Ni nani kama mama

Nani kama mama? Hadithi hii itakufunza umuhimu wa kuwa muwazi kuhusu familia yako.

Binti mmoja alizaliwa na kulelewa na Mama ambaye ni kichaa wale wakuzunguka na kuokota vitu barabarani, pamoja na ukichaa wake lakini yule mama alimlea vizuri binti yake akimpa chakula mpaka alipofikia umri wa kwenda shule. Kwa bahati nzuri yule binti alipata msamaria mwema ambaye alimsomesha, ingawa yule msamaria mwema alijaribu kumchukua yule Mama na kukaa naye lakini haikusaidia.
 
 
Kila aliporudishwa nyumbani siku mbili alirudi mtaani kuokota makopo na kula matakataka. Pamoja na ukichaa wake lakini kila siku ilikuwa ni lazima kwenda kwenye ile nyumba alikokuwa akilelewa binti yake kumsalimia na kila siku alikuwa akibeba chakula kwaajili ya binti yake.
 
 
Ili binti yule ale kile chakula illibidi kila siku kumuwekea chakula kizuri kwenye mfuko na pale alipokuwa akiomba basi walimpa kile chakula na yeye kabla ya kula alimletea binti yake. Maisha yaliendelea hivyo mpaka binti alipoenda chuo ndipo Mama alibaki mpweke akizunguka zunguka tu mtaani. Kule chuoni binti alifanya vizuri na alipomaliza chuo alifanikiwa kupata mchumba.
Alirudi kumtambulisha kwa wale wazazi waliomlea, lakini chakushangaza tusiku aliyorudi kumtambulisha mchumba wake na Mama yake alikuepo. kwa uoga na aibu aligoma kabisa kumtambulisha, ingawa yule mama alimng'ang'ania lakini alidanganya kuwa ni kichaa tu ambaye alizoea kumpa zawadi. Siku iliisha na mipango ya harusi ikafanyika, baada ya miezi mitatu ikafanyika harudi kubwa na ya kifahari.
 
 
Wakiwa katikati ya sherehe binti alishangaa kumuona Mama yake anaingia akiwa maevaa nguo zake chafu vilevile, Mama alisogea mpaka mbele watu wakimshangaa akatoa mfuko wake wa chakula na kumkabidhi binti yake ili ale. Binti aliukataa na kuanza kupiga kelele lakini kabla hajafanya chochote Mume wake aliuchukua ule mfuko na kuufungua kisha kuanza kukila kile chakula.
 
 
Watu wote walishtuka na kuanza kushangaa, lakini yule bwana harusi alichukua Mic na kusema. Huyu ndiye Mama mkwe wangu, Mama mzaa chema. Najua mnamshangaa na hali yake lakini kwa hali hii hii ndiyo alimza na kumlea mke wangu na ndiye atakuwa Bibi wa watoto wangu" Kila mtu alibaki kushangaa hata yule binti alishangaa huku machozi ya kimtoka, yule kijana alimgeukia mkewe.
 
 
"Najua sababau za wewe kuficha lakini unapaswa kutambua kuwa nakupenda na nampenda Mama yako kama vile ninavyompenda Mama yangu. Ulimwengu mzima utamuona kichaa lakini yeye ndiye aliyekuzaa na kukufanya uwe hivi leo. Unavyoniona hivi Baba yangu alinizaa na kunitelekeza, pamoja na pesa zake akili zake lakini alinitelekeza, sasa hembu jiulize kichaa ni nani kati ya mwanaume aliyetelekeza mwanae au Mama kama huyu ambaye mpaka leo anajua bado ni mtoto na anakujali kwa chakula?"
 
 
Ukumbi mzima uliibuka kwa vifijo, watu wakishangilia biti akiwa anatokwa na machozi alimkumbatia Mama yake, alichukua kile chakula na wote wakaanza kukila. Yule kijana ndiyo alimualika kwani siku aliyoenda kutambulishwa na kumuona alihisi kitu hivyo akaamua kufuatilia mpaka alipoujua ukweli. Alijua sababu ya mchumba wake kuficha lakini alitaka ulimwengu mzima kujua kuwa hajali na anampenda bila kujali historia yake.
 
HAKUNA KAMA MAMA, UPENDO WAKE HAUNUNULIWI WALA HAUPUNGUI USICHOKE KUMUAMBIA NAMNA UNAVYOMPENDA.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Emmanueli image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jamvini Main: Burudani File: Download PDF Views 489

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Hadithi ya Binti mfalme

Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na

Soma Zaidi...
Usichofahamu kuhusu mazoezi

Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo hufahamu kuhusu mazoezi,ni mambo ambayo utokea au no matokeo mazuri kwa watu wanaofanya sana mazoezi.

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano, baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kuona udhaifu wake kwamba anapenda sana mali.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tano)

Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya Nimlaumu nani ambapo juma anapanga na madaktari wanaopima DNA ili kuweza kutambua kwamba mtu mimba ni ya kwake na sio ya Frank kwa hiyo tuendelee kusikiliza mpaka tutakapoona mimba itakuwa ya Frank au juma.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI part 1

Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku

Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)

Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini.

Soma Zaidi...
Mahusiano ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake.

Soma Zaidi...
Kila kitu ambacho wanaume wanatakiwa kufahamu kuhusu wanawake.

Hii ni siri kubwa kuhusu wanawake. Hapa utajifunza jinsi ya kumfanya mwanamke asikuache.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI (sehemu ya sita)

Post inahusu zaidi hadithi ya NIMLAUMU NANI ambayo ni sehemu ya sita, katika kipengele hiki tunaenda kumwona msichana Amina anapambana na hatimaye anafunga ndoa ya kiserikali na Frank

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, kuhusu hadithi hii ni pale Jackie anaandikiwa barua na Julius ili apotezwe akili na wavulana wengine kwa sababu Jackie aliwapita darasani.

Soma Zaidi...