2.UPUNGUFU WA VITAMINI
1.Upungufu wa vitamini A hupelekea kukauka kwa ngozi, uoni hafifu na kuathirika kwa koo na ngozi
2.Upungufu wa vitamin B1 hupelekea kukosa hamu ya kula, udhaifu wa miguu, kupungua kwa hisia kwenye neva kudhoofu kwa misuli na kuathirika kwa akili.
3.Upungufu wa Vitamin B2 hupelekea kupata ugonjwa wa pellagra yaani vidonda vya mdomo na ulimi, ukuaji hafifu, kupasuka kwa nbgozi hasa sehemu za sikio na pua.
4.Upungufu wa Vitamin B12 husababisha matatizo katika uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu. Na kusababisha aina ya ugonjwa wa anaemia
5.Upungufu wa vitamini C husababisha kutoka damu kwenye mafinzi, kuchelewa kupona kwa majeraha, maumivu ya viungo na kudhoofu kwa mishipa ya damu hasa kwenye ngozi.
6.Upungufu wa vitamin D husababisha kuleta matege.
7.Upungufu wa vitamin k husababisha kuchelewa kuganda kwa damu kwenye jeraha

UPUNGUFU WA MAJI
Maji yakipungua mwilini yanaweza kuleta madhara makubwa hata kifo. Hali hii ikitokea kuwa maji yamepunguwa kwa kiasi kikubwa sana kwa haraka mgonjwa ataongezewa maji. Hili linajulukana sana. Ila nataka kuongezea maarifa hapa kuhusu kupunguwa kwa kawaida nini adhari zake kwenye mwili.

Endapo maji yakipungua kwa hali hya kawaida mtua ataanza kuhisi kiu. Pia maji yanaweza kusababisha maumivu ya kichwa. Choo kuwa kigumu na hatimaye kutoka na damu kwa sababu ya kuchubua kuta za haja kubwa. Mkojo kuwa mchache na kutokwa na jasho kwa kiasi kidogo sana. Mtu anaweza kuhisi kuchanganyikiwa na kuhisi kama kichwa chaje ni chepesi sana. Pia athari nyingine unaweza kuziona kwenye ngozi pale ngozi inapopoteza uhalisia wake wa kujikunja na kusinyaa. Ngozi inakuwa ngumu na imekauka.