Ujue ugonjwa wa tauni
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa tauni ambao kwa kitaalamu huitwa plague ni Ugonjwa unaosababishwa na wadudu ambao huitwa kitaalamu huitwa yersinia pestis ambao ukaa ndani ya panya.
Ujue ugonjwa wa tauni.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kuwa ugonjwa wa tauni ni Ugonjwa unaosababishwa na wadudu wanaoitwa kwa kitaalamu yersinia pestis wadudu hawa uishi ndani ya panya na viroboto ambao ufyonza damu kwenye panya ufyonza pamoja na wadudu hawa, na pia viroboto uweza kung'ata binadamu na kuingiza wadudu wanaoitwa yersinia pestis ambao usababisha ugonjwa wa tauni ambao uwatesa watu wengi na kusababisha madhara mbalimbali kwenye jamii.
2. Ugonjwa huu umeenea katika sehemu mbalimbali za Afrika, Asia, na Amerika inavyokadiriwa ni kuwa kuanzia mwaka elfu moja mia tisa tisini na nne mpaka elfu mbili na tatu watu elf mbili mia nane na hamsini wameripotiwa na shirika la WHO, asilimia tisini waliokuwa wameugua ugonjwa huu ni waafrika ukilinganisha na mataifa mengine ,kwa hiyo na Tanzania mpaka sasa kuna sehemu ambapo ugonjwa bado upo na unaowasumbua watu sehemu ambazo zinapatwa na Ugonjwa huu ni sehemu zenye unyevunyevu kwa wingi ukilinganisha na sehemu nyingine.
3. Ugonjwa huu kwa ujumla unaweza kutibiwa na kupotea kabisa kwenye jamii kwa sababu watu wanapaswa kuzingatia usafi ili kuepuka kuwepo kwa panya ambao wanatunza hawa wadudu na pia kwenye kipindi cha mavuno watu wanapaswa kuwa makini ili kuweza kuepuka kuongezeka kwa panya ambao ndio chanzo cha Ugonjwa huu,kwa wakati mwingine dalili za Ugonjwa huu uchanganya watu na kuwa kama Dalili za kawaida kama vile homa na mwili kuishiwa nguvu ila zinabadilika kadri ugonjwa inavyoongezeka.
4.Dalili nyingine ambazo zinaweza kujitokeza ni kama vile miwasho kwenye mwili, maumivu ya kichwa ambayo yanaweza kuanza taratibu na ukitumia dawa yanaisha na baadae yanaanza tena maumivu kwenye mwili, kichefuchefu na kutapika, kuwepo kwa vipele kwenye kwapa, na Dalli hizi utofautiana na kuongezeka kadri siku na mda unavyoenda.
5.Kwa hiyo jamii nzima inapaswa kuelimishwa kuhusu Ugonjwa huu na kujua Dalili zake kwa sababu wakati mwingine Dalili hizi ufanana na magonjwa mengine ya kawaida kwa hiyo ni lazima kuzijua kwa uhakika ili kuweza kupata huduma sahihi na kuepukana na madhara mengine makubwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitabu cha Afya π2 Kitau cha Fiqh π3 Simulizi za Hadithi Audio π4 Madrasa kiganjani π5 ai web app π6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Kujitenga na jamii: Je, ni ishara ya unyogovu?
βKatika ulimwengu wa kisasa uliounganishwa kidijitali, kitendawili cha upweke katikati ya umati kimezidi kuwa kikubwa. Makala haya yanachunguza uhusiano wa kina kati ya tabia ya kujitenga na jamii (social withdrawal) na afya ya akili, hususan unyogovu. Tunachambua dalili, sababu za kisaikolojia, na tofauti kati ya hitaji la muda mfupi la upweke na ugonjwa wa unyogovu wa kitabibu, huku tukitoa mwongozo wa hatua za kuchukua ili kurejesha ustawi wa kijamii
Soma Zaidi...Dalili za kifua kikuu kwa watoto.
Posti hii inahusu zaidi dalili za kifua kikuu kwa watoto,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto pindi wanapopata Maambukizi ya kifua kikuu.
Soma Zaidi...Kupunguzwa kwa kiwosi cha lehemu (Cholesterol) mwilini.
Lehemu (cholesterol) ni kiambato muhimu katika mwili wa binadamu, lakini kiwango chake kinapozidi kiasi kinachohitajika, huwa hatari kubwa kwa mfumo wa moyo na mishipa ya damu. Makala hii inatoa uchambuzi wa kitaalamu kuhusu taratibu za kupunguza lehemu mbaya (LDL), umuhimu wa uwiano wa lehemu nzuri (HDL), na mikakati ya kisayansi ya kudhibiti lehemu kupitia lishe, mazoezi, na dawa.
Soma Zaidi...Dalili na Ishara za mawe kwenye figo
Mawe kwenye figo yana sababu nyingi na yanaweza kuathiri sehemu yoyote ya njia yako ya mkojo kutoka kwa figo hadi kibofu chako.
Soma Zaidi...Athari za kula vyakula vyenye sukari nyingi kila siku.
Katika ulimwengu wa sasa, sukari imekuwa kiungo kikuu katika vyakula vingi vilivyosindikwa, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa magonjwa yasiyoambukiza. Makala haya yanachambua athari za muda mrefu za ulaji wa sukari nyingi, ikizingatia afya ya moyo, uzito wa mwili, na utendaji wa kimetaboliki, huku ikitoa mikakati ya kitaalamu ya kupunguza matumizi ya sukari kwa maisha marefu na yenye tija.
Soma Zaidi...Kutokwa na jasho kupita kiasi wakati wa kulala: Chanzo chake.
kuamka katikati ya usiku ukajikuta nguo zako au mashuka yameloa jasho hadi unalazimika kubadilisha, licha ya kwamba chumba kina ubaridi wa kutosha? Hali hii kitaalamu inajulikana kama Night Sweats. Makala haya yanachambua vyanzo mbalimbali vinavyosababisha tatizo hili, kuanzia sababu za kawaida za kimazingira hadi viashiria vya matatizo ya kiafya yanayohitaji ushauri wa daktari.
Soma Zaidi...