Hatua tatu anazozipitia mgonjwa wa tauni

Hatua tatu anazozipitia mgonjwa wa tauni

Posti hii inahusu zaidi njia au hatua tatu muhimu anazopitia Mgonjwa wa gauni, kuanzia kwa Maambukizi mpaka kwenye hatua ya mwisho hasa kama Ugonjwa huu haujatibiwa mapema.

Hatua tatu anazozipitia Mgonjwa wa tauni.

1.Hatua ya kwanza ni pale kiroboto mwenye Maambukizi ambaye ameyapata kutoka kwa panya anamngata mtu na kuingiza wadudu ambao kwa kitaalamu huitwa yersinia pestis, wadudu hao hawapiti kwenye mfumo wa mzunguko wa damu bali upitia kwenye lymphatic na kushambulia limfu node za kwenye kwapa, kwenye shingo na sehemu mbalimbali ambazo zina limfu.

 

2.Pia hizo limfu zinakuwa na Maambukizi hali ambayo ufanya hizo limfu kubwa na ma upele na na upele hayo utoa usaha ambapo Usababisha maumivu makali kwa mgonjwa kwa hiyo Dalili hii kwa watu wengine ushindwa kutambuliwa mapema kama ni tauni au nini kwa hiyo matibabu ulenga zaidi Dalili hali ambayo Usababisha kushindwa kupona na kusababisha hatua nyingine kama tutakavyoona hapo chini.

 

3.Baada ya Maambukizi kuingia kwenye node uingiliana na mzunguko wa damu hii hatua ya wadudu kuingia kwenye mzunguko wa damu kwa kitaalamu huitwa septicaemia, kwa hiyo kwenye damu wadudu ushambulia mishipa ya damu na kufanya mzunguko wa damu kuwa wa shida hali ambayo Usababisha kupasuka kwa mishipa ya damu na kusababisha kuvuja damu kila mahali.

 

4.Ugonjwa ukifikia kwenye hali hii wengine udhani kwamba ni ebola na kuanza kuwa tenga na kuwakimbia wagonjwa kwa hiyo ni vizuri kabisa kuhakikisha kuwa dalili za Ugonjwa huu zinatambulika mapema na katika hatua hii matibabu yanaweza kufanya kazi.

 

5.hatua ya tatu ni pale ambapo wadudu wanasambaa kwenye mapafu ambapo kwa kitaalamu huitwa pneumonic, kwa hiyo wadudu wakizidi kwenye damu uhamia kwenye mapafu na kuweza kuyashambulia, na katika hatua hii mgonjwa anapumua vibaya vibaya na kwa hatua hii mgonjwa anaweza kuambukiza kwa hiyo ni vizuri mgonjwa akifikia hatua hii akaweza kutunzwa vizuri na sehemu yenye hewa.

 

6 . Kwatika hatua hii ni vigumu kwa mgonjwa kupona kwa sababu Maambukizi yanakuwa yamesambaa sehemu mbalimbali kwenye mwili, kwenye damu na mapafu pia na sehemu nyingine pia ushambulia kwa hiyo tunapaswa kujua Dalili hizi ili kuweza kupambana na ugonjwa huu.

 

7.pia jamii inapaswa kupewa elimu kuhusu Dalili za Ugonjwa huu na kuweza kutambua Dalili zake mapema ili kuweza kupata matibabu ipasavyo kwa sababu kuna dawa ambazo zinatumika dawa zenyewe ni kama ifuatavyo, dawa za antibiotics kama vile streptomycin, Tetracycline, doxycycline ambazo utumika na kuponyesha Ugonjwa huu.

 

8.Dawa hizi utumika kama ifuatavyo, kwa kuanza na streptomycin tumia milligram 30, vidonge viwili kwa siku tatu, Tetracycline tumia milligram kuanzia mia mbili hamsini mpaka mia tano mara nne kwa siku kumi, na doxycycline vinatumika kwa siku saba hizi dawa zinapaswa kutumika kwa maagizo ya wataalamu wa afya sio kutumia kiholela tu.

 

9.pia tunapaswa kujua kuwa ugonjwa huu upo na unatibika kwa hiyo mila na desturi zisizofaa tuziache ili kuweza kuokoa maisha ya watu

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 2335

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Dalili za fangasi wa kucha.

Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili,sababu za Hatari,na namna ya kujizuia na fangasi wa kucha.

Soma Zaidi...
Namna ya kuepuka Ugonjwa wa ngiri.

Posti hii inahusu zaidi namna au njia za kuepuka na Ugonjwa huu wa ngiri ambao uleta madhara kwa watoto, vijana na watu wazima, kwa hiyo ili tuweze janga hili ni lazima tufanye yafuatayo.

Soma Zaidi...
Faida za Kunywa Maji Mengi Kila Siku

​Maji ni kiini cha uhai na yanachukua zaidi ya nusu ya uzito wa mwili wa binadamu. Post hii inaangazia umuhimu wa kunywa maji ya kutosha kila siku, jinsi yanavyosaidia utendaji kazi wa viungo vya mwili, na vidokezo vya kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha

Soma Zaidi...
Fahamu Ugonjwa wa uchovu sugu.

Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa uchovu sugu ni ugonjwa tata unaoonyeshwa na uchovu mwingi ambao hauwezi kuelezewa na hali yoyote ya matibabu. Uchovu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa shughuli za kimwili au kiakili, lakini haiboresha kwa kupumzika

Soma Zaidi...
Sababu na Chanzo cha vidonda vya tumbo

Zijuwe sababu za kutokea kwa vidonda vya tumbo. Sababu kuu za vidonda vya tumbo hizi hapa

Soma Zaidi...
Dalili za upungufu wa maji mwilini.

Upungufu wa maji mwilini hutokea unapotumia au kupoteza Majimaji mengi zaidi ya unayonywa, na mwili wako hauna maji ya kutosha na Majimaji mengine ya kufanya kazi zake za kawaida. Usipochukua nafasi ya Vimiminika vilivyopotea, utapungukiwa na maji.

Soma Zaidi...