Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi


image


Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi.


Hasara za wivu na kutokuwa wazi.

1. Palikuwepo na wasichana wawili marafiki sana na waliofahamika pia kwa wazazi wao kuwa ni marafiki majina ya wasichana hao ni lisa na Lina ,urafiki wao ulitokana na wazazi wao waliishi sehemu moja na watoto hao walikua wanapendana kwa sababu ya wazazi wao pia walikuwa marafiki.

 

 

 

2.Watoto lina na Lisa wakiwa na miaka mitano walipelekwa kuanza chekechea walipelekwa na mama Lisa kuandikishwa kwa sababu ya kuzoeaana lina hakuona shida kwamba amepelekwa na mama Lisa shule kwa sababu alimwona kama mama yake pia, kwa hiyo mama Lisa aliwaandikisha na akawaacha pale shule na wakati wa kuondoka waliweza kurudi nyumbani kwa sababu hapakuwa mbali.

 

 

 

 

3. Siku zilienda na watoto hao wakawa wanasoma shule na matokeo yao yalikuwa mazuri mno na walikuwa hawaachani kila sehemu ukimwona lina kuna Lisa,na waalimu waliwapenda sana kwa sababu ya urafiki wao, nidhamu na pia ufaulu wao na kwa sababu walikuwa wadogo hawakuona shida kuishi na kupendana na kusaidiana katika kila kitu hasa kusoma pamoja na kucheza pamoja.

 

 

 

 

 

4. Basi watoto hao walipofika darasa la sita wakaanza kukua kimwili na kuanza kuwa na hisia hali ambayo iliwafanya kuwa tofauti kidogo kwa sababu palikuwepo na wanachuo wa mazoezi yaani kwa kitaalamu huitwa wanachuo wa field, yaani wale waliokuja kufanya mazoezi shuleni, mmoja kati yao akaanza mahusiano na Lisa ila Lisa hakumwambia lina na lina aliona kila kitu kinachoendelea kwa hiyo Lisa akapunguza kutembea na lina kwa sababu akihofu anaweza kumwambia mama yake.

 

 

 

 

5. Siku zikaendelea na Lisa akafanya mtihani akawa mtoto wa thelathini kati ya mia moja na siku zote alikuwa mtoto wa kwanza au wa pili walikuwa wanapisha na lina ,ila lina siku hiyo akawa wa kwanza mama Lisa akashangaa sana na alikuwa ameshashutuka kwa sababu Lisa alikuwa hana mahusiano mazuri na lina na siku hizo walikuwa hawasomi wala kucheza wote kama mwanzo, basi mama Lisa akaamua kwenda shule kwa waalimu kuuliza waalimu wakamwambia aende kwa lina atapata jibu kamili na waalimu walijua kila kitu ndipo mama Lisa akaenda kwa mama lina kupata jibu kamili.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha. Soma Zaidi...

image Hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hati.a ya kijana mchonganishi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Jaribio la kwanza la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Aladini katika pango la utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...