NI ZIPI KAZI ZA PROTINI MWILINI?


image


Makala hii inakwenda kukuletea kazi kuu za protini na vyakula vya protini katika miili yetu. Mkala hii itakusaiidia kujuwa namna ya kupangilia lishe yako kiusalama zaidi baada ya kujuwa kazi za protini katika miili yetu.


KAZI ZAPROTINI NA VYAKULA VYA PROTINI MWILINI

Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini. Kazi za protini mwilini:- Kujenga mwili; Kupona kwa vidonda na majeraha Kutengeneza antibody (kinga za mwili) Kutengeneza hemoglobin (chembechembe zaseli nyekundu za damu) Kutengeneza enzymes zinatumika katika kumeng;enya chakula Kutengeneza homoni Kuthibiti kichakati na shughuli za ndani ya seli Huhusika katika kutengeneza tishu (nyama na misuli) ndani ya mwili Nywele, kope, nyusi, vinyweleo na kucha hutokana na rotini  

 

1. Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.  

 

2. Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.  

 

3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.  

 

4. Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.  

 

5. Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.  

 

6. Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha.  



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image je ni vipi vyakula vyenye protini kwa wingi?
Makala hii iatakuletea aina kuu tano za vywkula vyenye protini nyingi zaidi. Kama ulikuwa unajiuliza kuwa ni vyakula ipi hasa vinaweza kukupatia protini kwa wingi ni vipi, makala hii ndio majibu yako kwa swali hilo. Soma Zaidi...

image Nini maana ya protini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini Soma Zaidi...

image Vyakula vya vitamin D
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin D Soma Zaidi...

image Fahamu kuhusu vitamini C na kazi zake
Makala hii itakujulisha kazi kuu za vitamini C mwilini. Hapa pia utatambuwa ni kwa nini tunahitaji vitamini C na wapi tutavipata Soma Zaidi...

image Kazi kuu tatu za vitamini C mwilini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi kuu tatu za vitamini C Soma Zaidi...

image Vyakula vya protini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya protini Soma Zaidi...

image Faida za kula maini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maini Soma Zaidi...

image Virutubisho vya mwili
Posti hii inahusu zaidi virutubisho vya mwili, ni aina tano za vyakula ambayo ufanya kazi mbalimbali kwenye sehemu za mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

image Vyakula hatari kwa mwenye kisukari
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula hatari kwa mwenye kisukari Soma Zaidi...

image Hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito. Soma Zaidi...