Posti hii inahusu zaidi mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza kiwango cha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza, kwa hiyo zifuatazo ni mbinu ambazo zinapaswa kutumika ili kupunguza kiwango cha magonjwa ya kuambukiza.
1.kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa kuna magonjwa mengi ya kuambukiza ingawa tunajaribu kuyatibu ila si yote yanaweza kuisha ila kuna njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza kiwango cha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza.njia zenyewe ni kama ifuatavyo.
2.Kuangalia mazingira.
Kwanza kabisa mazingira ya watu yanapaswa kuangaliwa, yaani maisha ya watu kwa ujumla kwa mfano usafi pakiwepo choo, maji yaliyochenshwa na kuchujwa na mambo mengine ambayo yanaweza kuwa chanzo cha uchafu.
2. Pia kuangalia chakula kinachotumiwa na watu wa kwenye mazingira kama kinaweza kuwasaidia watu kuweza kuwa na kinga ya kupambana dhidi ya magonjwa na jinsi ya kutumia chakula kama ni sahihi.
3. Vile vile tunapaswa kuangalia kama kuna mtu yeyote kwenye jamii ana Dalili za ugonjwa tunapaswa kukusanya sampuli na kuzipeleka maabara ili kutambua tatizo lililopo na kuweza kutatua tatizo kwenye mazingira.
4. Pia kama kuna Ugonjwa ambao umekidhiri kwenye jamii husika ambao unaleta shida na matatizo makubwa kwa jamii hiyo chanjo ni lazima ili kuweza kutokomeza Tatizo lililopo.
5. Tibu magonjwa yaliyomo kwenye mazingira kwa kutumia dawa mbalimbali ambazo zimeagizwa na wahudumu wa afya baada ya kugundua ugonjwa uliopo kwenye mazingira.
6 . Pia elimu inapaswa kutolewa kwa jamii baada ya kuangalia mazingira, chakula kinachotumiwa na watu waliopo kwenye mazingira husika ili kuhakikisha kuwa wanatumia chakula kwa kuzingatia mlo kamili na kuepuka utapia mlo kwa watoto na watu wazima.
7. Kuhakikisha kubwa mazingira yanakuwa masafi kwa kukata nyasi ndefu, kufukia mashimo,kuchoma takataka mbalimbali zilizoizunguka nyumba na kuhakikisha kuwa watu wamefundishwa namna ya kutunza mazingira na pia kuhakikisha kubwa wanachemsha maji na kuchuja kabla ya kunywa.
8. Kuhakikisha mazingira hayana wadudu wanaosababisha magonjwa, wadudu kama vile chawa, mbu, viroboto, kunguni na wengine wengi ambao ukaa kwenye mazingira ya watu, kama kuna dawa wanaweza kuuawa ili kupunguza Magonjwa.
9. Pia kuhakikisha watu wanapata mahitaji ya msingi ya maisha kama vile makazi, mavazi na chakula pia wapewe na dawa kama kuna Magonjwa vile vile na wale ambao hawajiwezi kabisa wanapaswa kutafutiwa huduma za kijamii kwa kupitia viongozi wa serikali.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake
Soma Zaidi...HOMA YA DENGUEHoma ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu.
Soma Zaidi...Hawa ni fangasi ambao wanashambulia sana kwenye kucha za vidole vya mikonobna miguu.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa ambapo mgonjwa hushindwa kupumua vizuri na hupelekea matatizo ya kudumu kama haujatibiwa mapema.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa macho, ni ugonjwa ambao ushambulia zaidi sehemu za nje za macho ambazo kwa kawaida uitwa conjunctiva na cornea hizi sehemu zikipata maambukizi zisipotibiwa mapema uweza kusababisha upofu kwa mgonjwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa ukoma ni Ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayejulika kama mycobacterium leprae.
Soma Zaidi...Zijuwe sababu za kuumwa nankichwa upande mmoja wa kichwa.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutokea kwa maumivu ya jino
Soma Zaidi...Tezi dume ambayo haijashuka si ya kawaida kwa ujumla, lakini ni ya kawaida kwa wavulana waliozaliwa kabla ya wakati.na muda mwingine zikipanda tumboni huwa hazishuki kabisa kwenye korodani.
Soma Zaidi...