendelea kwenye shule hiyo walipanga hivyo kusudi na Moses aje kusoma chuo pale karibu na shule anayosomea Rhoda.
Rhoda akiwa kidato cha tano na Moses alikuwa chuo kikuu mwaka wa kwanza,kwa sababu waalimu waliwaamini sana Rhoda hata alipokuwa anatoka nje ya shule walikuwa hawana wasiwasi naye, kwa sababu Moses alikuwa na mkopo asilimia wote walishirikiana kutumia mkopo huo, inagwa baba yake Rhoda alikuwa na pesa nyingi sana ,kwa hiyo Moses akiwa chuo kikuu mwaka wa tatu Rhoda alikuwa mwaka wa kwanza kwenye chuo hicho hicho na waliishi kama baba na Mama chuoni, kwa hiyo Rhoda alibeba ujauzito mwingine mara ya tatu na wenyewe wakaamua kutoa, kwa hiyo mimba zilitolewa tatu.
Moses alimaliza chuo akaajiliwa Arusha na wakahaidiana kuoana na baadae na Rhoda akamaliza chuo akaajiliwa singida na wote wakawa wanafanya kazi na wanaopenda sana, ila kwa sababu ya Rhoda kutoa mimba mara kwa mara kijana alifikiri kwamba je? Nikimuona ataweza kujifungua? Kwa hiyo kijana akaamua kuoa kwa Siri na ndoa ikafungwa kanisani ila Kuna mtu alimwambia Rhoda kuhusu kufunga ndoa
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jamvini Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1313
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki. Soma Zaidi...
Hadithi za alif lela u lela
Haya ni masimulizi ya Hadithi za alif lela u lela Soma Zaidi...
USALITI (sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara. Soma Zaidi...
Hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha Soma Zaidi...
Chemsha bongo na bongoclass
Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Mama mchoyo na mwehu, kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu alichukua ule mkate akawapstia watoto wa yule mama wakiwa wanatoka shule kwa hiyo tutaona kilichotokea kwa wale watoto. Soma Zaidi...
Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambao walipoteana katika hali za kukimbizwa na wazazi Ili waweze kutimiza ndoto zao na siku wakakutana wakiwa watu wazima. Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)
Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, tunajua kuwa mama yake na binti alimtorisha yule binti mbali kabisa ila kijana naye aliamua kutoroka na kumfuata binti mfalme na hatimaye akampata alipo. Soma Zaidi...