Swala ya tarawehe jinsi ya kuiswali

Post hii itakwenda kukufundisha kuhusi swala ya tarawehe, faida zake na jinsi ya kuiswali.

5. Swala ya Tarawehe
Swala ya Tarawehe ni miongoni mwa Sunnah zilizokokotezwa. Swala hii huswaliwa katika mwezi wa Ramadhan tu wakati wowote kati ya kipindi baada ya swala ya Isha na kuingia kwa swala ya Alfajiri. Umuhimu wa swala hii umedhihiri katika Hadithi ifuatayo:

 


Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akisisitiza swala ya usiku katika mwezi wa kufunga (Ramadhani), bila ya kuifaradhisha kwao. Alikuwa akisema: Atakaye swali katika usiku wa mwezi wa kufunga, akiwa na imani na akitarajia malipo (kutoka kwa Allah (s.w), dhambi zake zilizotangulia husamehewa. (Muslim)

 


Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali Tarawehe katika sehemu ya pili ya usiku (katika wakati ule ule wa Tahajjud). Mtume (s.a.w) aliswali Tarawehe pamoja na masahaba katika jamaa siku tatu, kisha akaacha na akawa anaswalia nyumbani kwake kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:

 


‘Aysha (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikwenda msikitini usiku na akaswalisha Tarawehe na watu wakaswali naye. Asubuhi watu wakasimuliana habari hiyo. Mtume (s.a.w) siku ya pili alikwenda kuswalisha watu wakajaa msikitini. Alifanya hivyo hivyo siku ya tatu. Asubuhi siku ya nne watu wakapeana habari na wakajazana zaidi msikitini kwa ajili ya sw ala ya Tarawehe lakini Mtume (s.a.w) hakw enda

 

kuswalisha. Baadhi ya watu walisema kwa sauti “swalah”, lakini Mtume (s.a.w) hakwenda msikitini mpaka Alfajir. Alipomaliza sw ala ya Alfajir aliwakabili watu na kuwaeleza: “Jambo lenu halikuwa limefichikana kwangu, lakini nilichelea kuwa kama ningaliendelea mfululizo na swala hiyo ya Tarawehe huenda ingalifanywa kuwa ni faradhi kwenu na huenda m ungalishindw a kuitekeleza ”. (Muslim)

 


Pamoja na Hadithi hii, pia Mtume (s.a.w) aliwasisitiza Waislamu kuswali swala za Sunnah majumbani mwao na kuwahakikishia kuwa kufanya hivyo kuna malipo makubwa zaidi. Swala ya Tarawehe iliendelea kuswaliwa na kila mtu nyumbani kwake katika kipindi chote cha Mtume (s.a.w) na kipindi cha Khalifa wake wa kwanza (Abu Bakar). Khalifa wa pili, Umar bin Khattab, alianzisha tena kuswali swala ya Tarawehe kwa jamaa msikitini kama inavyoendelea mpaka hivi leo.

 


Idadi ya Rakaa za Swala ya Tarawehe

 


Kumekuwepo na maelezo tofauti kuhusiana na idadi ya rakaa za Swala ya tarawehe kutoka kwa wanazuoni tofauti. Lakini kutokana na Hadithi iliyosimuliwa na Mama Aysha (r.a) na kupokelewa na Maimamu wa Hadithi, Mtume (s.a.w) hakupata kuswali zaidi ya rakaa 11 katika mwezi wowote ule. Hadithi ya Jabir (r.a) iliyopokelewa na Ibnu Khuzaimah na Ib n Hibban, Mtume ameripotiwa kuswali rakaa nane za tarawehe na rakaa tatu za witri pamoja na Masahaba wake na kisha siku iliyofuatia akawa hakutoka kwenda kusalisha.

 


Ama kuhusiana na kuswali rakaa ishirini, ni kweli kuwa Khalifa Umar, Uthman na Ali (r.a) waliswali kwa rakaa hizo. Imamu Ibnu Hibban amesema kuwa mwanzoni ilikuwa ni rakaa kumi na moja isipokuwa kisomo (kisimamo) kilikuwa kirefu kiasi cha watu kuchoka. Hivyo baadaye ikaamuliwa kuwa idadi ya rakaa iongezwe na kisomo kipunguzwe na kuwa cha wastani ingawaje jambo hili halikuingiza Swala ya Witri, kutoka hapo kwenye rakaa 20 ilifika kwa badhi ya wengine akiwemo Imamu Malik hadi rakaa 36 ikiwa kisomo kimezidi kufupishwa. Iliyo sunnah ni kuswali tarawehe kwa rakaa 11-8 za kisimamo cha usiku cha kawaida na rakaa 3 za witri. Kwa kuwa mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur-an inahimizwa sana kuwa Waislamu wahitimishe Qur-an yote alau kwa kusoma juzuu moja kila siku. Tarawehe ni swala sawa na swala nyingine hivyo kusihi kwake kunafungamana na kupatikana khushui, masharti na nguzo zote za swala. Ama hizi tarawehe zinazoswaliwa katika misikiti mingi mbazo Imamu hupata sifa kwa kuswali mbio mbio pasipo na mazingatio wala utulivu ni kinyume kabisa na utaratibu wa swala. Watu wengi ambao huharakisha kumaliza swala ya tarawehe kwa kiasi cha kutokamilisha nguzo za swala hawapati malipo yoyote kutokana na swala zao. Bali kwa kuwa watu hawa wanaifanyia swala mchezo hapana cha kutarajia zaidi ya adhabu kali waliyoahidiwa na Allah (s.w):

 

“Basi adhabu itawathibitikia wanao swali, ambao wanapuuza swala zao”. (107:4-5)

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/15/Monday - 11:26:56 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 928


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Al-Arba-uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 5: kujiepusha na uzushi katika dini
Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini Soma Zaidi...

Zijuwe nguzo 17 za swala.
Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla. Soma Zaidi...

Swala ya tahiyatul masjidi yaani maamkizi ya msikitini, pamoja na swala za qabliya na baadiya
Post hii inakwenda kukujuza kuhusu swala za qabliya, baadiya na tahiyatul masjid. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 4: Uumbwaji wa mwanadamu
HAdithi hii itakufundisha namna ambavyo mwanadamu anapitia hatuwa mbalumbali tumboni mwa mama yake Soma Zaidi...

Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 2: Ujio wa Jibril kwa Mtume (s.a.w)
Hii ni hadithi ya pili katika kitabu cha Arbain Nawawiy Soma Zaidi...

Jinsi ya kuswali swala vitani
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika ilibkuswalibukiwa vitani. Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swwla ya dhuha na faida zake
Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Umuhimu wa swala yaani kuswali kwa mwanadamu
Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala. Soma Zaidi...

Ijuwe swala ya Tawbah na jinsi ya kuiswali
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya sinnah ya tawba. Soma Zaidi...