Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya dalili za gonorrhea
Dalilii za gonorrhea
Gonorrhea au gonoria ni moja kati ya magonjwa yanayoenezwa kupitia ngono. Huweza kusababishwa na bakteria na kuathiri wanaume na wanawake. Kuweza kuathiri mdomo, koo, mkundu na sehemu za siri kwa wanaume na wanawake. Huweza kuambukizwa kwa kupitia ngono ya mdomo, ngono ya ukeni ama kwenye mkundu. Kwa watoto huweza kuathiri macho. Gonorrhea (gonoria) huambukizwa kutoka kwa mama kuja kwa mtoto wakati wa kujifunguwa.
Dalili za gonoria (gonorrhea) zinaweza kuchelewa kuonekana kwa wanawake kuliko kwa wanaume. Wapo wengine hawaonyeshi dalili yeyote ile hadi hali itakapokuwa ni mbaya zaidi. Kwa mara nyingi dalili za gonoria (gonorrhea) huonekana kuanzia siku 2 mpaka 7 baada ya kuambukizwa. Na kwa wanawake inaweza kuchelewa zaidi hadi mwezi.
Ni zipi dalili za gonoria (gonorrhea)?
Dalili za gonoria (gonorrhea) unaweza kuwa na dalili tofautitofauti kulingana na jinsia. Dalili kwa wanawae na kwa wanaume zinaweza kutofautiana kulingana na maumbile ya jinsia hizi. Muda wa kutokea dalili hizi pia hutofautiana. Pia huweza kuahiri maeneo mengi mwilini.
Dalili za gonorrhea kwa wanaume:-
1.Maumivu wakati wa kukojoa
2.Kutokwa na majimaji kama usaha kwenye uume.
3.Kuvimba pamoja na maumivu ya korodani.
Dalili za gonorrhea kwa wanawake
1.Kutokwa na uchafu sehemu za siri
2.Maumivu makali ya maeneo ya nyonga
3.Maumivu makali wakati wa kukojoa
4.Kutokwa na damu kabla ya hedhi na baada ya hedhi
Dalili za gonoria (gonorrhea) katika maeneo mengine ya mwili:
1.Maumivu ya mkundu, na kutokwa na kama kinyesi pamoja na maumivu ya tumbo na mvurugiko.
2.Maumivu ya macho, kushindwa kuvumilia mwanga mkali, na macho kutoa kama usaha
3.Vidonga vya koo na kuvimba kwa tezi na lumph kwenye shingo
4.Maumivu ya viungio pamoja na kuwa na joto.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Kwa nini unapata maumivu makali wakati wa kuingia hedhi, je unajuwa sababu za maumivu makali ya tumbo la chago.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yatokanayo na fangasi
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanaume
Soma Zaidi...Swali langu: Ukiwa na areji , afu kupata muwasho korodani unapo jikuna unga kutoka nayo fangasi?
Soma Zaidi...ATHARI ZA KUTOTIBIWA VIDONDA VYA TUMBO Kuachwa kwa vidonda vya tumbo bila kutibiwa, vinaweza kusababisha: Kutokwa na damu kwa ndani.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa kusinyaa kwa Misuli. Ni maradhi yanayopelekea uzalishwaji hafifu wa misuli, hivyo kupelekea misuli kukosa protini, kushunwa kukuwa na kusinyaa.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha ishara na dalili za Saratani ya utumbo mdogo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo unapaswa kufanya kama una tatizo la kiungulia.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi njia za kumgundua mgonjwa wa kaswende, njia hizi utumika baada ya kuongea na mgonjwa kuhusu maisha yake hasa kujamiiana na watu mbalimbali.
Soma Zaidi...UGONJWA WA GONORIA NA DALILI ZAKE (GONORRHEA)Gonoria (gonorrhea) ni katika maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.
Soma Zaidi...